jimmyfoxxgongo
JF-Expert Member
- Jan 23, 2013
- 5,352
- 9,293
Mkuu naona bado hujaelewa kitu, nipo mwaka wa kwanza sasa nawezaje fanya hayo mambo? Pili am concerning with eye care professional. Sorry kwa kunielewa vibaya. Ndio tunasoma anatomy, boich, physio, micro na mengine mengi
Kawaida Taifod haipon kbsa
Bali wale wadudu hupungua na kuongezeka ukikaz upme uambiwe huna utakesha .
Mkuu hujanielewa kwanza nilitaka kujua hicho kipimo cha widal test unakifanya katika hospital zipi na unapewa majibu baada ya muda gani?
Mkuu widal test zipo za aina mbili:
1.Tile method hii huwa ni quick method na unaweza kuyapata majibu yako kwa muda mfupi tu.
Njia hii faida yake ni kwamba unapata majibu mapema sana lakini tatzo ni kwamba haina ubora katika dhana nzima ya kuupata ugonjwa.
Kuna uwezekano mkubwa wa kupewa majibu positive ilhali ni negative
2. Tube method hii ni njia ya pili.hii inachukua muda kidogo inakuwa ni zaid ya masaa 24 kwa sababu inahusisha incubation.
Ukilinganisha na njia ya kwanza hii ni bora zaidi kuliko ile ya juu ingawa hii pia inaweza kukupa majibu ambayo sio sahihi.
Njia sahihi ya kupima typhoid fever ni stool culture kwa ajili ya ku-isolate hawa wadudu wa typhoid hii haina shaka
Lakini pia mkuu kwa njia nilizokutajia hapo juu ukipimwa na ukaonekana widal test positive ukimaliza dawa hutakiwi kukurupuka tena kwenda kupima kwa sababu zile antibodies hubaki mwili kwa muda walau miez mitatu ndo zinaweza kuwa cleared.hapa daktari anatakiwa kujua historia ya mgonjwa vizuri.
Mkuu uliyesema wadudu hupungua tu sio kweli typhoid inapona vizuri kabisa bila tatzo ila ukutane na mtaalam tu
LT