Nina tatizo la umeme takribani wiki sasa nimeriporti TANESCO mpaka sasa tatizo halijatatuliwa

IT PROFESSIONAL

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
228
95
Wadau naandika Uzi huu tena kwa masikitiko makubwa,Nina tatizo la umeme takribani wiki sasa nimeriporti Tanesco mpaka sasa tatizo halijatatuliwa unaenda mpaka ofisini kwao unawaeleza wanakuambia mafundi wapo bize ,then watakuja inapita siku ya kwanza mpaka wiki tatizo bado mafundi hawajaja na tatizo halijatatuliwa.

Hivi naomba kuuliza kama mteja ninaporipoti tatizo inanihusu nini kuambiwa mafundi wapo bize na inanipa faidi gani kuambiwa hivyo wakati familia yangu inalala na giza?

Mimi binafsi nawaomba Waheshimiwa wenye dhamana ya utumbuaji ,tumbueni Tanesco Songea Maana hili jipu lishaiva,mimi nishamaliza kama kuna wadau wengine wana kero kama za kwangu watafunguka hapa chini.Asanteni
 
Hivi kwa nini mikoa mingine hawawaulizi wenzao Dodoma wanafanyaje kazi? Dodoma kwa kweli ni wasikivu 95% hiyo 5% tuseme ni matatizo ya kibinadam. Ila nao wasilewe sifa
 
Zipo njia nyingine nyingi mbadala za kujipatia umeme mfano: umeme wa jua, pesa ya bill ikusanye tafuta solar panel yako ya 200watts nunua power backup batteries pia mbona utasahau Tanesco. Monopoly lazima asumbuwe .
 
Wadau naandika Uzi huu tena kwa masikitiko makubwa,Nina tatizo la umeme takribani wiki sasa nimeriporti Tanesco mpaka sasa tatizo halijatatuliwa unaenda mpaka ofisini kwao unawaeleza wanakuambia mafundi wapo bize ,then watakuja inapita siku ya kwanza mpaka wiki tatizo bado mafundi hawajaja na tatizo halijatatuliwa.Hivi naomba kuuliza kama mteja ninaporipoti tatizo inanihusu nini kuambiwa mafundi wapo bize na inanipa faidi gani kuambiwa hivyo wakati familia yangu inalala na giza?
Mimi binafsi nawaomba Waheshimiwa wenye dhamana ya utumbuaji ,tumbueni Tanesco Songea Maana hili jipu lishaiva,mimi nishamaliza kama kuna wadau wengine wana kero kama za kwangu watafunguka hapa chini.Asanteni
Mkuu mara nyingi wale watu wa reception pale emergency ni wakuda sana.
We nenda ofisi zao halafu uwachimbe mkwara unaenda kuwashitaki kwa manager wao, au wakizingua pitiliza moja kwa moja mpaka ofisi ya manager eleza matatizo yako.

Umeme utawaka ndani ya masaa mawili tu
 
Mkuu naunga mkono hoja taneasco ni jipu kubwa aisee mm kuna kitu kinaitwa service change yaan hapa ndio tunapigiwa kweli kweli aisee
 
Juzi juzi Iringa kuna mtoto alikufa kwa kukanyaga nyaya za umeme zilizo anguka. Wakasingizia hawakupewa taarifa ila wananchi wanasema walitoa taarifa. Nilimuona Msemaji wao anajitapa kwa mbwembwe huku akionesha kwenye kitabu chao cha kumbukumbu za matukio ile taarifa haipo. Inavyo onekana kwa hawa jamaa taarifa ni inayotolewa pale unapofika ofisini kwao na kusaini kitabu chao. Ila kwa kutumia simu ni kama unajisumbua, watasema hawajapata taarifa.
 
Mimi nilishaenda ofisin kwao kutoa taarifa na reference number ninayo,watakapoanza kutumbuliwa wasije wakasema sikuwapa taarifa kila kitu ninacho.
 
Tatizo mita haikubari kuingiza umeme ,walikuja kucheki wakasema wanakuna mafundi wa mita now ni kama siku nne ,na nimewafuata ofisin kwao wakaniambia nisubiri mafundi wanakuja ,sasa imebaki stori kila ukipiga emergence wanakuambia tatizo wanalifahamu watakuja.
 
Mita yako inaanza na namba gani?
 
ngojenikuweni na subira gas imebgunduliwa tlillion12.7
itawanufaisha watanzania wote kma mnavyonufaika na madini..........
 
Ungewakatia mpunga kidogo mambo yanekuwa safi... Sasa hivi umeme ungekuwa unawaka waaa. Wahenga walishakwambia penye udhia penyeza rupia...
 
Back
Top Bottom