Nina tatizo la macho kuwasha kila ifikapo usiku

Nyanda lunduma

Senior Member
Apr 10, 2015
187
68
Habar wana jf,

Niende moja kwa moja kwenye maada yangu hapo juu , hilo tatizo la macho kila mara ifikapo usiku macho yangu huwasha sana na kusababisha nijikune na kupelekea mpaka kuwa mekundu, nimeenda Hospital na dawa kushauri vizuri dawa za kutumia ila mpaka sasa bado inasumbua.

Nimekuja kwenu wana jf kupata msaada mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali;

Tatizo limekuanza lini?

Una umri gani?

Usiku unalala kwenye chumba chenye mwanga wa kutosha?

Matumizi ya simu yakoje, unavaa miwani wakati wa kusoma?

Je hali hiyo ipo mchana pia?

Unakula matunda na mbogamboga?

Umewahi kutumia dawa ya macho bila maelekezo ya Dr.?

Yanatoa tongotongo?

Jibu hayo maswali iwe rahisi mtu kukupa msaada.
 
Mkuu Mimi pia nilikua na changamoto hiyo siku chache tu zilizopita

Sema Mimi nilikua pia nawashawa kwenye viganja vya mikono

Nikaenda hospital, dokta akaniambia inaweza ikawa Ni allergy so akanipatia dawa na hiyo hali ikapotea kabisa
 
Hilo swala la kiroho tafuta mchungaji akuombee macho yako yana uwezo wa kuona vitu watu wasivyooona usiku wakati wa ndoto sasa maadui wanafanya kazi za kukusumbua usilale wanajua ukilala utaona mambo yao fanya hivyo utakuja nitafuta na kunipa zawadi
 
Asante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom