Nina tatizo la kutopata hedhi kwa wakati, kwa mwaka naweza kupata hedhi mara tatu

Jun 24, 2017
9
3
Jamani ndgu zangu mm Nina umri wa miaka 21 naomba msaada Nina tatizo la kutopata hedhi kwa muda mwingi Hali inayonifanya nikose Raha.

Kwa mwaka napata Mara 3 tu. Na pindi ikitokea napata maumivu makali Sana na kichefuchefu Mara ya mwisho ilikuwa 30/12/2020 Hadi Leo sijaona Tena na Sina dalili yoyote na Wala Sina ujauzito.
 
Tafuta toto la ndizi teke lile linaning'inia kwenye mkungu maganda yake mekundu ndani ndio kuna ndizi changa.

Toa zile za juu ubakishe zile changa zaidi twanga upate juisi yake nusu kikombe cha chai inakua nyeusi kunywa hasubuhi ukiweza na jioni siku saba,utaleta mrejesho
 
Jamani ndgu zangu mm Nina umri wa miaka 21 naomba msaada Nina tatizo la kutopata hedhi kwa muda mwingi Hali inayonifanya nikose Raha. Kwa mwaka napata Mara 3 tu.Na pindi ikitokea napata maumivu makali Sana na kichefuchefu Mara ya mwisho ilikuwa 30/12/2020 Hadi Leo sijaona Tena na Sina dalili yoyote na Wala Sina ujauzito.
Unatakiwa kuelewa kuwa kupata siku zako ni pale kuta za kizazi zinapomomonyoka kutoka na kwamba mwezi huo haukubeba mimba.

Vitu vinavyomomonyoka huwa ni tezi zilizotengenezwa na Hormone ya Prpgesterone kama maandalizi ya kumpokea mtoto atakayetungwa

Amenorrhea ni neno la kitaalamu la kukosa kuona siku zako.

Zipo za aina mbili.

1. Prinary Amenorrhea
2. Secondary Amenorrhea

Primary Amenorrhea ni ile ambayo mwanamke hapati period hata baada ya kufika miaka 15.

Secondary Amenorrhea ile mtu amhae alishaona Period ila sasa zimepotea kwa zaidi ya miezi mitatu walau.

Secondary Amenorrhea ndo tatizo ulilo nalo wewe. Kuna sababu nyingi za kupata hii hali.

Sababu za mwenendo wa Maisha yako.
1. Kufanya Mazoezi sana
2. Kuwa na utapia mlo au kutokula, kukonda
3. Stress

Sababu za Kimwili
1. Matatizo katika Mfumo wa ubongo katika Hypothalamus na Pituitary.

2. Kuzalisha kwa wingi hormone za Prolactin mgonjwa huwa na dalili ya kutoka maziwa kwenye titi pale anapojikamua iwe kidogo au kwa wingi.

3. Kuwa na mtatizo ya Hormone za Thyrpid kiungo hiki hukutwa shingoni na kikivimba huitwa Goitre.

4. Kuwa na mvurugiko wa hormone za kike zile zinazoandaa kizazi kupokea Mimba kama nilivoanza kwenye utangulizi.

5. Kushikana kwa kuta za kizazi labda kwa sababu uliwai kusafisha mimba.

6. Ovarian Failure

Sababu ndio kama hizo na mara nyingi unaitaji kwenda hospitali walau kufanyiwa utafiti ili kujua chanzo na ili uanze matibabu ya kuzirejesha siku zako.

Tunaweza kuwasiliana zaidi kama utaitaji msaada wa kitabibu katika hospitali kama utakuepo Dar.

Pole sana.
 
Tafuta toto la ndizi teke lile linaning'inia kwenye mkungu maganda yake mekundu ndani ndio kuna ndizi changa,toa zile za juu ubakishe zile changa zaidi twanga upate juisi yake nusu kikombe cha chai inakua nyeusi kunywa hasubuhi ukiweza na jioni siku saba,utaleta mrejesho
Nachemsha hiyo juice au bila kuchemsha.
 
Jamani ndgu zangu mm Nina umri wa miaka 21 naomba msaada Nina tatizo la kutopata hedhi kwa muda mwingi Hali inayonifanya nikose Raha.

Kwa mwaka napata Mara 3 tu. Na pindi ikitokea napata maumivu makali Sana na kichefuchefu Mara ya mwisho ilikuwa 30/12/2020 Hadi Leo sijaona Tena na Sina dalili yoyote na Wala Sina ujauzito.
SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI KWA WAKATI
FAHAMU SABABU ZA MWANAMKE KUKOSA HEDHI /KUTOPATA HEDHI KATIKA MPANGILIO MAALUMU (AMENORRHEA)

Elimu kwa wanawake na wasichana kuepukana na magonjwa mbalimbali yanayosababisha kukosa hedhi iliyo salama, kutokana na maswali yenu ya kwanini mwanamke huwa anakosa hedhi ilhali Hana mimba??nimeona ni vyema kuelezea hili tatizo kwa undani ili muweze kutambua vizuri tatizo hili ambalo kitaalamu linajulikana kama AMENORRHOEA

AMENORRHEA NI NINI??
hii ni hali ya mwanamke ambaye amepevuka na kukomaa maumbile yake ya Uzaz kushindwa kupata hedhi/kupitiliza siku za hedhi
~kwa ufupi tatizo hili limekua likiwakumba na kuwaletea usumbufu wa kisaikolojia wanawake wengi wakidhani kwamba wamepata ujauzito nk, hata hivyo tatizo hili la kukosa hedhi linaweza kutokea awali au baadae kabisa maishani
~kuna aina mbili za tatizo hili (amenorrhea)

(1)PRIMARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke/msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo ambapo Hali hii huweza kuendana na kutopata mabadiliko ya kimaumbile yanayoambatana na kuvunja ungo kama vile KUOTA NYWELE SEHEMU ZA SIRI, KUOTA MATITI, NK ila bado hapati siku zake

(2)SECONDARY AMENORRHEA ~hii ni hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito wala hanyonyeshi na ambaye hajakoma hedhi na wala hatumii dawa za Uzazi wa mpango ambapo awali alikua akipata hedhi kama kawaida Lakini akasimama kwa muda huenda ni miezi au mwaka mzima hapati hedhi mpaka sasa
~NAMNA AMBAVYO MWANAMKE HUPATA HEDHI
Kwa Kawaida ili mwanamke apate hedhi katika mzunguko ulio Sawa ni lazima tezi ya hypothalamus na pituitar pamoja na kiwanda cha mayai(ovaries) viwe vinafanya kazi kwa ushirkiano yani sawasawa

~VYANZO VYA TATIZO HILI
Vyanzo vya tatizo hili vyaweza kuwekwa katika Makundi makuu matatu ambayo ni vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo katika tezi ya pituitar, mfumo wa Uzazi na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke visababishi hivyo ni Γ·

πŸ‘‰
matatizo katika hypothalamus ambapo matatizo haya husababisha Γ·uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitar, ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya Uzazi,
πŸ‘‰
uzito mdogo kuliko Kawaida
πŸ‘‰
pituitar kushindwa kufanya Kaz vzur baada ya seli zake kufa hii ni iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua
πŸ‘‰
kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu (PROLACTINEMIA)
(proclatin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha hivyo Hali ya kuwa proclatin nyingi katika damu husababisha kukosa hedhi
πŸ‘‰
kuwa na msongo wa mawazo ni hatari
πŸ‘‰
kuziba kwa utando unaozunguka uke (HYMEN) hivyo kukosekana tundu la kupitishia damu

(IMPERFORATE HYMEN)
πŸ‘‰
Mazoezi makali ya mwili na ulaji mdogo wa Chakula, tabia hii hushusha homoni ambayo inahusika na kuweka siku zako katika Hali nzuri yani hufanya leptin kuwa katika kiwango cha chini sana hivyo ni hatari
πŸ‘‰
ugonjwa wa kurithi wa GALACTOSEMIA unaoambatana na kuwa na kiwango kidogo cha sukari aina ya GALACTOSE katika damu
πŸ‘‰
baadhi ya magonjwa ya viungo vya Uzazi yamekua yakiambatana na kusimama kwa hedhi mfano wa magonjwa hayo ni POLYCYSTIC OVARIAN SYNDROME
πŸ‘‰
MENO PAUSE ~hii ni hali ambayo hutokea kipindi cha miaka 42_55 homoni zinazohusika na kupata hedhi huwa Kwenye kiwango cha chini sana kiasi hufanya haziwezi kufanya Kazi sawasawa

DALILI ZA TATIZO HILI
πŸ‘‰
Mwanamke kuwa na vinyweleo vingi na kuota ndevu hii inamaanisha na kuashiria kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni za kiume za ANDROGEN
πŸ‘‰
kuongezeka uzito kupita kiasi
πŸ‘‰
matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito wala hanyonyeshi
πŸ‘‰
mwanamke kuwa na mhemko kuliko Kawaida
πŸ‘‰
uke kuwa mkavu
πŸ‘‰
kutokwa jasho sana wakati wa usiku
πŸ‘‰
mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria kuwepo kwa tatizo katika ovaries
πŸ‘‰
kutokupata hedhi katika mpangilio

MATIBABU
NA JINSI YA KUJIKINGA NA TATIZO HILI
matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kutibiwa hospital kutokana na chanzo cha tatizo ambapo huwa ni kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji pale patapobidi
NOTE :Ni vizuri kuongea na daktari ili ajue ni kwa namna gan atakusaidia pia waweza kufanya mambo yafuatayo ili kujiepusha na tatizo hili

ZINGATIA ULAJI ULIOSAHIHI AMBAO UNAHUSISHA ULAJI WA MATUNDA KWA WINGI NA MBOGA ZA MAJANI
TUMIA JUICE YA WATERMELON/MAJI YA MSHUBIRI
FANYA MASAJI KWENYE TUMBO LA CHINI KWA KUTUMIA MAJI YA UVUGUVUGU (UKIWA KTK BREED) HII ITASAIDIA KUONGEZA DAMU NYINGI KUTOKA
KULA CHAKULA KISICHOTOKANA NA DAMU (VEGETARIAN DIET) CHENYE PROTIN NYINGI MFANO, NAZI, MAHARAGE, KOROSHO NA KARANGA
Hakikisha unazingatia haya ili kuepukana na madhara ya huu ugonjwa ambayo ni makubwa sana
MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA IWAPO TATIZO HILI HALITAPATIWA MATIBABU
Mwanamke kuchelewa kuingia menopause hali huu ni mbaya kwani husababisha SARATAN YA MATITI kwa kias kikubwa
mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwasababu ya kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na uke kuwa mkavu
husababisha matatzo ya kutopata usingizi
matiti husinyaa na kupata hedhi Bila mpangilio.
Tiba yake ipo nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia upate kupona.
Ukitumia hizo njia na hujapona nitafute mimi nipatekukutibia maradhi yako upate kupona.
 
Unatakiwa kuelewa kuwa kupata siku zako ni pale kuta za kizazi zinapomomonyoka kutoka na kwamba mwezi huo haukubeba mimba.

Vitu vinavyomomonyoka huwa ni tezi zilizotengenezwa na Hormone ya Prpgesterone kama maandalizi ya kumpokea mtoto atakayetungwa

Amenorrhea ni neno la kitaalamu la kukosa kuona siku zako.

Zipo za aina mbili.

1. Prinary Amenorrhea
2. Secondary Amenorrhea

Primary Amenorrhea ni ile ambayo mwanamke hapati period hata baada ya kufika miaka 15.

Secondary Amenorrhea ile mtu amhae alishaona Period ila sasa zimepotea kwa zaidi ya miezi mitatu walau.

Secondary Amenorrhea ndo tatizo ulilo nalo wewe. Kuna sababu nyingi za kupata hii hali.

Sababu za mwenendo wa Maisha yako.
1. Kufanya Mazoezi sana
2. Kuwa na utapia mlo au kutokula, kukonda
3. Stress

Sababu za Kimwili
1. Matatizo katika Mfumo wa ubongo katika Hypothalamus na Pituitary.

2. Kuzalisha kwa wingi hormone za Prolactin mgonjwa huwa na dalili ya kutoka maziwa kwenye titi pale anapojikamua iwe kidogo au kwa wingi.

3. Kuwa na mtatizo ya Hormone za Thyrpid kiungo hiki hukutwa shingoni na kikivimba huitwa Goitre.

4. Kuwa na mvurugiko wa hormone za kike zile zinazoandaa kizazi kupokea Mimba kama nilivoanza kwenye utangulizi.

5. Kushikana kwa kuta za kizazi labda kwa sababu uliwai kusafisha mimba.

6. Ovarian Failure

Sababu ndio kama hizo na mara nyingi unaitaji kwenda hospitali walau kufanyiwa utafiti ili kujua chanzo na ili uanze matibabu ya kuzirejesha siku zako.

Tunaweza kuwasiliana zaidi kama utaitaji msaada wa kitabibu katika hospitali kama utakuepo Dar.

Pole sana.
Safiii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom