Nina tatizo la kutoisha mkojo, nikimaliza kukojoa nikikaa baada dk 20 naskia mkojo tena. Nikimaliza kukojoa mwisho matonematone hutoka

Dalili ya tezi dume! Kwani tezi dume ni nini?
Tezi dume ni moja ya tezi la uzazi la kiume ambalo kila mwanaume analo, tezi hili lipo chini ya kibofu cha mkojo na linazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.

Jinsi umri unavyoongezeka tezi dume nalo huongezeka ukubwa ambao
unaweza kuwa wa kawaida au saratani.

Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume:

Maambukizi ya Bakteria (Prostatitis).

Kukua kwa tezi dume ambalo sio saratani (Benign Prostatic Hypertrophy-BPH).

Saratani ya tezi dume.

Tafadhali bonyeza hapo chini kupakua jarida kwa maelezo zaidi

Attachment: Download


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sijawahi kuwa natatizo lamkojo kutoka bila hiari yangu naskia mkojo na nnaweza kuubana hata masaa2 Ila ndo hivo nikikojoa baada ya dk30 ntahis Tena mkojo na kuhusu UTI mpaka umri huu miaka33 sjawahi kuugua UTI kwakweli
Unachokula kiangalie inawezekana huli wanga ilishanitokeaga, tengeneza juisi ya tangawizi kunywa kidogo mara mbili kwa siku hata mara tatu hiyo hali itaisha
 
Habar ndugu zangu mim nikijana wa miaka33 kwakipindi kireefu nimekua nashida nikinywa maji hata robo kikombe baada ya dk20 ntahis mkojo nikienda kukokoja ntakojoa ile naumalizia mkojo mwishoni unatoka kwa kukatakata namatone matone mwisho wakukojoa...
Mkuu nenda hospitali kacheki, huenda tatizo la tezi dume lina kunyemelea
 
mkuu nenda hospitali kacheki huenda tatizo la tezi dume lina kunyemelea
Nimeshacheki, nilikua muhimbili hakuna tatizo lolote lililoonekana. Nimeambiwa nipimwe kipimo cha kuingiza kifaa katika njia ya mkojo wajue ni nini shida Ila nimefikiria kwanza maana kuingizwa kitu Tena ktk njia ya mkojo
 
Kwa dalili zako,haraka haraka unaweza ukawa na ugonjwa wa DIABETES INSIPIDUS( chanzo inaweza ikawa ni figo(nephrogenic)nau ni ubongo (central) ) fika MUHIMBILI watakufanyia vipimo na kukutibu tatizo lako]
Nimefika muhimbili nimefanyiwa ultrasound damu na mkojo hawakuona kitu wamedai waniingizie kifaa ktk njia ya mkojo
 
Diabetes insipidus sio kisukari mzee, kisukari ni Diabetes mellitus. Vitu viwili tofauti kabisaa Nenda hospitali utapata tiba

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mkuu nilifika muhimbili vipimo vya awali ultrasound na damu hakukuonekana kitu ziada, wameelekza nifanyiwe kipimo Cha mrija kuingizwa ktk njia ya mkojo
 
Habar ndugu zangu mim nikijana wa miaka33 kwakipindi kireefu nimekua nashida nikinywa maji hata robo kikombe baada ya dk20 ntahis mkojo nikienda kukokoja ntakojoa ile naumalizia mkojo mwishoni unatoka kwa kukatakata namatone matone mwisho wakukojoa...

Pole kwa kuumwa,
Ili kutatua tatizo hili na kwa jinsi ambavyo unaeleza umekwishafanya vipimo mbalimbali ni vyema kumwona daktari bingwa wa njia ya mkojo (urologist + nephrologist).

Tatizo laweza kuanzia:
1: Mfumo wa kutengeneza mkojo
Hapa inahusika homoni na mishipa yake ya fahamu.

2: Mfumo wa utunzaji mkojo/mfuko wenyewe. Kuna mambo mengi ya kuzingatia.

3: Mifumo ya kuruhusu mkojo kutoka sphincter zilizoko kwenye kibofu.

4: Mfumo wa kuruhusu kutoka mkojo/mishipa ya fahamu.

5: Viungo vingine vinavyozunguka kibofu cha mkojo vyaweza kuwa chanzo cha hitirafu.

6: Matibabu/mazoezi mengine yaliyopita.

7: Mfumo wako wa mgongo.
 
May be urethral stricture yaan kwenye njia ya mkojo kutoka nje kuna vizuiz vimeota hapo ambapo sometimes vinazuia kutoa mkojo wote na kuubakisha mwingine ndan. Nenda hospital waangalie huko kwenye njia ya kutoa mkojo nje.
 
Back
Top Bottom