Nina tatizo la kutoisha mkojo, nikimaliza kukojoa nikikaa baada dk 20 naskia mkojo tena. Nikimaliza kukojoa mwisho matonematone hutoka

Kwa dalili zako, haraka haraka unaweza ukawa na ugonjwa wa DIABETES INSIPIDUS(chanzo inaweza ikawa ni figo(nephrogenic)nau ni ubongo (central) ) fika MUHIMBILI watakufanyia vipimo na kukutibu tatizo lako]
 
Nipo mkoa wenye joto
Binafsi naweza sema nipo kama wewe, ila naishi mikoa ya baridi. Huwa nikirudigi home, hali inakuwa ya kawaida tu. Ila hata hapa, endapo nikiwa nimekula vizuri na kwa wakati, hata ninywe maji nusu jagi, hali itakuwa ya kawaida tu.

Hebu jaribu kuangalia food na life style yako. Mwili ukiwa unafanya kazi kazi, ukinywa maji yanakaa mwilini maana yatapatiwa kazi pia.
 
Sasa ndugu kila kitu umepima na uko sawa, saa nenda ukanywe tumaji twa Mwamposa.
 
Tezi dume kwa umri wa miaka33 tu..mbona hospitalini shapimaga kwa miaka tofaut ultrasound ya tumbo mara3 kwa tatizo lingine kabisa na tezi dume ikaonekana iko sawa tu
Wewe unajua wanavyopima Tezi dume? Usiwe mbishi hiyo ni dalili kuwa Postate imevimba au ni Postate cancer
 
Kama upo mjini Dar nenda hospitali za wahindi ukaangaliwe mkojo wako utakuwa unayo maradhi ya UTI aka mkojo mchafu na Bacteria na infection kwenye njia ya kibofu cha mkojo. Au unayo Maradhi ya KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA).
Haya ni maradhi ya kutokwa na mkojo bila ya khiari . Kabla mkojo haujakusanyika vizuri kwenye kibofu cha mkojo na mgonjwa kujiandaa kwenda chooni, hutokwa na mkojo hata kabla ya kufika chooni.

SABABU:
(1) Kulegea kwa kibofu cha mkojo.
(2) Maradhi ya kisukari.
(3) Kuwa na minyoo tumboni.
(4 Kutumia madawa ambayo huchochea kutokwa kwa mkojo.
(5) Kuwa katika mazingira au hali ya hewa ya baridi.
(6) Kunywa kwa wingi vinywaji, pombe,n.k.
Nitafute kwa wakati wako nipate kukutibia ili uweze kupona maradhi yako.
 
Kwa dalili zako,haraka haraka unaweza ukawa na ugonjwa wa DIABETES INSIPIDUS( chanzo inaweza ikawa ni figo(nephrogenic)nau ni ubongo (central) ) fika MUHIMBILI watakufanyia vipimo na kukutibu tatizo lako]
Mkuu kisukari wala sina mkuu, sukari yangu nikiwa sijala ni 5.1
 
Binafsi naweza sema nipo kama ww, ila naishi mikoa ya baridi. Huwa nikirudigi home, hali inakuwa ya kawaida tu. Ila hata hapa, endapo nikiwa nimekula vizuri na kwa wakati, hata ninywe maji nusu jagi, hali itakuwa ya kawaida tu.

Hebu jaribu kuangalia food na life style yako. Mwili ukiwa unafanya kazi kazi, ukinywa maji yanakaa mwilini maana yatapatiwa kazi pia.
Kazi yangu ni ya duka, ni ya kukaa tu.
 
Kama upo mjini Dar nenda hospitali za wahindi ukaangaliwe mkojo wako utakuwa unayo maradhi ya UTI aka mkojo mchafu na Bacteria na infection kwenye njia ya kibofu cha mkojo Au unayo Maradhi ya KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA)...
Mkuu sijawahi kuwa natatizo la mkojo kutoka bila hiari yangu, nasikia mkojo na nnaweza kuubana hata masaa 2 Ila ndo hivyo, nikikojoa baada ya dk 30 nitahisi tena mkojo na kuhusu UTI mpaka umri huu miaka 33 sijawahi kuugua UTI kwakweli
 
Kwahiyo ulitaka ukojoe kila baada ya masaa 4
Sio kila baada ya masaa manne namaana ya kwamba mbona sikuchukui mda kidogo mkojo ndio unibane maana najiona tofauti na watu wengine huchukua hata masaa 3 na kuendelea ndio hubanwa namkojo na hapo ni anakua kanywa maji hata lita moja
 
Back
Top Bottom