Nina tatizo hili la kiutumishi wa UMMA naomba msaada kujuzwa

Ingekuwa rahisi kupata hicho anacho kifikiria cha UKUU WA IDARA kwani anauzoefu mkubwa ktk mambo ya Elimu. Huko aliko sasa ana anza upya

Kwa mfano kama angesoma fani yake faida zingekuwa zipi? Maana nasikia unapanda tu labda toka D1 Mpaka D3 basi mfano kama mtumishi alikuwa ana bachelor akaenda kuongeza mastaers
 
mdau si useme ukweli tu kwamba umechoka kuwa mkata nyasi unataka ukuu wa idara.
 
Maelezo meeeengi, lakini hapa we unaonekana unataka ukuu wa idara. Hapo kazi unayo, maana miaka 7 ni lazima itimie ndo utakuwa na kigenzo cha kupata ukuu wa idara. Na kwa ngazi ya mshahara ulioanzia itakuchukua muda kufikia sifa kwani mkuu wa idara anatakiwa awe na TGS-G au TGS-H ili iwe rahisi kumsogeza kwenye TGS-I ambayo ndiyo stahili ya mkuu wa idara, endapo itatokea mkuu wako hayupo kwa sababu yoyote ile, unaweza kukaimu lakin si kurasimishwa cheo hicho. Nakuombea PEPO MTAKA VYEO akutoke maana utawamaliza wenzako ofisini.

mmmh! Maneno makali lakini yaliyo beba ukweli mtupu!
 
nyie ndo AG Werema anawaite "Rent seekers Marasmus"..... pole sana ndugu.. kumbe kusoma sio kuelimika!!
 
Kwa mfano kama angesoma fani yake faida zingekuwa zipi? Maana nasikia unapanda tu labda toka D1 Mpaka D3 basi mfano kama mtumishi alikuwa ana bachelor akaenda kuongeza mastaers

ni kweli anapanda kidogo lakini wakati wa kufanya uteuzi wa mkuu wa Idara uwa wana angalia Elimu (kuanzia digrii na kuendelea) na Uzoefu(si chini ya miaka 5 ktk fani husika). hivyo si ajabu akapata ongezeko dogo la D3 alafu baada ya Mwaka mmoja akapata uteuzi kuwa Mkuu wa idara ya Elimu ambayo ngazi yake ni LSSE1.
 
Mkuu,miaka 7 imeshakatika toka andiko lako, haujapata tu ukuu wa idara?
 
Wanajamvi naomba kujua vigezo vya uteuzi wa wakuu wa idara katika hizi halmashauri za wilaya ni kwamba wengine wanasema mpaka uwe na uzoefu wa kazi zaidi ya miaka 7 kwa idara moja tu yaani ile unayoifanyia kazi na wengine wanasema mpaka uwe na uzoefu wa miaka 7 katika utumishi wa UMMA haijalishi idara moja unayofanyia kazi bali ni idara yeyote ile katika halmashauri ilimradi umeutumikia UMMA kwa miaka 7.kwa hiyo napata mkanganyiko hapo.

Ni hivi mimi nilikua mwalimu ambaye niliajiliwa mwaka 1998 baadae nikajiendeleza kwa kusoma chuo cha mipango dodoma degree na masters ambapo nimemaliza mwaka juzi 2010 na baada ya kuhitimu nikarudi wilayani kwangu na kufanya recategolization nimehamishiwa idara ya mipango nina mwaka na kidogo mpaka sasa toka nihamishiwe idara hii mpya je kwa uzoefu huu wa mwaka mmoja katika hii idara ya mipango nina uwezo wa kuteuliwa na kua mkuu wa idara??kwasababu ukihesabu toka nianze kazi 1998 mpaka sasa ni miaka 13 ambapo 12 nilikua mwalimu shule za msingi na nimekua afisa mipango kwa mwaka mmoja kwa hiyo naomba msaada wa kujuzwa hilo pia kama kuna waraka wa uteuzi wa wakuu wa idara mmoja kati yetu anao ningeomba atuwekee hapa ili na sisi tuuone walau uweze kutusaidia kutatua jambo hili maana nakosa raha kabisa kwa kua siyaoni matunda ya elimu yangu kichwa kimebaki kimechanganyikiwa kabisaaaaaa maana ukiniambia nitumikie cheo hiki kipya miaka 7 ndipo nipate ukuu wa idara maana yake nitaupata uafisa mipango wa wilaya karibia na kustaafu.mbaya zaidi nilipofanyiwa recategolization maana yake nilirudishwa kwenye TGS D kama mtu wa entry point kweli haya naona kama ni maumivu makali sana ndio maana nimeona niingie hapa jamvini kwani naamini jamvi hili litasaidia kupata maoni mbalimbali na nyaraka za vyeo juu ya jambo hili
Kwa hiyo unalilia ukuuu wa idara!? Kwa hiyo ulienda kusoma ili uwe mkuu wa idara? Yani kuleta mada Kama hiii kwenye jukwaa hili walahi haufai hata kuwa Msaidiz wa idara, nimekushusha Sana, mkuuu ukuu wa idara hupewa watu wenye heshima zao sio mtu Kama wewe, hupewa watu Wa kujitambua wewe bado una utoto Sana mno haufaiiiiiiiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ukweli mkubwa unachokisema, ingawa tumeshuhudia pia watu wa hovyo wengi tu wanapewa ukuu wa idara.
 
Mkuu,miaka 7 imeshakatika toka andiko lako, haujapata tu ukuu wa idara?

Soma huo uzi Post No 1 Jamaaa aliacha kazi 2014, huenda keshajinyonga huko kwao Iringa maaana tangu Septemba 2019 hajaonekana JF.
 
Soma huo uzi Post No 1 Jamaaa aliacha kazi 2014, huenda keshajinyonga huko kwao Iringa maaana tangu Septemba 2019 hajaonekana JF.
Ahsante kwa taarifa.
 
Punguza tamaa ya kutaka cheo ndugu, hizi kazi za umma hazina mwenye nazo, siku ikifika cheo unapata lakini siku ikifika utakiacha pia. Nimesoma maelezo yako kwa umakini lakini huna la ziada bali una uchu wa cheo. Watu kama nyie ni hatari sana makazini. Fanya kazi ulizo pangiwa matunda yako ndiyo yatakupandisha.

Ushahuri mzuri sana.
 
Haya masuala ya vyeo magumu sana!inategemea nani anakujua!!MKUU WANGU WA SHULE BADO ANA DIPLOMA JAPO TAMISEMI WANATAKA MWENYE DEGREE!!!NA ANADUNDA TU!!!Kwa hiyo bora uingie kwenye ujasiria mali!!!
 
Haya masuala ya vyeo magumu sana!inategemea nani anakujua!!MKUU WANGU WA SHULE BADO ANA DIPLOMA JAPO TAMISEMI WANATAKA MWENYE DEGREE!!!NA ANADUNDA TU!!!Kwa hiyo bora uingie kwenye ujasiria mali!!!
Kinachomata ni connection,hakuna kuangalia una elimu kiasi gani.
 
Back
Top Bottom