Nina tatizo hili la kiutumishi wa UMMA naomba msaada kujuzwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina tatizo hili la kiutumishi wa UMMA naomba msaada kujuzwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Aug 17, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wanajamvi naomba kujua vigezo vya uteuzi wa wakuu wa idara katika hizi halmashauri za wilaya ni kwamba wengine wanasema mpaka uwe na uzoefu wa kazi zaidi ya miaka 7 kwa idara moja tu yaani ile unayoifanyia kazi na wengine wanasema mpaka uwe na uzoefu wa miaka 7 katika utumishi wa UMMA haijalishi idara moja unayofanyia kazi bali ni idara yeyote ile katika halmashauri ilimradi umeutumikia UMMA kwa miaka 7.kwa hiyo napata mkanganyiko hapo.

  Ni hivi mimi nilikua mwalimu ambaye niliajiliwa mwaka 1998 baadae nikajiendeleza kwa kusoma chuo cha mipango dodoma degree na masters ambapo nimemaliza mwaka juzi 2010 na baada ya kuhitimu nikarudi wilayani kwangu na kufanya recategolization nimehamishiwa idara ya mipango nina mwaka na kidogo mpaka sasa toka nihamishiwe idara hii mpya je kwa uzoefu huu wa mwaka mmoja katika hii idara ya mipango nina uwezo wa kuteuliwa na kua mkuu wa idara??kwasababu ukihesabu toka nianze kazi 1998 mpaka sasa ni miaka 13 ambapo 12 nilikua mwalimu shule za msingi na nimekua afisa mipango kwa mwaka mmoja kwa hiyo naomba msaada wa kujuzwa hilo pia kama kuna waraka wa uteuzi wa wakuu wa idara mmoja kati yetu anao ningeomba atuwekee hapa ili na sisi tuuone walau uweze kutusaidia kutatua jambo hili maana nakosa raha kabisa kwa kua siyaoni matunda ya elimu yangu kichwa kimebaki kimechanganyikiwa kabisaaaaaa maana ukiniambia nitumikie cheo hiki kipya miaka 7 ndipo nipate ukuu wa idara maana yake nitaupata uafisa mipango wa wilaya karibia na kustaafu.mbaya zaidi nilipofanyiwa recategolization maana yake nilirudishwa kwenye TGS D kama mtu wa entry point kweli haya naona kama ni maumivu makali sana ndio maana nimeona niingie hapa jamvini kwani naamini jamvi hili litasaidia kupata maoni mbalimbali na nyaraka za vyeo juu ya jambo hili
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Talk to "people who make decisions". Dont believe in maandishi.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  can u notify me examples of peoples who make decision?
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Katibu mkuu na wasaidizi wake.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  Ongea taratibu, mkuu wa idara yako nasikia hana hata cheti cha lasaba. Tena nasikia ana mikoba ya babu yake wa Gamboshi
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hapa nilipo hakuna mkuu wa idara amehamishwa kwa hiyo yupo jamaa amekaimishwa tu na ana bachelor
   
 7. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwanza naomba uelewe kuwa Elimu na miaka saba pekee havitoshi automatically kukufanya uwe mkuu wa idara. Ni utendaji bora wenye ufanisi na tija katika utumishi wa umma. Nadhani OPRAS unayo, angalia comment za boss wako kwenye hiyo OPRAS yako.
  Pili nije kwenye swali yako. Jibu ni kwamba ni UZOEFU KAZI. Kwa hiyo kama ni Mipango basi ni miaka isiyopungua saba katika kitengo cha mipango. Mwambie Afisa Utumishi akupe kitabu cha muundo mpya wa utumishi katika halmashauri, utaona sifa za kila kada. Ukishindwa nikumbushe baada ya sikukuu nitakuwa ofisini, nikupatie
   
 8. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unataka UKUU WA IDARA?
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nataka kujua vigezo vinavyotumika kumpata mkuu wa idara katika situation kama hiyo TGS I c mchezo
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mchango wako mzuri nimeupokea nashukuru mkuu
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bujibuji acha vituko nipo serious kikubwa nataka kujua tu taratibu zake zipoje na anayepandisha ni TAMISEMI au UTUMISHI WA UMMA??
   
 12. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ninachokiona wewe una uchu na madaraka, na usipojiangalia unaweza kuua mtu kwa kuutafuta ukuu wa idara. Ninachoweza kukushauri ni kuwa mvumilivu, endelea kufanya kazi zako kisomi, onesha kuwa unaweza na kwa kuwa uko karibu na mkurugenzi, kazi zako zitakuwa apreciated na utapandishwa daraja accodingly.

  lakini ukianza kuutafta ukuu wa idara, utaanza kuharibu baadhi ya mambo.

  Kwani ulisoma ili uwe mkuu wa idara au afisa mipango?
   
 13. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Haupo serious mkuu =@kilimasera. Nimekumbuka kitu, mwaka jana ulileta thread iliyosema' nina masters ya management, sina kazi'. Siyo wewe? Ngoja niitafute nikuwekee. Naomba kwenye masuala kama haya yanayohusu maisha tuwe makini maana wengine tunayachukulia very serious
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nakushukuru kwa ushauri lengo si kwamba nataka kuwa mkuu wa idara kikubwa nataka kujua vigezo kama ni miaka 7 ya utumishi wa umma au ni miaka 7 ya kufanya kazi yangu hii mpya kubwa ni hilo ni vizuri nikajua future yangu ili nijipange sawasawa
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  sina uhakika katika hilo, lakini nadhani ni miaka 7 ktk idara hiyo. Kama ungesoma education kwa masters hiyo, ungeupata mda si mrefu.

  Ninachokushauri kuwa mvumilivu, mambo mazuri hayataki haraka mkuu. Idara ya mipango nimefanya pt miaka ile, kwa habari ya maslah, iko safi, haijalishi una nafasi gani. Ni kuwa kwenye mipango tu basi inakuweka nafasi nzuri
   
 16. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nashukuru nimekupata mkuu thanx a lot
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nina kazi tayari tatizo ni hapo kwenye uteuzi wa ukuu wa idara
   
 18. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,127
  Likes Received: 1,726
  Trophy Points: 280
  mi navyojua ukifanyiwa recategorization unaendelea kulamba mshahara wako uleule,kwani mara nyingi haushushwi labda kama ulipandishwa kimakosa tu,kama umeshushwa bro nenda kwa wanaohusika na masuala ya utumishi wa umma wakusaidie ila sio hao walioshusha mshahara wako,tafuta wengine uwaelezee kwa uhuru,kuhusu suala la kuwa mkuu wa idara ni hadi uteuliwe kwani hicho cheo hakiji kwa mserereko kama hv vya kawaida,piga kazi,utaonwa tu na mwisho wa cku utateuliwa,pole sana mkuu
   
 19. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Pole sana kwa kurudishwa nyuma mshahara wako, ulitakiwa kuhama nao as mshahara binafsi.

  Suala la ukuu wa idara forget about that, ualimu then mipango uwe mkuu wa idara kwa mwaka mmoja uliofanya kazi. Ungeenda idara ya elimu may be ingekuwa rahisi lakini everything is possible, just fight.
   
 20. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Liwalo na liwe bora uwe na bidii ya kuimba nyimbo zetu wenye mapembe na mdomo wa kula bila kushiba
   
Loading...