Nina tamaa ya kuwekeza

DongoJeusi

Member
Aug 1, 2018
79
76
Heri ya mwaka mpya wana JF hongera sana kwako kwa kuweza kuiona hii siku ya leo na pole sana kwa wale ambao bado ni wagonjwa naamini kwa MUNGU muweza watapata nafuu.

Mimi mwanafunzi wa chuo fulani hapa Mwanza na nipo mwaka wa pili sasa tamaa yangu kubwa sana mpaka hivi sasa Ni kuwekeza katika biashara hususani biashara ya DAGAA kwa hapa Mwanza maana zinapatikana na soko Ni kubwa kwa mikoani hususani Mbeya , morogoro , Iringa kwa tafiti ndogo niliyojaribu kuifanya.

Katika kila tamaa lazima kuwepo na changamoto zinazofanya malengo yasiende mbele.Je ni masomo ndio yanafanya malengo yasiende mbele? Jibu ni hapana.

Biashara yingi kwa hapa kwetu Tanzania na dunia kiujumla unapohitaji kuianzisha ni lazima kuwepo na vitu kama MTAJI, NGUVU KAZI,SEHEMU YA KUFANYIA BIASHARA NA KILE UNACHOTALAJIA KUFANYA.

Kwahiyo katika hivyo vinne Ni MTAJI PEKEE umekuwa Ni changamoto inayonikwamisha kuweza kuwekeza.Nilikaa na nikawaza kipi cha kufanya kupambana na hii changamoto mwisho nilikuja na wazo LA kukopa BENKI Ila sina chochote cha kuweza kuweka lehani ili BENKI iweze kunipatia mkopo .

Nikaona kuwa wapo ndugu zangu hapa JF waliopitia njia Kama hiii ninayopitia Mimi na wakafanikiwa katika uwekezaji.

Ni njia gani hizo walipitia kuweza kupata MTAJI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaji ni akili zako na uwezo wako wa kuthubutu , unaweza tumia ulicho nacho ukaanza ata kwa gunia moja ya dagaa adi apo baadae utakapo zidi kukuua.

Pia unaweza tumia akili ukakaa na wenye mtaji uka draft kilichopo na unacho kiona ni wengi wanapesa ila wanakosa pa kuweka na ukafanya biashara ya pamoja (zingatia kuwa mwaminifu hakika utafika narudia kuwa mwaminifu)

Hakuna ambae atakuja kukupa pesa kwa njia rahisi kama unavyodhani...ikiwa wewe ni kijana unaweza unganisha nguvu na mtu mwingine mkaanza kwa pamoja
 
Ila hapo uliposema mtu kuja na pesa sikumaanisha hivyo. Ila shukrani kwa hayo mengine yatafanyiwa kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom