Nina sifa zote lakini sipati mpenzi, je nina gundu?

Mimi ni miongoni mwa wale 7 uliowahi kuanao advance! Na ni mm niliekwendea kwa babu! Utakoma kujishebedua huu mwaka wako!
 
Heshima mbele waungwana.

Kuna ishu inanitatiza sana wakuu, kipindi cha nyuma, hususan wakati nikiwa nasoma high school na baada ya kumaliza form six (mwaka 2006) nilikuwa na zali sana la kupendwa na wasichana kiasi kwamba nishawahi tongozwa na wasichana kadhaa, na hali iliyonifanya nisipate tabu kabisa kutafuta madem by that time, kwa kweli nilikuwa na wasichana wengi ambao walifika 7 na wote walikuwa active (ndani ya miaka 2 tu), kwa kipindi nikiwa a-level, mpaka namaliza mwaka 2006 hadi najianda kuanza chuo mwaka 2007.

Mwaka 2007 kwenye mwezi wa 6 niliamua kubadili tabia na nikashawishika kwenda kupima ukimwi kwa mara ya kwanza, na nikasema kama nikiwa negative, basi naachana kabisa na mambo ya kuwa na wasichana wengi, namshukuru mungu nilienda pale angaza mnazi mmoja na nikapima na majibu yakatoka niko poa kabisa, kuanzia pale nikawapiga chini wale madem mmoja baada ya mwingine, kwa kweli watatu kati ya hao 7 walishikwa na uchungu na walinililia sana na ilifikia kipindi nikawaambia nimeamua kuokoka, so ni mpaka nifunuliwe.

Sasa baada ya pale niliishi kwa amani sana na nilipata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu mwaka 2007 huo huo. Baada ya pale sikuwa kabisa na ishu za wasichana, na mpaka namaliza chuo nilikuwa peke yangu, na sikuwahi ku experience ile hali ya "kutokewa" na wasichana kwa kipindi chote chuoni hali iliyonifanya nifanye vizuri kwenye course zote mpaka namaliza mwaka wa 3 sijawai pata supplementary .

Nilimaliza chuo mwaka jana 2010, na namshukuru mungu suala la ajira halikunisumbua kwani nilipata kazi nzuri tu.

Tatizo linalonisumbua ni kwamba kwa sasa ndio nahitaji sasa nimpate msichana mwenye heshima na mtulivu ili kama tukienda vyema, nimuandae kwa ajili ya kufanya naye future.

Wakuu hili limekuwa ni bonge la changamoto, maana sioni hata msichana yoyote mwenye time na mimi, japokuwa now days nina tofauti kubwa na kipindi hicho cha nyuma, kipindi cha nyuma nilikuwa mwembamba na kamwili kadogo tofauti na sasa hivi nimepata mwili na ninafanya mazoezi kiasi kwamba nina mwonekano mzuri ukilinganisha na kipindi kile, lakini zaidi ya hapo ni kwamba, now days nina hela [***] tofauti na kipindi cha nyuma ambapo sijawahi kuwa hata na laki moja na sijawahi hata siku moja kumhonga dem hela wala kumnunulia nguo lakini nilikuwa napendwa.

Imefikia wakati naanza kuwaza isije kuwa miongoni mwa wale wasichana niliokuwa nao alinisababishia gundu ndo maana sipati msichana wa kufanya uhusiano.

Naombeni mnisaidie waungwana.

Nifanye nini?

Je jambo hili ni la kawaida au kuna kitu hapa?

___________________________________________
[***] Naona hapo nilipoweka stars panawakera wengine.

Kati ya wale uliokuwa nao enzi hizo hakuna mmoja wapo uliyekuwa na mapenzi ya kweli na ambaye bado yupo single ili uweze kurudisha mapenzi naye.
 
inawezekana tatizo ni kabila lako. Social networks zimewezesha watu kushare experience, ambayo madhara yake ni social alienation kwa watu wenye tabia fulani fulani, au wanaotoka maeneo fulani.
So, SAHAU kuhusu shape na vijisenti, angalia tabia zako. Shape inaweza kukulipa kwenye Mr. Dar City Centre, etc. Vijisenti vitakusaidia kwenye investments, kiti kirefu, etc.
... JISHUSHE.
 
Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu kwahiyo na wewe gaaa gaa nao weee utapata waukweli tu ni vigumu kumtokea demu ukakuta huyohuyo ndio anakufaa inabidi uchunwe chunwe mpaka upate wala ausihangaike kuwatafuta kwa tochi
 
Heshima mbele waungwana.

Kuna ishu inanitatiza sana wakuu, kipindi cha nyuma, hususan wakati nikiwa nasoma high school na baada ya kumaliza form six (mwaka 2006) nilikuwa na zali sana la kupendwa na wasichana kiasi kwamba nishawahi tongozwa na wasichana kadhaa, na hali iliyonifanya nisipate tabu kabisa kutafuta madem by that time, kwa kweli nilikuwa na wasichana wengi ambao walifika 7 na wote walikuwa active (ndani ya miaka 2 tu), kwa kipindi nikiwa a-level, mpaka namaliza mwaka 2006 hadi najianda kuanza chuo mwaka 2007.

Mwaka 2007 kwenye mwezi wa 6 niliamua kubadili tabia na nikashawishika kwenda kupima ukimwi kwa mara ya kwanza, na nikasema kama nikiwa negative, basi naachana kabisa na mambo ya kuwa na wasichana wengi, namshukuru mungu nilienda pale angaza mnazi mmoja na nikapima na majibu yakatoka niko poa kabisa, kuanzia pale nikawapiga chini wale madem mmoja baada ya mwingine, kwa kweli watatu kati ya hao 7 walishikwa na uchungu na walinililia sana na ilifikia kipindi nikawaambia nimeamua kuokoka, so ni mpaka nifunuliwe.

Sasa baada ya pale niliishi kwa amani sana na nilipata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu mwaka 2007 huo huo. Baada ya pale sikuwa kabisa na ishu za wasichana, na mpaka namaliza chuo nilikuwa peke yangu, na sikuwahi ku experience ile hali ya "kutokewa" na wasichana kwa kipindi chote chuoni hali iliyonifanya nifanye vizuri kwenye course zote mpaka namaliza mwaka wa 3 sijawai pata supplementary .

Nilimaliza chuo mwaka jana 2010, na namshukuru mungu suala la ajira halikunisumbua kwani nilipata kazi nzuri tu.

Tatizo linalonisumbua ni kwamba kwa sasa ndio nahitaji sasa nimpate msichana mwenye heshima na mtulivu ili kama tukienda vyema, nimuandae kwa ajili ya kufanya naye future.

Wakuu hili limekuwa ni bonge la changamoto, maana sioni hata msichana yoyote mwenye time na mimi, japokuwa now days nina tofauti kubwa na kipindi hicho cha nyuma, kipindi cha nyuma nilikuwa mwembamba na kamwili kadogo tofauti na sasa hivi nimepata mwili na ninafanya mazoezi kiasi kwamba nina mwonekano mzuri ukilinganisha na kipindi kile, lakini zaidi ya hapo ni kwamba, now days nina hela [***] tofauti na kipindi cha nyuma ambapo sijawahi kuwa hata na laki moja na sijawahi hata siku moja kumhonga dem hela wala kumnunulia nguo lakini nilikuwa napendwa.

Imefikia wakati naanza kuwaza isije kuwa miongoni mwa wale wasichana niliokuwa nao alinisababishia gundu ndo maana sipati msichana wa kufanya uhusiano.

Naombeni mnisaidie waungwana.

Nifanye nini?

Je jambo hili ni la kawaida au kuna kitu hapa?

___________________________________________
wewe la amsingi print sheat zaku kapost vijijini utawakamata kwa staili hiyo na kama una gundu bac ni pindi ya popo bawa 2008 utakula kwa macho bharadhuli wee!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom