Nina sifa zote lakini sipati mpenzi, je nina gundu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina sifa zote lakini sipati mpenzi, je nina gundu?

Discussion in 'Love Connect' started by ZIPOMPAPOMPA, Oct 2, 2011.

 1. ZIPOMPAPOMPA

  ZIPOMPAPOMPA Member

  #1
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele waungwana.

  Kuna ishu inanitatiza sana wakuu, kipindi cha nyuma, hususan wakati nikiwa nasoma high school na baada ya kumaliza form six (mwaka 2006) nilikuwa na zali sana la kupendwa na wasichana kiasi kwamba nishawahi tongozwa na wasichana kadhaa, na hali iliyonifanya nisipate tabu kabisa kutafuta madem by that time, kwa kweli nilikuwa na wasichana wengi ambao walifika 7 na wote walikuwa active (ndani ya miaka 2 tu), kwa kipindi nikiwa a-level, mpaka namaliza mwaka 2006 hadi najianda kuanza chuo mwaka 2007.

  Mwaka 2007 kwenye mwezi wa 6 niliamua kubadili tabia na nikashawishika kwenda kupima ukimwi kwa mara ya kwanza, na nikasema kama nikiwa negative, basi naachana kabisa na mambo ya kuwa na wasichana wengi, namshukuru mungu nilienda pale angaza mnazi mmoja na nikapima na majibu yakatoka niko poa kabisa, kuanzia pale nikawapiga chini wale madem mmoja baada ya mwingine, kwa kweli watatu kati ya hao 7 walishikwa na uchungu na walinililia sana na ilifikia kipindi nikawaambia nimeamua kuokoka, so ni mpaka nifunuliwe.

  Sasa baada ya pale niliishi kwa amani sana na nilipata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu mwaka 2007 huo huo. Baada ya pale sikuwa kabisa na ishu za wasichana, na mpaka namaliza chuo nilikuwa peke yangu, na sikuwahi ku experience ile hali ya "kutokewa" na wasichana kwa kipindi chote chuoni hali iliyonifanya nifanye vizuri kwenye course zote mpaka namaliza mwaka wa 3 sijawai pata supplementary .

  Nilimaliza chuo mwaka jana 2010, na namshukuru mungu suala la ajira halikunisumbua kwani nilipata kazi nzuri tu.

  Tatizo linalonisumbua ni kwamba kwa sasa ndio nahitaji sasa nimpate msichana mwenye heshima na mtulivu ili kama tukienda vyema, nimuandae kwa ajili ya kufanya naye future.

  Wakuu hili limekuwa ni bonge la changamoto, maana sioni hata msichana yoyote mwenye time na mimi, japokuwa now days nina tofauti kubwa na kipindi hicho cha nyuma, kipindi cha nyuma nilikuwa mwembamba na kamwili kadogo tofauti na sasa hivi nimepata mwili na ninafanya mazoezi kiasi kwamba nina mwonekano mzuri ukilinganisha na kipindi kile, lakini zaidi ya hapo ni kwamba, now days nina hela [***] tofauti na kipindi cha nyuma ambapo sijawahi kuwa hata na laki moja na sijawahi hata siku moja kumhonga dem hela wala kumnunulia nguo lakini nilikuwa napendwa.

  Imefikia wakati naanza kuwaza isije kuwa miongoni mwa wale wasichana niliokuwa nao alinisababishia gundu ndo maana sipati msichana wa kufanya uhusiano.

  Naombeni mnisaidie waungwana.

  Nifanye nini?

  Je jambo hili ni la kawaida au kuna kitu hapa?

  ___________________________________________
  [***] Naona hapo nilipoweka stars panawakera wengine.
   
 2. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  umeipanga thread yako vizuri, utapata tu...
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pole sana.
   
 4. ZIPOMPAPOMPA

  ZIPOMPAPOMPA Member

  #4
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh, naomba ushauri na wewe unanipa pole??
   
 5. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #5
  Oct 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  kweli watanzania bado tunaitaji kufanya kazi sana ili tuweze kukabiliana na haya mabadiliko ya kidunia na utandawazi. graduate anapofikiria ushirikina katika mapenzi na kuamua kupost thread jf ili akina ritz, faizafox,omr,mwita,zomba na............... wajue kwamba yeye ni handsome anahela kama million 2 or 3 kwenye his bank account.na maelezo kibao ya kuonyesha jinsi gani alivyokuwa akibadilisha wanawake.
  jiulize nani anayekusifu kwa kuwabadili wanawake. bulll...shit.........mwenzio sijui yupo wapi naye alitokea udom akaja na habari za uhandsome apa jf. alichokipata anajua mwenyewe. jiandae kufata nyayo zake.
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Dah, pole sana..
  Lakini jina Zipompapompa mbona limekaa kike zaidi?
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  kwahiyo pole huitaki?
   
 8. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  kwake hizo ni sifa "zote", kazi ipo!
   
 9. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  umejieleza vizuri na sehemu kubwa ya maelezo yako ni kujisifia tu,hya kila la kheri
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Oct 2, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Kwa kifupi watafuta msichana humu JF!
  Au nimekosea mkuu
   
 11. ZIPOMPAPOMPA

  ZIPOMPAPOMPA Member

  #11
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu nachelea kusema kwamba umenielewa vibaya, na wala sipo hapa kwa ajili ya kujisifu maana ni upuuzi kujisifu with anonymous id, nani anayenijua hapa jf?? Mkuu wewe hujui lakini mwenzako kila siku najiuliza sababu ni nini, may be hayajakukuta ndo maana unaona nimekuja kujisifu.
   
 12. A

  Ashle Member

  #12
  Oct 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "so mpaka nifunuliwe" Unakamatwa kwa maneno ya kinywa chako. Hivyo mpaka utakapofunuliwa ndipo utakapompata huyo unayemtafuta. Goodluck
   
 13. ZIPOMPAPOMPA

  ZIPOMPAPOMPA Member

  #13
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  in short sina kawaida ya kutafuta wasichana sehem za namna hii, nimekuja ku-shere hapa mmu nikijua huenda kuna mtu ashawai kutana na ishu kama yangu, what if kama kuna kitu nakosea??
   
 14. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Si uwatokee mwenyewe! Au unasubiri utongozwe!
   
 15. P

  Peter lilayon Member

  #15
  Oct 2, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua nini mwombe mungu mwanangu ndo mpango mzima alafu fanya urafiki na wasichana wengi esp wale unao wataka ili uweze kusort, hela ndo kila kitu mzee make more frind 2mia hela jaman.
   
 16. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  unamvuto wa nje Huna swaga kwa madem ndo maana wanakupotezea be flexible jichanganye na watu mademu wako wengi sana afu usisahau ku hangout clasic areas.kila la kheri
   
 17. ZIPOMPAPOMPA

  ZIPOMPAPOMPA Member

  #17
  Oct 2, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ni mawazo yako mkuu.
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hakuna hata binti unayeona ana kidalili cha kumind swaga zako? Au unawafungia vioo?
   
 19. v

  valid statement JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  hah hah hahaaa teh teh teh... Jamaa anasubiri atongozwe kama alivokuwa 4m 6 teh teh.
   
 20. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  jitahidi kutenda mema
   
Loading...