Nina shambuliwa na mawazo ya kutaka kujiua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina shambuliwa na mawazo ya kutaka kujiua

Discussion in 'JF Doctor' started by Anne Maria, Jun 24, 2012.

 1. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa siku hizi mbili mfululizo nimekua nikipata sana mawazo ya kujiua kila ikitokea nafasi ya kuweza kujiua nawaza kujiua
  Jana nilikua nimepakia kwenye gari natokea masafa marefu na milango haikua imelokiwa,, kwahiyo kila wakati wazo linanijia kuwa nifungue mlango na kujitupa katikati ya barabara wakati gari lipo kwenye speed ya juu,, na leo tena mawazo hayo yameniandama siku nzima,, nikaamua kuwashirikisha dada zangu wakaniuliza kama nina kitu kinani depress lakini sioni kama nina jambo lolote linalo ni depress i feel fine,, am happy lakini sijui kwanini kila wakati napata kishawishi cha kujiua.... kiukweli nakosa raha kwa sababu ya hali hii leo nusura nifungue mlango wa gari wakati ipo kwenye kasi ya ajabu barabarani
  Naombeni mnisaidie hili ni tatizo la kiakili ama ni nini?? ninahitaji kupatiwa tiba yoyote ya hospitali?

  NB hii hali hiko nyuma ilishawahi kunitokea mara kadhaa ila nikaweza kujikaza na kuishinda nilisali na kuombewa lakini kwa sasa naona imekuja kwa nguvu zaidi..kusali ninaendelea ila najiuliza kwa nini linanijia?
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hili ni tatizo la kiakili, hebu nenda hospital, kama upo Dar nenda Muhimbili kamwone Dr Hogan au Dr Frank watakusaidia. Afu kipindi hiki acha kuendesha gari mpaka hali hiyo itakapoondoka. Pole sana
   
 3. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,681
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Pole, na uhakika wakati Unafikiria hayo siaminia Kama unakuwa kwenye full control of your mind, Kama huna any depression then hii ni issue inayoitaji Maombi.


   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  Pole sana. Umefanya la maana sana kuwashirikisha dada zako waombe wasikuache uwe pekee yako na unapokuwa kwenye gari hakikisha kunakuwa na mtu pembeni yako ambaye yuko karibu na mlango. Pia itakuwa ni vizuri sana ukaenda hospitali ili kuwaona wataalamu ili wakusaidie na tatizo hili kubwa, sala pia ni muhimu sana ili kuepukana na hali hii. Nakuombea Mungu ili hali hii ya kutaka kusitisha uhai wako uachane nayo.
   
 5. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  pole sana kwa hali hiyo ndugu. ila naona umeweka mipaka ya ushauri wa namna ya kuondokana na tatizo hilo, eti "tiba yoyote ya hospitalini"

  Fanya yafuatayo:
  • Kama unaishi sehemu ambayo unajitegemea kwa chakula na maradhi (yaani huwa unapata wakati wa kuwaza leo ntakula nini), ondoka nenda kwa ndugu ambaye uko huru sana ukiwa kwake hasa wazazi kama wapo.(kinachotakiwa hapa upate pumziko la bila kuwaza utakula nini. we ule kile watakacho tafuta wazazi)
  • Ikiwa ulizoea kukaa katika familia ya watu wengi yenye ucheshi na pilikapilika za aina mbalimbali na sasa umeondokana nayo, basi ni wakati muafaka wa kutembelea familia hiyo kila Unapohisi hali hiyo inakujia
  • Fuatilia mwenendo wako wa tabia, kama uko katika kipindi cha kujifunza tabia fulani mbaya mf. kuiba, ukatili, uchawi, umalaya, kutukana, dhuluma n.k ambazo hukuwahi kuwa nazo hapo mwanzo achana nazo kabisa hata kama ni kwa ushawishi wa watu wanaokzunguka. Ni bora wakwite fara usalimike kuliko kutimiza matakwa yao uangamie.
  • Kama wewe ni mtu wa kujitenga sana na watu(ant-social) achana na tabia hiyo, wakati wote jumuika na watu upige story mbalimbali na kama huna marafiki basi badili tabia zako mbaya.
  • Jaribu kukumbuka kama kunanadhiri yoyote uliwahi kuweka, kwamba ufe endapo ikiivunja au usipoitimiliza. Na sasa umekwenda kinyume na hiyo nadhili. Kama ndivyo hivyo, basi kama ulivyoamini ktk nadhili,Kwa imani yoyote iliyo kuu kuliko hiyo ya nadhili utaweza kuondokana na hiyo nadhili.
  • hii ya mwisho ni sababu ya kiimani zaidi, yawezekana kuna roho ya mauti inakuandama bila kujali imetokana na nini. Mimi naamini kwamba ukiombewa(yaani hiyo roho ya mauti ikemewe na ikuachie) utapona kabisaa. Ila kama kunauovu unafanya uachane nao na umrudie Mungu wako,vinginevyo hata ukiombewa itatoka na kurudi tena ukiirudia dhambi.
  hata mfadhaiko wa mawazo husababisha hali kama hii,lakini nimeona umekataa kwamba huna mfadhaiko wowote.


  MAOMBI NDIO DAWA YA HILO TATIZO. NIKIWA SHULENI MKWAWA SEC KABLA HAKIJAWA CHUO, HALI HII ILIKUWA IKIMPATA DADA MMOJA HIVI AMBAYE KILA MARA ALIKUWA ANAFANYA MAJARIBIO YA KUJIUA NA KUOKOLEWA NA WATU. ALIKUWA AKIOMBEWA MAPEPO YANASEMA YAMETUMWA NA SHANGAZI YAKE KUMSABABISHIA AJIUE ILI ASIENDELEE NA MASOMO. AKIOMBEWA ALIKUWA ANAOKOKA NA KUPONA LAKINI BAADA YA MWEZI ANARUDIA UOVU NA SAKATA LAKE LINAANZA TENA. MWISHOWE ALIFUKUZWA SHULE KWA UTOVU WA NIDHAMU. SIJUI IKUWAJE HUKO ALIKOELEKEA
   
 6. leh

  leh JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  na mie natanguliza pole zangu, sina cha kuongeza naona salosalo kaafunika yote ila hii ya roho na kuombewa.. sipo kabisa
   
 7. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jitupe tu barabarani,hutakufa!
   
 8. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  pole sana bidada, ushauri umeshapewa fanya yote uliyoshauriwa hapo juu na mwisho usisahau kukemea hiyo spirit of death (pepo la kujiua, roho ya mauti) it is an issue!

  I am glad umeweka wazi, nusu ya ushindi tayari. I hope hao ndugu zako hawatafungwa kiimani na kudharau shida yako.
   
 9. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  embu jaribu kujiheshimu ndugu yng,mwenzako anaomba ushauri seriously wewe unaleta jokes.sio lazima kila kitu u-comment
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,953
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  pole sana bidada, nakushauri fuatilia ushauri wa salosalo na dr wa kwanza kabisa ili kutatua. Ila nikutie moyo Mungu akisha kuonyesha kitu basi jua kesha kitatua so huwez kujiua tena manake ameshamshinda huyo ibilisi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Yawezekana maisha yako yamekuwa monotonous kiasi cha kupoteza flavour. Unahitaji kubadili staili ya maisha, ipe upya fulani. Kama umefanikiwa sana, na una raha sana, jaribu kuachana na raha hizo na kuishi maisha ya kujinyima kidogo; nenda kijijini na sehemu zenye nature usikilize sauti za ndege na wanyama, nk. Kwa kubadili mtindo wa maisha na mazingira unaweza kuona tena upya wa maisha ktk maana nzuri zaidi.
   
 12. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,118
  Trophy Points: 280
  Ushauri wangu kwako ni huu, mpokee Yesu kristo awe Bwana na mwokozi wa maisha yako na umwombe akuondolee hayo yote yanayokukabiri. Naamini ukimwomba kwa dhati, utapata unalotaka.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,119
  Trophy Points: 280
  Pole sana ila mimi hali hio ilinipata nikiwa kidato cha nne na nilifikia stage ya kumeza piriton sikumbuki idadi yake pamoja klorokwini sita nilijiskia kufa ila mchana ule nilikula nikalala nikiamini sitaamka baada ya hapo nikawa headboy na mwenyekiti wa ukwata, sikumbuki kupata tena tatizo hilo; jitahidi kusali
   
 14. G

  GTesha JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 203
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kiembembe ni kama muhehe!
   
 15. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Omba sana dada ilo ni pepo la mauti
   
 16. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante nitafanya hivyo nikienda dar kwa sasa sipo tz
   
 17. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante Merrita ninaomba Mungu anisaidie,,..
   
 18. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Una maanisha nini hapa sijakuelewa
   
 19. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  pole kwa yaliyokupata kwahiyo hukupata tena hali ya kutaka kujiua?? uliombewa?? haukupata matibabu yoyote ya hospitali?
   
 20. Anne Maria

  Anne Maria JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  YESU KRISTO ni BWANA na Mwokozi wa maisha yangu na ndo maana ninamuomba sana bila kuchoka kama umenote huko nyuma nilishawahi kuipata hii hali nikaombewa na watumishi wa MUNGU na mimi kuomba ikaondoka ila kwa sasa imerudi tena na bado ninaomba lakini najiuliza kwa nini imejirudia tena kwa nguvu zaidi? asante sana kwa ushauri
   
Loading...