Nina shahada ya Uhandisi wa Mitambo, natafuta ajira

Engineer,unaweza ku overhaul engine ya 20KVA,500KVA?unauzoefu wa kufanya preventive maintainance kwenye diesel generators,air-conditions,unajua welding kidogo?
Au ukipata inabidi tukufundishe?
Ku overhaul engine, maintenance ya generarator na welding experience ninayo isipokuwa kwenye maswala ya air conditioning sijawahi fanya ila ni mwepesi kwenye kufundishika na ninaelewa haraka huku nikifanya kazi kwa usimamizi mdogo.

Kama kuna opportunity tupeane mkuu
 
Mwana TET mwenzangu pole aisee, ila nenda pale Alistair Pale kurasini karibu na uhamiaji ,wanaweza kukupokea kwa ajiri ya intern,...

Jaribu na simba logistics pale matumbi kama unaelekea tabata relini omba intern au kazi
Shukrani injinia mwenzangu, nitajihidi kufanya ivyo. Wacha niweke mambo sawa ili jumatatu mungu akipenda niyatekeleze hayo uliyonishauri
 
Ingia portal.ajira.go.tz kuna taasis wanataka ME , pia hata erb huwa wanatafutia graduate engineer sehemu ya intern,
Natamani kufanya hivyo mkuu na mpaka account ajira portal ninayo ila kikwazo sijajisajili na ERB na nafasi wanazozitoa kwasasa wanataka uwe registered na ERB.
KIKWAZO CHA KUTOJISAJILI NI PESA
 
Habari za wakati huu wakuu.

Mimi ni kijana muhitimu wa Shahada ya kwanza ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering) mwaka 2019 kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT). Naishi Mbagala, Dar es salaam

Najitokeza mbele yenu kuomba msaada wa kupata sehemu ya kujishikiza (internship, volunteer au kazi) ili walau maisha yaendelee maana hali imekuwa mbaya kwa upande wangu na familia kwa ujumla haswa ukizingatia Mimi ndie tegemezi na Mzee alishafariki siku nyingi.

Mbali na elimu yangu, kipaji nilichonacho ni ufundi wa vifaa vya electronics(Simu, tv, radio, feni nk), changamoto kubwa ni mtaji

NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI.
Jiunge na wengine au Jaribu kwenda Sido
 
Jiunge na wengine au Jaribu kwenda Sido
Shukrani mkuu kwa ushauri wako ila sijakuelewa ulivyonambia nijiunge na wengine ni wakina nani hao wengine na huko sido nipeleke maombi ya internship au kuna kazi zilizotangazwa ?
 
Ndiyo tatizo,, Elimu yetu ya kibongo haifundishi mtu kujiajiri inafundisha mtu kuajiriwa,,,, karibu mtaani kuuza machungwa,, nguo za mitumba,,dawa za meno,, sabuni,,bila kusahau kupaka kucha mademu na wamama......
 
Shukrani mkuu
 
Ajira portal wametangaza ajira university of dar es salaam wanahitaji workshop instructor, Tena hiyo nafasi iko Re-advertised ,semaa nini mpaka ERB, ..
 
Kuonana na CEO au HR bila appointment naye ni ngumu sana, ikitokea hiyo ni bahati, kwahiyo ukimpa mlinzi/receptionist documents zako mwambie akupelekee kwa muhusika hapo hapo, alafu akuletee feedback kama zimepokelewa au zimekataliwa, then mengine yatafuata huko mbeleni.
Mmmh!
Kwa jinsi watanzania walivyo na roho mbaya na ngumu, kwa huo mtindo wa kuwaamini hao walinzi na receptionist kuwa watamfikishia boss, tegemea sifuri.
Maofisini kumejaa fitna tu.
 
Mmmh!
Kwa jinsi watanzania walivyo na roho mbaya na ngumu, kwa huo mtindo wa kuwaamini hao walinzi na receptionist kuwa watamfikishia boss, tegemea sifuri.
Maofisini kumejaa fitna tu.
Siwezi kataa kwa hili, ila still bado wapo waaminifu na wenye roho safi pia , kwahiyo mazingira yakikulazimu kufanya hivyo, itakubidi tu.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ajira portal wametangaza ajira university of dar es salaam wanahitaji workshop instructor, Tena hiyo nafasi iko Re-advertised ,semaa nini mpaka ERB, ..
Hiyo ndio changamoto mkuu, sijajisajili na ERB
 
Bado natafuta fursa wakuu,

Kwa mwenye connection naomba tusaidiane.
 
Nami napenda kukutia moyo katika utafutaji wa kazi, maana changamoto hii inaweza kumpata mtu yeyote. Tofauti na sehemu za kutafutia kazi kama TaESA, ZoomTanzania na sehemu zilizotajwa na watangulizi wangu, tazama pia kazi ambayo haujasomea lakini unaweza kuifanya, k.v.

Customer Care kwenye shirika la simu, Kazi kwenye studio n.k. Hata kama kazi haiendani na "hadhi" ya elimu yako, ni hatua tosha kwa ajili ya kupanda hatua nyingine kadri unavyojitahidi kufahamiana na watu wa taaluma yako na kujitengenezea mtandao. Kwa uzoefu wangu, mashirika ya Tanzania hayana utamaduni wa kujibu baruapepe kwa wakati.

Nadhani ni vema kwenda moja kwa moja kwenye shirika husika, kuomba miadi na muhusika, na kuulizia mara kwa mara pale jibu linapochelewa.

Utapato kazi, tathmini uwezekano wa kuwa na bima ya ajira. Hii itakusaidia kuwa na kipato mbadala iwapo utapoteza kazi huku ukiendelea kutafuta kazi nyingine. Kwa mtu anayetegemewa na familia, jambo hili huweza kuwa la msingi katika karne yetu
 
Shukrani mkuu kwa kunitia moyo na ushauri wako wenye tija, kwa hakika nimejifunza jambo kutoka kwako.

ASANTE SANA.
 
Back
Top Bottom