Nina Shahada ya kwanza ya Rasilimali watu (Human Resource Management) Natafuta kazi au sehemu ya kujitolea

DaniBai

New Member
Jan 3, 2020
1
1
Hello!! Habari?

Kama kichwa hapo juu kunavyosema, natafuta kazi, iwe ya kujitolea au ya malipo kwangu sawa tu, ikiwa ya miezi kadhaa (mkataba), au namna yoyote in terms of time kwangu poa tu.

Kwa kifupi nina Shahada ya kwanza ya Rasilimali watu (Human Resource Management), kutoka chuo kikuu Mzumbe. Toka nchukue cheti mpaka sasa nakaribia mwaka nahustle tu kutafuta kazi au sehemu ya kujitolea, ukiachilia mbali interviews nlizofanya lakini mpaka sasa bila bila.

Hivyo napenda kutumia nafasi hii, kutangaza ninatafuta kazi ya HR au yoyote inayoendana na hiyo kama Administration. Naweza anza ngazi yoyote itakayopangwa kama vile assistant au nkiwa tu kwenye department kusaidia mambo itafaa zaidi, na nina imani thabiti nitadeliver.

Kupitia elimu ya darasani, research niliyofanya na kuandika (presented at Mzumbe University in May 2017), na uzoefu nilionao/kuupata, nimeweza kudevelop attributes mbalimbali na kuwa competent katika mambo hayo. Mfano wa mambo hayo ni kama Human Resources and Administrative functions, Administrative and Labour law, customer care and financial management, leadership, performance management, public private partnership na mengine mengi yanayoendana na Human Resources na utawala kwa ujumla (Management and Administration)

Kwa sasa napatikana Dar es salaam. Ila nina uwezo wa kwenda popote na kuishi popote ili mradi kazi ipo.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu. Natumaini ntapata mrejesho, au kupatiwa connection katika hili. Asante.

DaniBai (DanBy)

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom