Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 259
- 353
Ukimchukia au kama humpendi Rais Samia Suluhu uwe na sababu. Sio sababu tu, bali sababu za msingi ambazo unaweza kuzijengea hoja nzito na kila mja akakuelewa.
Kimsingi Rais Samia ndani ya siku 495 za Urais wake, amefanya makubwa katika kila sekta, wazungu wanasema 'No stone left unturned'. Kwenye kilimo sina cha kusema nadhani kila mtu anajua ongezeko la bajeti zaidi yaa 100% ya bajeti ya 2021/2022.
Kwenye elimu ndio habari, madarasa zaidi ya 15,000 ya shule za sekondari na shule za msingi yamejengwa ndani ya miezi mitatu tu. Kwa mara kwa kwanza katika historia ya nchi hii, hakuna mtoto alibaki nyumbani kusubiria majibu ya awamu ya pili baada ya matokeo kutangazwa, bali kila mtoto alipata darasa na alipata kiti na meza, na hakuna ada. Mama kaondoa kabisa ada ya kidato cha tano na sita na wanafunzi wa vyuo vikuu wameboreshewa zaidi mazingira ya mkopo wao wa elimu ya juu.
Katika afya, hivi sasa kila kuna mkakati wa kujenga zahanati kwenye kila tarafa na kuna nyingine tayari zimeshajengwa huku kila wilaya ikitengewe bil. 500 kupata hospitali ya Wilaya, Mama etu huyo, tunataka kitu gani watanzania?
Nina sababu zaidi milioni moja za kumsapoti Mama. Muda hautoshi kuzieleza hapa, ila kadiri siku zinavyokwenda mbele nitakuwa natoa kadhaa kama leo, hadi zitimie milioni 1. Ombi langu usicheze mbali na ukurasa huu kwa dondoo za kila siku.