Nina sababu 50+ za kutompa kura yangu JK,Wewe Je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina sababu 50+ za kutompa kura yangu JK,Wewe Je?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by makoye2009, Oct 28, 2010.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF na wapenda maendeleo na mabadiliko ya nchi hii bado siku 2 kuingia kwenye fainali za kinyang'anyiro cha Urais,Ubunge na Udiwani. Fainali hizo zitakuwa hapo tarehe 31/10/2010 kuanzia saa 12 asbh mpaka saa 10 jioni. Napenda kuweka mambo hadharani kwamba nina sababu 50 na zaidi za kutompa JK kura yangu pamoja na wafuasi wake wote. Sababu zenyewe ni hizi hapa:
  1. Kikwete na CCM yake alikataa kura yangu kama Mfanyakazi kwa kuninyima nyongeza ya MSHAHARA.
  2. Kikwete na CCM ameshindwa kutekeleza sera yake ya MAISHA BORA kwa kila Mtanzania badala yake imekuwa ni BORA MAISHA na MAISHA BORA KWA MAFISADI.
  3. Kikwete na CCM yake ameshindwa kuwalipa wazee wa iliyokuwa JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI.
  4. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia DHAHABU yetu kuleta maendeleo.
  5. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia TANZANITE yetu kuleta maendeleo.
  6. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia ALMASI yetu kuleta maendeleo.
  7. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia URANIUM yetu kuleta maendeleo.
  8. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia GAS yetu kuleta maendeleo.
  9. Kikwete na CCM yake ameshindwa kutumia MAJI,MITO yetu kuleta UMEME wa uhakika.
  10. Kikwete na CCM yake ameshindwa kukemea MAFISADI NDANI CCM.
  11. Kikwete na CCM yake amempigia kampeni LOWASSA mtuhumiwa wa Ufisadi.
  12. Kikwete na CCM yake amempigia kampeni MRAMBA mtuhumiwa wa Ufisadi.
  13. Kikwete na CCM yake amempigia kampeni CHENGE mtuhumiwa wa Ufisadi.
  14. Kikwete na CCM yake amempigia kampeni MRAMBA mtuhumiwa wa Ufisadi.
  15. Kikwete na CCM yake amekodisha RELI yetu kwa RITES ya INDIA na kuia.
  16. Kikwete na CCM yake ameshindwa kuteua bodi ya kuiendesha ATCL na sasa iko ICU.
  17. Kikwete na CCM yake ameshindwa kuteua CEO na bodi ya kuiendesha TTCL na sasa iko HOI.
  18. Kikwete na CCM yake amechelewa kuteua bodi ya kuindesha TANESCO na sasa INAJIKONGOJA.
  19. Kikwete na CCM yake ameshindwa kuzuia/kuua MBU na malaria inaendelea kuua kina mama na watoto.
  20. Kikwete na CCM yake ameshindwa KUWARUHUSU WANAFUNZI WA VYUO VIKUU kuja kupiga kura kwenye vituo vyao yaani Vyuo Vikuu.
  21. Kikwete na CCM yake wameonyesha ubaguzi wa Uraia kwa BASHE kwamba ni msomali na baada ya kupata mtu wao wakamrudishia Uraia tena wa kuzaliwa.
  22. Kikwete na CCM yake wameonyesha ubaguzi wa Uraia kwa WENJE kwamba si mzaliwa wa Tanzania baali ni MKENYA na NEC ikatupa nje madai yao.
  23. Kikwete na CCM yake ameoyesha udhaifu wa KIAFYA KWA KUANGUAKA ANGUKA jukwaani pale Jangwani.
  24. Kikwete na CCM yake ni WASHIRIKINA kwa kumruhusu Kigagula SHEIKH YAHYA kuwatisha watu kuwa ANALINDWA NA JINI.
  25. Kikwete na CCM yake ni mbinafsi na mchoyo kwa kuruhusu FAMILIA(Salma na RIZ1) KUMFANYIA KAMPENI.
  26. Kikwete na CCM yake wameonyesha UDINI kwa kuchagua viongozi wote waandamizi wa Kampeni zake kuwa ni WAISLAMU.
  27. Kikwete na CCM yake wamewatummia REDET kudanganya watu kuwa anakubalika.
  28. Kikwete na CCM yake wametumia JESHI kutisha wapiga kura wasijitokeze ili CCM washinde kwa kishindo.
  29. Kikwete na CCM yake ametoa AHADI zenye thamani ya Tshs.Trilioni 90 kiasi ambacho serikali yake haina na haiwezi kutekelezeka ahadi hizo.
  30. Kikwete na CCM yake wamekataa MIDAHALO ambayo inawapa Wananchi kukuliza na kuchambua sera za vyama. Kwa hiyo JK NA CCM ni waoga.
  31. Kikwete na CCM yake wamemzushia DR.SLAA kuwa amechukua mke wa mtu na kumpa rushwa MAHIMBO afungue kesi Mahakamani.
  32. Kikwete na CCM yake alimkingia kifua MKAPA asifunguliwe mashataka kwa kukiuka KATIBA NA MAADILI YA KAZI kwa kufanya biashara IKULU.
  33. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuzuia MAUAJI YA ALBINO.
  34. Kikwete na CCM wameshindwa KUONDOA MSONGAMANO WA MAGARI Dar-es-salama.
  35. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuimarisha Uchumi wa Tanzania kwa kutumia Raslimali tulizopewa na Mwenyezi Mungu.
  36. Kikwete na CCM kuwa Rais wa kusafiri KILA WAKTI KUTEMBEZA BAKULI LA OMBAOMBA na anapoulizwa umaskini wa Tanzania unatokana na nini anajibu kuwa HAJUI.
  37. Kikwete na CCM yake wameshindwa KUZUIA MFUMKO WA BEI na hivyo THAMANI YA SHILINGI YETU IMEZIDI KUPOROMOKA.
  38. Kikwete na CCM yake kwa karibu miaka 50 ya uongozi bado WANANCHI WAKE WANAKAA KWENYE NYUMBA ZA TEMBE NA MBAVU ZA MBWA.
  39. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuboresha ELIMU YA SEKONDARI kwa kujenga shule za KATA ZISIZOKUWA NA VIWANGO NA HAZINA WAALIMU.
  40. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuboresha ELIMU YA MSINGI ambako watoto wanamaliza darasa la SABA NA HAWAJUI KUSOMA.
  41. Kikwete na CCM yake tangu MV.BUKOBA IZME NA KUUA WATU 900+ ameshindwa kuleta meli mpya mpaka mwaka huu ndipo ametoa ahadi ya kuombea kura.
  42. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuwashtaki wamiliki wa kampuni ya KAGODA NI YA NANI.
  43. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuwashtaki wamiliki wa kampuni ya DEEP GREEN.
  44. Kikwete na CCM yake wameshindwa kuwashtaki wamiliki wa kampuni ya MEREMETA.
  45. Kikwete na CCM yake wamekataa kuwa ELIMU NA AFYA haziwezi kutolewa kwa kuwa ni gharama kubwa mno kuliko hiyo pesa inayoibiwa na MAFISADI.
  46. Kikwete na CCM yake wamekataa kuwa BEI ZA VIFAA VYA UJENZI haziwezi kushuka bei kwa vile gharama za uzalishaji ni kubwa mno kuliko hiyo pesa inayoibiwa na MAFISADI.
  47. Kikwete na CCM yake wanawaona wapinzani kama maadui wakati nao ni Watanzania kama wao.
  48. Kikwete na CCM yake walihusika na mauaji ya wafuasi wa CUF zaidi ya 25 mwaka 2000 ili waingie madarakani.
  49. Kikwete na CCM yake kutamka lugha zenye utata za kusema WAPINZANI WANATAKA KUMWAGA DAMU ilhali wao ndio wanaoanzisha vurugu kwa kuwatumia Green Guards ILI DAMU IMWAGIKE.
  50. Kikwete na CCM yake kutumia lugha za kifidhuli za kuwatukana Wapinzani kuwa ni MAJUHA WALIOJAA MATUSI.
  51. Kikwete NA CCM KUENDELEA KUTUMIA (MASHANGINGI) MAGARI YA ANASA YANAYOUZWA BEI MBAYA NA MATUMIZI MAKUBWA YA MAFUTA.
  52. Kikwete na CCM yake kuendelea kuwa na BARAZA LA MAWAZIRI KUBWA ILI AWAZE KUWAPA ULAJI MARAFIKI,NDUGU NA JAMAA(Serikali ya Kishkaji).
  53. +......Endeleza kama unayo sababu.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 3. T

  The King JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  Shule na hospitali zetu na jinsi mgonjwa aliye mahututi anavyopelekwa hospitali na mengineyo mengi sana
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu hizo rangi naona kama KALI SANA aisee!

  please naomba zibadilishe
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Kweli Inasikitisha sana! Kwa utajiri huu tulionao Eeeh Mola tukomboe!
   
 6. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,768
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Kwa style hii utategemea kupata Marubani, Waalimu, Madaktari, Ma engineer kweli? Chezea Elimu kama wanavyofanya CCM then uone gharama yake!! ni sumu inaambukiza kizazi hadi kizazi.
   
 7. J

  JIWE2 Senior Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  CCM mkafie mbali
   
Loading...