Nina plan ya kuja bongo ndugu zangu ila ningependa kujua hali ya usalama kwa sasa ikoje?

Hofu ya nini mkuu,? Mbona huku kuko salama. Amani na usalama imetamalaki nchini kote.
 
Ukija niambie niwe board guard wako nitakupokea karibu kwasasa Tanzania siyo sehemu salama kwa
Sio salama kvp bingwa? Imaana wasiojulikana bado wapo kazin au Panya road wanaendeleza operation zao?
 
Bongo hali shwari kabisa, amani 900%. Maisha mazuri tunakula raha tu njoo na hela tu usije kutupiga mizinga tu huku bongo, siku hizi tunatembelea mahamvee, machev, Ford, Navigators, na kila magari makubwa na mapana uyajuayo... TZ sasa ni zaidi ya Brunei..
Hahaha kumpiga mbongo kizinga ni sawa sawa na kumuomba nyoka miguu aisee. Kuhusu usalama kama unachoongea ni kwel basi ntashuka kuifariji familia
 
Nani kakudanganya wewe, wabongo tuko vizuri kifedha na maisha murua tu bata zinaliwa kama tuko CopaCabana au Miami beach.. Zile bata unazoziona zakina 50Cent, Rihanna, Kriss-brown, Bekham, Christiano Ronaldo tunazila tu hapa Bongo kila siku..
 
Kwanza kabisa napenda kutanguliza shikamoo kwa wakubwa, na habari gani kwa wale wa rika langu

Bila kupoteza muda leo nimekuja kwenu nikiwa na habari za kusikitisha kidogo baada ya kufiwa na ndugu yangu week iliyopita.

Nisingependa kuzungumzia sana kuhusu sababu ya kifo chake. Kwahiyo kwa desturi zetu (japo sio lazima) nahitajika kwenda nyumbani kuwafariji ndugu jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wetu.

Lakini sasa kabla ya kwenda ningependa kujua hali ya usalama wa nchi kwa sasa ikoje?

Je hawa wanaoitwa "Wasiojulikana", pia nasikia kuna wale wanaojiita Panya road, wengine sijui Mende wanyanyua kabati na wengine wengi wa aina hiyo bado wapo, na wanaendelea na operation zao kama kawaida? Au wameshadhibitiwa na vyombo vya usalama?

Nimeona kabla ya kuja kichwa kichwa ni bora niulizie hapa ili nipate uhakika wa majibu kwenu. Maana ndugu zangu kwa sasa wapo katika hali ya majonzi na ukizingatia wengine wanahitaji nifike tu bila kujua usalama wangu utakuwaje kwa siku nitazokuwa huko nyumbani.

So hao wa aina hiyo nikiwauliza wataniambia njoo tu hapa tuko salama kitu ambacho pengine ni kweli au sio kweli. So naamini nyinyi ndugu zangu mliopo humu mnafahamu zaidi kuliko sisi tulioko nje ya boda.

Waswahili wanasema nyumba usiolala au kuishi hauwezi kujua ubovu wake. Sio nifike nikiwa nimechoka na mchoko wa kutembea angani muda mrefu halafu usiku nivamiwe na Panya road tupigane mapanga kwa lengo la kuchukua kila nilichokuwa nacho, au nije nipotezwe na "Wasiojulikana" wakati mimi nimekuja kwa sababu ya msiba na sio kwa sababu nyingine yoyote.

Nikipata majibu tofauti na yale ninayoyahitaji mimi naua safari rasmi. Namalizia kwa kutoa shukrani kwa wote mliosoma na kutoa michango yenu mbalimbali kuhusu niliyouliza.

Asanteni sana.
Kama ndugu zako wako shwali ndo hali ilivo tunapambana kusaka ugali na kuondoa stress za kuisoma namba kwenye keyboard tu mengine shwali tu
 
Kaa hukohuko tuachie nchi yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom