Nina Pepo la kupendwa na wake za watu

famicho

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,157
2,699
Habari wanajamvi,

Kwa kweli nina tatizo la kupendwa na wake za watu, na mpaka hapa nishachangia kuvunja ndoa tatu katika maeneo tofauti.

Na kwa sasa kuna wawili wananiwinda kwa udi na uvumba. Mmoja kati yao amesema yupo tayari tukacheki kwanza afya, baada ya hapo anataka nimpe ujauzito kwani mume wake inaonekana ana matatizo ya kizazi.

Nimeleta humu ili mnijibu, je hii hali inayonikuta inasababishwa na nini? Na pia naombeni ushauri ni kwa jinsi gani naweza jikwamua kutoka katika hali hii, kwa maana naumia sana na haya mambo, hata amani sina maana najiona ni mkosefu na mtenda zambi kuu, hivyo sitaki kuendelea na hizi habari.

Karibuni kwa ushauri, nishaurini bila kunionea aibu wala upendeleo.
 
Endelea tu kupendwa maana hakuna namna ila upo siku watu watampenda Mke wako na watamkwea vzr tu
 
Pole ndugu subiri waje wenye elimu zaidi juu ya hayo mambo Kama ni spiritual au vpi watakushauri
 
Inavyoonekana wanawake wengi hawaridhishwi ndani ya ndoa zao hadi kutafuta msaada 'kwa jirani' na hili ndio hasa linaongeza ushawishi wa kuvunjika kwa ndoa nyingi. Wanaume wengi wameendekeza mipombe na viroba kitu kinachowapunguzia uwezo wa kushughulikia wake zao... Kwa kweli hili ni janga...
 
Kwel kabisa mkuu, mmoja ashawahi kuniambia ana miezi kadhaa hajawahi fika orgasm
 
Kwel kabisa mkuu, mmoja ashawahi kuniambia ana miezi kadhaa hajawahi fika orgasm
Duh! Moja ya njia ya kuepuka haya matatizo ni kuwa na mke wako kama bado hujaoa. Pia usiweke ukaribu sana na wanawake kiasi cha kukupa mwanya wa kuzoeana nao. Cha tatu kumbuka kumwomba Mwenyezi Mungu akupe ujasiri wa kukabiliana na vishawishi na kuweza kuvishinda...
 
Asante mkuu, i shall work on that
 
Sio kesi wewe endelea ila cha maana wewe inabidi uoe hili na sisi tukuharibie uone uchungu wake.
 
Duh! Moja ya njia ya kuepuka haya matatizo ni kuwa na mke wako kama bado hujaoa. Pia usiweke ukaribu sana na wanawake kiasi cha kukupa mwanya wa kuzoeana nao. Cha tatu kumbuka kumwomba Mwenyezi Mungu akupe ujasiri wa kukabiliana na vishawishi na kuweza kuvishinda...
Asiposikiliza huu ushauri basi tena
 
Cha msingi jua unachofanya ni uvunjifu wa amri ya 6 na ya 9 plus 10 kwenye zile amri 10 za Mungu kama zilivyoainishwa kwenye biblia.
Ujira wa dhambi ni mauti. Be sure that unachofanya ni kazi ambayo kama ilivyo ada kuwa kila kazi ina ujira wake na kwa hilo ujira wake ni mauti.
You have a chance to walk out from it all since your conscience is live and ready to repent. Do it while you still can.
Contrary to that Mzee, mi simoooooo na mchanga wa pwani huuuuuooooooo
 
Una umri gani? Hongera Sana kwa kupendwa na wake za watu na kuwafikisha orgasm.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom