Nina muonekano mzuri lakini mahusiano yangu hayadumu. Nini tatizo?

Nilivyosoma maelezo yako tayari nmegundua tabia yako. Kwanza unajiskia na kujiona kupitia hivyo vichache unavyomiliki na sura yako.
Wanawake wengi wanapenda security (usalama) katika nyanja zote yaani kiuchumi, kimahusiano na kijamii.
Kwa mujibu wa maelezo yako umeshindwa kuwahakikishia security wanahisi unaweza kuwaacha anytime.
Badilisha staili ya maisha...fikiria kama mtu mzima.
Mawazo ya kuplay yaache, chagua marafiki wenye haiba nzuri baadaye utapata mtu sahihi
 
Huyu akipewa mzigo hapigi, unafikiri nani atadumu na wewe.

Mwanamke atadumu na wewe ukiwa na fedha za kumtimizia mahitaji yake hata kama atachit bado ataendelea na wewe.

Kama unafedha ya kawaida na akikupa unampa mpaka anasema asante bai yaani anatosheka ujue hatakuacha kukuacha ni mpaka apate mtu atakayekuzidi kiuchumi na kimtooombo
 
Pole sana...

Punguza majigambo na majivuno...

Idadi kubwa ya wanawake wanachukia wanaume wenye sifa na wanaojigamba...

Kingine inawezekana huna nyota nao...


Cc: mahondaw
 
Piga picha pamoja na bibi yako, halafu jua wanaume wenye hamu ya mahusiano ya kudumu, wanakuona utakuwa kama bibi yako
 
kwahyo wakati uko mdgo ulinusurika kubemendwa? kwahiyo wameanza kukubemenda ukubwani kama una sura nzuri wanaume wanapenda sana ,mwanamke anaejielewa hataki sura maana mtakua ni sawa na ndoa ya jinsia moja
 
Asanteni sana nilishafanikiwa kwa wengi mliokuwa mnauliza kabila langu mimi ni msukuma sikutaja hapo mwanzo maana naelewa mada ambavyo ingebadilika. Shukrani kwa wote mlioshiriki
 
Umeeleza vizuri mdogo wangu ila haukuangalia hadhira unayoitumia ujumbe binafsi nimependezwa na ulivyofunguka ingawa wengi wamekuponda. Ushauri wangu usimfanye mwanamke wako kuwa insecure kwa sababu ya huo mwonekano wako naamini kama ni mwanamke kweli anayejielewa kama ulivyoeleza hapo awali basi yakulazimu umuheshimu. Kumpata mwanamke mzuri mwengine ni rahisi ila trust me kumpata mwanamke wa vigezo vikupendezayo huwa haitokei mara mbili ninazungumza haya kutokana na uzoefu. Hakikisha una mweka huyo mwanamke karibu na mfanye awe anakupenda zaidi kuliko kitu chengine chochote hivo visa ni kutokana na mapenzi yake kwako na anahofu sana ya kukupoteza kama ilivyo kwako
 
Usije ukawa harmorapa wewe hebu tuma picha yako tuone huo muonekano
 
japo wanakuponda ila somehow mimi nimekuelewa, umejisifia ili tuweze kukuelewa na jinsi ya kukusaida, nnachoweza tu kukwambia kwanza jiangalie una mtreat vp mtu unaekuwa nae kwenye mahusiano, tatizo wanaume wengi wazuri mnaringa mno, yani mnaona kama vile ni kazi ya mwanamke kuhakikisha ana fight for u, akunyenyekee ahangaike na wewe kisa tu wewe ni handsome hasa mnapokuwa na wasichana wenye muonekano wa kawaida huwa mnamashauzi sana na ni mateso kwa kweli, been there done that. Pili hakikisha kile unachokitaka kwenye mahusiano basi unakionyesha ili mwenzio aone mpo pamoja sio moyoni unataka mtu sahihi wa kutulia nae lakini kimatendo hueleweki unataka nini, achana na mambo ya kumuonyeshea mwenzio kwamba wewe unaweza kupata mwanamke yoyte wakati wowote hata kama humcheat lakini hicho kitendo cha kumuweka mwenzio roho juu si kizuri na hautakaa udumu na yoyote yule.


Kwani wanawake hamringi? Au utatetea kuringa kwenu kwasababu nyie ni wanawake mrsleo
 
Mwanaume unajisifiaje uzuri ati?
Utakuwa unashida.
Ujue wanawake hawako secured na wanaume wanaoonekana watavutia wengi zaidi yake.

Mwanaume tafuta hela, kula kiafya. Piga mzigo mpaka mtu akimbie na chu.pi mkononi. Hakuna atakuacha kirahisi
 
Mtoa Mada nimemuelewa vizuri sana.Nia sio kujisifia.Kwa yeye anashangaa hatishi kiasi akimbiwe.Ndo akaamua kuelezea alivyo.Wenyewe mnaita Handsome boy..
Tukija kwenye point ni kwamba wanawake hawapo kwa muonekano Japo mwanaume akiwa mfupi saaana( Emoro) ni tatizo lingine
Ila Kikubwa wanawake walio wengi wa nataka kuwa Na MTU wa Uhakika kwa maana a protective man kwa hali zote..
Unaona hapo Hakuna muonekano .
Pia the way you treat your partner matters a lot
Ndo Mana unaweza kuta msichana alisalitiwa Na huyu mwanaume akamwacha but inakuwa ngumu kumsahau remembering those precious and good treatments given.
Sio kwamba wanaume wengine hawapo au hawajamtaka but what any lady need is good treatment and being taken care of.
A man with care Conquers the heart of a lady with sweet words.
 
We ndo huyu
tapatalk_1562434960468.jpeg
 
MDOGO WANGU ANAHITAJI MSAADA WAKUU,

Mimi ni kijana mwenye umri kati ya miaka 20-25 mwenye asili ya mmoja ya wapo ya kabila kubwa la nyanda za kaskazini nchini. Ni kijana handsome boy (huambiwa hilo na wanawake takribani kila siku pia nimekuwa na marafiki wengi wa kiume ambao wamejenga urafiki na mimi wakiamini huwarahisishia kujuana na wanawake wazuri).

Pamoja na Hayo wanawake wengi sana hunionyesha wazi kutaka kuwa na mahusiano na mimi niliosawa nao sawa kiumri na walionizidi umri (nimenusurika kubemendwa mara nyingi sana wakati nilipokuwa mdogo).

Mbali na kuwa na mwonekano unaowavutia watu wa jinsia tofauti na yangu nimekuwa na tatizo la mahusiano yangu kutodumu. Mahusiano ya kimapenzi nimeanza tangu nikiwa na umri wa miaka 14 lakini sijawahi kuwa na mahusiano yaliyodumu hata miaka 2,

Sincerely speaking sijawahi kuwa na mwanamke ambae nilimuona tunaweza kuwa na future naye mpaka nilipofika chuo kikuu. Pamoja na kupata mwanamke huyo ambae moyoni nilisema sasa nimepata mtu niliyekuwa natamani kuwa nae kwani ana tabia, mwonekano na attitude niipendayo mimi.

Lakini mahusiano yangu na yeye yamekuwa ni mchezo wa paka na panya, kila siku ni visa na hamna kuaminiana yaani yeye huhisi na msaliti mda wote na kila siku hujipeleka kwa wanaume wengine ili kunifanya niwe na wivu mwisho wa siku nimegombana na wanaume wengi sana kwasababu yake.

Lengo la kuandika hii nakala ni kuomba ushauri kwani kama kijana mtafutaji na mwenye malengo ya kufanikiwa nafahamu umuhimu wa kuwa committed na mahusiano mmoja na hivyo kujiepusha na umalaya.

KI-TABIA:
Mimi ni mwanaume mstarabu(nina muheshimu kila ananiheshimu+anayejiheshimu), siyo mzungumzaji sana (msikilizaji zaidi), Mtu nisiyependa kujadili maswala ya watu binafsi( wengi huniamini sana na siri zao), ni open minded person (sifahamu Kiswahili chake),

WASIFU:
Ni mwanafunzi wa chuo kikuu anayekaribia kumaliza chuo kikuu hivi karibuni, ki wadhifa wa kifedha nipo wastani ( nina gari ingawa uwezo kutembea nao kila safari bado sina), Nina exposure kidogo ya kusafiri nje hasa nchi za ndani ya bara la Afrika, Nimezaliwa na kukulia Dar hivyo harakati zangu nyingi za utafutaji zinafanana na vijana wengi wa hapa mjini.
Ungemalizia tu kusema unatafuta girlfriend
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom