Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Uzi mzuri ila haya mambo ya vilemba bwana🤣🤣
Nilichogundua kilemba ndio changamoto inayofanya biashara iwe ya faida nyingi maana haiwi na watu wengi sana watakaoshusha bei ya bidhaa,inavyoonekana ukitoboa kwenye kilemba basi umeshatoboa kibiashara.😃
 
Kingine ni vile watu hawana uaminifu vinginevyo mnaungana wawili au watatu, mnakuza mtaji mwisho wa siku kila mtu anaweza kuwa na fremu yake.
 
Usinunue mazao na kuweka store nenda sokoni uwe unanunua nafaka kwa wakulima na wale wanaotoa vijiji, we uwe unauza kama wholesale
Ukiwa unanunua afu unaweka store ukisubili price kupanda hiyo sio biashara bali ni kamali cos posibility ya kushuka inakuwepo kubwa

Ushauli wangu: Fanya research ya nafaka unayotaka kuuza mfano mchele anzia wanakonunulia(kobolewa) inaweza ikawa Kahama, Mpanda, Mbeya n.k ili kujua season kwa mwaka ukimaliza tafuta store town hapa wanapouza nafaka agiza au uwe unaenda mwenyewe mwanzo hautakuwa unapata faida kubwa ila kadri muda unavyozidi kwenda faida utayona tena kubwa kubwa.

Mwisho wasiku utapata wenyeji wa maeneo uliyochulia mzigo watakuwa wanajua wewe unataka mchele wa aina gani so itakuwa rahisi kwao kukutumia mzigo unao utaka au una mechi na soko lako

Nb: Ninapatikana Moshi (kiusa) jilani na panoni petro station nauza maharage na mchele kutoka kahama grade 1 kiroba 50kg 85000 kwa kilo 1700 na grade 2 kiroba 50kg 75000 kwa kilo 1500 na maharage price ya sokoni kwa jumla 2200 ya songea na 2300 kwa yanayotea sanya juu hapahapa moshi
Kyusa street karibu na madogo wanachoma kuku wa kienyeji jioni!!? Nitakuja kukuungisha nikija pande hizo.
 
Hiyo hela yako utaipoteza mkuu ukienda Kkoo. Licha ya kwamba biashara si nzuri hapo lakini huo mtaji utaenda kuchoma. Kwanza kilemba tu hata hiyo 35 yako itapotea. Me nadhan nenda mkoa unaoanza kuchipukia. Ama fanya biashara ingine mtaani
Mkuu kilemba ndo nini?
 
Niyie mpo dunia ya ngapi wakuu achana na hao watakupoteza kabisa kabisa mkuu

FAIDA YA HARAKA NA KWA WINGI

Bayern
Madrid
Man City
Dortmund
Inter
Juve
Celtic
Piga 7 X 34 = halafu ukipata hiyo hela toa % 20 iliyobaki yote ni yako mkuu hapa wazee wa mikeka wataelewa hii plan

USHAURI WA BURE

Nunua au jenga lodge sehemu nzuri waka na vinywaji na chakula

Usafarishaji nunua coster fanya daladala

Au ukishindwa vyote hiyo pesa itapotea kama upepo tu nawasilisha
hahahahahah yaani akabet
 
Wakuu nimebangaiza nimefanikiwa kuweka Milioni 35 nataka kuingia katika biashara Kariakoo, nifanye biashara gani?


Michango ya wadau






Zaidi soma>>
Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)
Mkuu nimepitia mawazo ya watu wengi sana hapa ni mazuri, ila wakati mwingine kila mtu anaiona biashara kulingana na upande aliosimama mfano pharmacist kukushauri ufungue pharmacy ni rahisi sanaa ila unaweza kukuta wewe na pharmacy ni giza ( simaanishi kuwa haiwezekani).Ushauri wangu kwako kwanza angalia kile kitu ambacho wew kwa mazingira yako unaweza kukifanya vizuri kabisa then chukua hatua tafuta ''mentor'' mtu atakayekushauri kuhusu hicho unachotaka kufanya halafu usiogope kupoteza muda chukua hata miezi sita ili kujua kwa usahihi unachotaka kufanya, kariakoo sio lazima sana uanze na fremu kubwa kuna vigoli pia laikin hakikisha lazima umpate mentor kabla ya kufanya chochote.
 
Back
Top Bottom