Nina mtaji wa milioni 20 nataka kufanya biashara ya duka la jumla la vyakula

Abby92

Member
Feb 8, 2019
7
95
Wakuu habari zenu, najua wengi humu ndani mnayo mawazo mazuri na wengine mnazo hadi experience (Uzoefu) wa baadhi ya mambo hasa katika biashara. Mimi ni mbobezi wa masuala ya Online (Mtandaoni) sasa nina kafungu cha mtaji wa milioni 20 nikawaza niwekeze kwenye biashara nje na field yangu ya kazi.

Mimi nipo Dar es salaam.

Wazo lililonijia ghafla ni kuwekeza katika duka la jumla la vyakula, yani nifungue duka la jumla litakalouza vitu kama mafuta ya kula, mchele, sukari, sabuni, unga nk. kwa jumla lakini. Nikasema ni share na huku labda naweza nikapata mawazo mazuri zaidi. Lengo ni kuwekeza kwenye biashara amabayo itanizalishia faida kwa speed (Haraka) na ambayo haitakuwa inanigharimu muda wangu. Yaani biashara ambayo ninaweza nikawa naisimamia hata kama nikiwa mbali.

Kama unawazo la biashara nyingine ambayo naweza kuifanya kwa mtaji wa Tsh milioni 20 nakukaribisha kwani mawazo yako ni muhimu sana kwangu na kwa wote watakao soma uzii huu.

Karibu.
 
Mikopo Chefuchefu

JF-Expert Member
May 15, 2017
3,399
2,000
Unataka kufa kwa presha wewe. Ni bora ufungue hardware. Hata usipopata wateja vitu haviozi.
Pia ukiweke faida ya asilimia ishirini, ukiuza vitu vya milioni moja, una laki mbili ndani...
 
MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
516
500
Chukua hii Ingia front mwenyewe mwanzo fika Mbeya angalia bei za mchele zinachezea 1200 hadi 1000 kwa kopo/Kilo chukua mchele ule supa kabisa sogeza DSM pack vizuri kuanzia nusu hadi 10kg then wekeza kwenye matangazo piga promo ya kufa kiumbe faida yake utaniambia.

Chakula hakikutupi mambo ya hardware sijui nini uchumi umeyumba sasa watu wamepunguza speed ya kujenga na ujue wapo mataycoon wa hiyo mambo na wanatoa na offa & free delivery
 
Fuqin

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
200
500
Abby92,
Kwa uzoefu wangu biashara hiyo unayoitaka sio mbaya ila mtaji wako bado mdogo angalau ml 50 ndo ungeweza kufanya biashara hiyo... kwanza sehem ya biashara iwe kubwa kwahyo kwa mwaka kodi itafika ml 5 hivii... mafuta kuna aina nyingi na zote uwe nazo, dumu , ndoo ndogo,ndoo kubwa, lita 3 , lita 1, kuna kila kampuni uwe nayo hapo tuu ml utakata ml 5... ngano kuna kila aina kilo 50, kilo 25,kilo 5, kuna ngano ya mo, ya bakhresa,kuna azania, hapo napo ml 3..

kuna sabuni ya unga ya kilo 15 zipo kmpuni kama 6 hivi na zote uwe nazo (klin,foma,kleesoft,mo safi, family) kuna sabuni za kuogea kila kampuni uwe nayo, kuna sabuni za miche kila kampuni uwe nazo, kuna sabunia za unga za kilo 1, nusu kilo, gram 250, kuna za Omo na Ariel, hapo utakata ml 5... bidhaa zipo nyingi sana siwezi kuorodhesha zote hapa... kuna pampes.. ndala... vinywaji kila aina ... bettri... pipi kila aina... unga wa sembe ... sukari na vyoote hivyo unatakiwa ununue kwa wingi kwa sababu ni duka la jumla ..... na hapo bado hujalipia tra. Kwahyo kama umeamua kufanya biashara hiyo taarisha ml 50 hivi kwa ushauri wangu ila kama ukiona mimi nakudanganya fanya reseach

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fuqin

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
200
500
Sawa mkuu, Je unaweza ukanishauri biashara gani ninaweza kuifanya kwa iyoo elaa?
Mimi nakushauri tafuta frem maeneo ya sokoni panapouzwa mchele wa jumla then uende mbeya ukafate mchele hapo utapiga kazi fresh... ila fanya research ujue bei za kila mchele sio ukurupuke kwenda ukanunua bei kubwa ukashindwa kuuza... think then do.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kizito2009

Senior Member
Jan 6, 2010
171
250
Wakuu habari zenu, najua wengi humu ndani mnayo mawazo mazuri na wengine mnazo hadi experience (Uzoefu) wa baadhi ya mambo hasa katika biashara. Mimi ni mbobezi wa masuala ya Online (Mtandaoni) sasa nina kafungu cha mtaji wa milioni 20 nikawaza niwekeze kwenye biashara nje na field yangu ya kazi.

Mimi nipo Dar es salaam.

Wazo lililonijia ghafla ni kuwekeza katika duka la jumla la vyakula, yani nifungue duka la jumla litakalouza vitu kama mafuta ya kula, mchele, sukari, sabuni, unga nk. kwa jumla lakini. Nikasema ni share na huku labda naweza nikapata mawazo mazuri zaidi. Lengo ni kuwekeza kwenye biashara amabayo itanizalishia faida kwa speed (Haraka) na ambayo haitakuwa inanigharimu muda wangu. Yaani biashara ambayo ninaweza nikawa naisimamia hata kama nikiwa mbali.

Kama unawazo la biashara nyingine ambayo naweza kuifanya kwa mtaji wa Tsh milioni 20 nakukaribisha kwani mawazo yako ni muhimu sana kwangu na kwa wote watakao soma uzii huu.

Karibu.
HOngera kwa kuwa na Milioni 20.Kiukweli hio biashra sio ya kusimamia ukiwa mbali.Faida ya biashara ya jumla ni ndogo hivo kama wafanyakazi sio waaminifu ni rahisi kujikuta unakula hasara.

Vile vile ni muhimu uwe na uzoefu angala na biashara ya duka la rejaraa kwanza kabla ya kufikiri duka la Jumla.Unaweza fungua duka la Rejareja la milioni 20 na ukatengeneza faida nzuri.Na kwa kuwa umesema biashara yako ni ya online basi unaweza hata kuweka kanafasi hapo dukani unakaa na unaunganishwa na internet unafanya kazi kwa bidiii kabisa.
 
Dukani

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
999
2,000
Sawa mkuu, Je unaweza ukanishauri biashara gani ninaweza kuifanya kwa iyoo elaa?
Labda ufanye biashara ya kuuza mchele tuu,, unaenda shamba kule kwenye zile mashine unanunua mchele bei poa ukija unaugred unapack unautangaza then unaingia sokoni utaniambia mkuu hela hapo zipo nje nje. Baada ya kugred utapata zile chenga unauza kwa wamama wauza vitumbua mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,512
2,000
Nahitaji kufanya biashara, na nimeshaanda mtaji kiasi cha zaidi ya milioni 20 , Tatizo langu nashindwa nifanye biashara gani na nianze vipi.

Yaani ugumu ninaokumbana nao ni aina ya biashara ambayo naweza kuanza nayo katika mazingira haya yanayotawaliwa na mabepari
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
17,849
2,000
Nahitaji kufanya biashara, na nimeshaanda mtaji kiasi cha zaidi ya milioni 20 , Tatizo langu nashindwa nifanye biashara gani na nianze vipi.

Yaani ugumu ninaokumbana nao ni aina ya biashara ambayo naweza kuanza nayo katika mazingira haya yanayotawaliwa na mabepari
Natamani nikuambia ufanye biashara iyo iliyokuingizia 20m.
 
Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
5,958
2,000
Nahitaji kufanya biashara, na nimeshaanda mtaji kiasi cha zaidi ya milioni 20 , Tatizo langu nashindwa nifanye biashara gani na nianze vipi.

Yaani ugumu ninaokumbana nao ni aina ya biashara ambayo naweza kuanza nayo katika mazingira haya yanayotawaliwa na mabepari
Nahitaji kufanya biashara, na nimeshaanda mtaji kiasi cha zaidi ya milioni 20 , Tatizo langu nashindwa nifanye biashara gani na nianze vipi.

Yaani ugumu ninaokumbana nao ni aina ya biashara ambayo naweza kuanza nayo katika mazingira haya yanayotawaliwa na mabepari
Ukitaka huo Fedha yake iendelee kukua fanya Bishara/kazi ambayo ulikua unaifanya mpaka ukapata hizo mil20
 
Mk54

JF-Expert Member
Dec 29, 2016
1,709
2,000
Abby92,
Kwa uzoefu wangu biashara hiyo unayoitaka sio mbaya ila mtaji wako bado mdogo angalau ml 50 ndo ungeweza kufanya biashara hiyo... kwanza sehem ya biashara iwe kubwa kwahyo kwa mwaka kodi itafika ml 5 hivii... mafuta kuna aina nyingi na zote uwe nazo, dumu , ndoo ndogo,ndoo kubwa, lita 3 , lita 1, kuna kila kampuni uwe nayo hapo tuu ml utakata ml 5... ngano kuna kila aina kilo 50, kilo 25,kilo 5, kuna ngano ya mo, ya bakhresa,kuna azania, hapo napo ml 3..

kuna sabuni ya unga ya kilo 15 zipo kmpuni kama 6 hivi na zote uwe nazo (klin,foma,kleesoft,mo safi, family) kuna sabuni za kuogea kila kampuni uwe nayo, kuna sabuni za miche kila kampuni uwe nazo, kuna sabunia za unga za kilo 1, nusu kilo, gram 250, kuna za Omo na Ariel, hapo utakata ml 5... bidhaa zipo nyingi sana siwezi kuorodhesha zote hapa... kuna pampes.. ndala... vinywaji kila aina ... bettri... pipi kila aina... unga wa sembe ... sukari na vyoote hivyo unatakiwa ununue kwa wingi kwa sababu ni duka la jumla ..... na hapo bado hujalipia tra. Kwahyo kama umeamua kufanya biashara hiyo taarisha ml 50 hivi kwa ushauri wangu ila kama ukiona mimi nakudanganya fanya reseach

Sent using Jamii Forums mobile app

Anaweza kuanza na Fast Moving Items, not necessarily awe na vitu vyote au brands zote. Nadhani afanye Utafiti kujua brands zinazotumika sana .

Na pia apate sehemu yenye Movement na frame bajeti iwe kuanzia laki2 hadi 5 lol
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom