Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Mugaji

Member
Jan 26, 2012
13
17
Duka.jpg

Wana JF naombeni ushauri wenu zikiwemo changamoto zake.

Baada ya kukaa na kufikiria kwa muda mrefu na kupata maoni mbalimbali hasa kutoka humu JF sasa nahisi ni wakati wa kuweka wazo langu hapa mnipe ushauri.Nafikiria kufanya biashara ya kuuza vipodozi kwa jumla na rejareja.Sehemu ninayofikiria kufungua ni Mbeya.Sasa nahitaji kusaidiwa ktk mambo ya fuatayo:

1.Utaratibu wa kuprocess kibali unaanzia wapi.
2.Sehemu(miji) za kuchukulia mzigo kwa kuzingatia unafuu wa kuchukulia na kusafirisha.
3.At least mtaji kwa kuanzia(kwa sasa nina 10M)
4.Napenda pia kujua rate ya profit
5.Nahitaji kujua risks ninazotarajia ku-encounter mbele ya safari.

Naomba kuwasilisha.


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUELEWA BIASHARA HII
Salaam,

Natumai muwazima wa afya, yoyote atakae bahatika kuuona uzi huu basi asiache kutoa chochote kitu ambacho kitanisaidia sana kuongeza maarifa katika hii maada niliyo ileta kwenu nikiamini kabisa kuwa nyie ndio watu wa pekee wa kunipa msaada kimawazo

Natamani na napenda sana kufanya biashara ya vipodozi (cosmetics) nasikia tu kwa watu kuwa ina mslahi sana lakini changamoto ni kwamba Sina ufahamu mkubwa sana kuhusu biashara hii mfano nilishajiuliza maswali kama.

1. Ni kiasi gani cha mtaji kinahitajika (minimum amount of capital)
2. Ni vipodozi vya aina gani vyenye uhitaji mkubwa sana sokoni(consumer needs)
3. Ni vipodozi gani vina faida kubwa sana
4. Hasara ambazo unaweza pata
5. Sehemu ya kuweka duka (Matter of location)
6. Sehemu nzuri ambayo naweza fungasha mzigo kwa bei rahisi sana( iwe nje au hata ndani ya nchi hapa mkoa wowote ule)

Na vitu vingine vingi tu ambavyo watu huwa wanazingatia pindi wanapo amua kuanzisha biashara

NAOMBA MSAADA WAKO KATIKA HILI MWANA JF

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wana jamvi,

Natarajia kufanya biashara hii ya duka la vipodozi kwa mkoa wa arusha, naomba kufahamu angalau kidogo kwa wenzangu wanao fanya biashara hii, mzigo huwa mnachukulia wapi, na changamoto zake pia zikoje.



MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
ABC's ZA BIASHARA HII

Mimi nafanya biashara ya vipodozi, pia ni mtaalam wa masuala ya urembo, vipodozi na afya. Kwa sasa siuzi tena kupitia duka langu bali naviuza kwa njia zingine na nashukuru Mungu mambo mengi nayajua vizuri na biashara inaendelea vizuri.

1. UTARATIBU WA KUANZIA
Kwanza inabidi upate eneo zuri na lenye nafasi ya kutosha kuweka vipodozi vyako na kufanya biashara hii. Jengo liwe na mwanga wa kutosha na liruhusu mzunguko mzuri wa hewa

Pili inabidi uwe na namba ya mlipa kodi (TIN) kutoka TRA kwa ajili ya kulipia kodi biashara yako na kupatia leseni manispaa

Tatu inabidi uende wilayani/manispaa unakotaka kufanyia hiyo biashara au ofisi za TANZANIA FOODS AND DRUGS AUTHORITY (TFDA) kama ipo karibu yako.

Hapo utaonana na watu wanaohusika na leseni za biashara za vipodozi kwa ajili ya ukaguzi wa eneo unalotaka kufanyia biashara ya vipodozi. Watakutoza ada ya ukaguzi.

Wakikagua na kukubaliana na eneo lako basi watakutaka ulipie kibali na leseni ili uweze kuruhusiwa kufanya biashara hiyo katika eneo hilo.
Taratibu zote za serikalini zikikubali basi hapo sasa utakuwa na baraka zote kuanza biashara hii.

2. MTAJI
Hakuna kiasi maalum cha mtaji ambacho unatakiwa kuanza nacho, cha msingi ni wewe mwenyewe unajiwezaje, duka lako ni size gani na unataka liwe la hadhi gani na kuwa na vitu gani.

Gharama kubwa zipo kwenye kodi ya jengo la biashara, shelf na makabati ya aluminium na vipodozi vya bei kubwa kama vile perfume original

Kwa hiyo nashindwa kusaidia kiasi cha mtaji cha kuanzia, lakini kwa kununua baadhi ya vipodozi vya kuanzia tu peke yake na kwa duka la ukubwa wa wastani basi million 5 inatosha. Cha msingi kuwa na plan kubwa na ya muda mrefu lakini unaianza mdogo mdogo bila kusimama.

3. CHANGAMOTO
Hakuna biashara isiyo na changamoto. Changamoto kubwa kwenye biashara ya vipodozi ni matakwa ya wateja na serikali.

Wateja wengi hupenda vipodozi ambavyo serikali imevipiga marufuku, feki/copy na vya bei ya chini kwa kuwa ndivyo huwaletea matokeo wanayoyataka haraka haraka japokuwa vinawaharibu sana baadae na kuathiri afya zao

Unatakiwa kutoa risiti kwa kila kipodozi utakachouza na kutunza kumbukumbu vizuri kwa ajili ya makadirio ya kodi. Ni marufuku kuweka vipodozi na bidhaa ambazo hazitakiwi, hata kama ndivyo vina wateja wengi na kukuletea faida kubwa

Kuna ukaguzi wa mara kwa mara na muda wowote unaweza ukapoteza biashara yako kama utakamatwa umeweka bidhaa zilizokatazwa

Kwa maelezo zaidi na ushauri wa kitaalam na kibiashara nawakaribisha ndugu na marafiki zangu nyote ambao mngependa kufanya biashara hii nzuri tuwasiliane ili niwape na documents zake muweze kuanza na kuendesha biashara hii vizuri.

/QUOTE]
Wengi hununua Kariakoo. Kwani wale wa Kariakoo huagiza kwa makontena kutoka nje (dubai na sehemu) nyingine nyingi tu!

Opposite filling station ya Big Bon, kuna maduka, ila wewe ingia kwenye uchochoro mmoja utakaotokezea mtaa mwingine wa nyuma! Huo uchochoro ni maarufu kwa jina la Sabasaba. Ukiumaliza tu, nenda duka la kwanza mkono wa kulia kwako linamilikiwa na dada anayeitwa Sharifa. Hata kama yeye hayupo, vijana wake watakusaidia hata mawazo vipodozi gani uanze navyo kununua!

Nunua kwanza mzigo wa 60% ya mtaji wako, kisha kavipange dukani kwako, with time utaua vipodozi gani hukuchukua (base on demand ya wateja katika eneo lako)! Ukiona umepata mahitaji ya kutosha, nenda kanunue mzigo wa 40% uliobakia!

Kuwa mwangalifu na expiry date hasa isiwe ya mda mfupi ujao, maana usipo uza itakuwa kwako!

Kuhusu vipodozi feki, sina jinsi ya kukushauri, zaidi ya kukuambia kila aina ya kipodozi (mwazni) chukua kiasi kidogo kwanza. Taratibu utavizoea.

Kila la kheri

Biashara yoyote, ianza kutokana na mtaji wako ila kiukweli biashara ya vipodozi unahitajika uwe na mtaji mkubwa kidogo ili uwe japo na kila aina ya kipodozi, lakini pia ni vyema ujue ni aina gani ya kipodozi vinatoka sana!

Pale Kariakoo, wanapo nunua vipodozi vya jumla ili kwenda kuviuza rejareja mtaani, taratibu ukizoea na wakikuzoea utapata na vile vipodozi vilivyopigwa marufuku, ambavyo kikweli ndio vinafaida kubwa ukienda kuuza dukani kwako!

Swala la lesni zake, kwa maduka ya rejareja hilo silijui lipo vipi, nadhani watakuja wanaojua zaidi watakupa majawabu!

Fanya hivi;-
Nenda Kariakoo, kuna eneo linaitwa Sabasaba lipo oppst na fuel station ya bigbon ukivuka ukiuvuka mtaa wa msimbazi (ulizia maduka ya mama mmoja anaitwa Sharifa) yeye ni importer mkubwa sana wa vipodozi nchini!

Usipomkuta yeye, basi vijana wake wapo, waulize chochote watakupa msaaada unaoutakankama ni aina gani ya vipodozi vya kuanza navyo kuvinunua kwa bisahara yako, na ni sh ngapi at least uanze nayo!

Pale Sabasaba, kuna maduka mengi sana, ila nimekuelekeza kwa huyo mdada kwakua yeye au vijana wake hawata take advantage ya ugeni wako wa biashara ili wakuuzie vipodozi ambavyo haviuziki sana au wakulalie bei ila kwa kadiri siku zinaenda utazidi kuyajua maduka mengi, na utafahamiana na watu wengi na mbinu nyingi!

Mwisho, nikutakie kila la kheri kwa biashara yako mpya unayotaka kuianza, ila kuwa mwangalifu na expire date at all time!
VITU UNAVYOHITAJI KUANZISHA BIASHARA HII
Kwa kusema kweli biashara ya vipodozi inalipa vizuri tu ukiielewa vizuri na kucheza vizuri na soko lako na biashara yenyewe kwa ujumla.

1. Nikiasi gani cha mtaji kinahitajika(minimum amount of capital) = Inategemea na msuli wako. Ila minimum uwe na kama Tsh Millioni Saba Hivi (7,000,000/=) Hivi kwa maeneo ya mjini; i.e.
- Kukodi fremu = Tsh 100,000/= kwa mwezi, miezi 6 >> 600,000/=; dalali utajuana naye mwenyewe
- Kusajili TFDA = 150,000/=
- Leseni halmashauri = 80,000/=
- Kodi TRA kama Tsh 150,000/= hivi kwa mwaka, quarter 1 utalipia Tsh 37,500/=
- Kuweka mashelfu ya aluminium na vioo = 1,000,000/=
- Kabati la chini la aluminium na vioo = 400,000/=
- Vipodozi angalau vya kuanzia = 4,000,000/=
- Pesa ya kukaa standby kwa ajili ya kuongezea vipodozi watakavyokosa wateja = 1,000,000/=
- Pia uwe na akiba ya kuendelea kuishi na kuhudumia familia yako bila kudokoa pesa kutoka kwenye duka lako kwa angalau miezi 3 hivi

View attachment 1078393

2.Ni vipodozi vya aina gani vyenye uhitaji mkubwa sana sokoni(consumer needs) = Soko la vipodozi mara zote ni dynamic; leo wateja wako wanatumia Rinju, baada ya miezi 6 watakuwa wanatumia kitu kingine. Pia inategemea sana na eneo utakaloweka duka lako, kuna maeneo wananunua bei na kuna maeneo wananunua brand. Ukitaka kufanikiwa hapa ngoja wakati ukiwa tayari kufungua duka basi fanya survey maduka ya wenzako wamestock nini kisha nenda kwa duka la jumla la eneo lako mwambie unataka ufungue duka la rejareja na ununue vipodozi kwake, muombe akuambie vipodozi vinavyotembea kwa wakati huo na vipodozi gani vya kuwa navyo anyway. Kwa hiyo ukiwa tayari kuingia sokoni ndo utafiti hili

3.Ni vipodozi gani vina faida kubwa sana = Vipodozi vyote vina faida kubwa sana. Faida inatokana na kasi ya kutoka kwa kipodozi husika na tofauti kati ya bei ya kununulia na kuuzia (profit margin). Kwa ushauri wangu ni bora uangalie mahitaji ya wateja wako kuliko faida. Unaweza kuweka vipodozi vyenye faida kubwa halafu vikawa havina movement kwenye location yako - utaangukia pua. Au unaweza kuweka vipodozi vya bei ya chini ambavyo wateja wako hawaviamini na wala hawavitumii.
View attachment 1078397

4.Hasara ambazo unaweza pata = Hili nimekuwa nikiwafundisha sana watu wanaokuja kujifunza kwetu biashara ya vipodozi A-Z. Zipo nyingi, ila karibia zote zinaepukika. Muuzaji kukuibia, adhabu za TFDA, adhabu za TRA, adhabu za halmashauri, vipodozi kuharibika, gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko faida ghafi (gross profit) na kadhalika.
List ya vipodozi vilivyoruhusiwa kuuzwa na vilivyokatazwa kuuzwa zote zinapatikana kwenye tovuti ya TFDA: www. tfda. go. tz (Toa hizo space)

5.Sehemu ya kuweka duka(Matter of location) = Location kama kawaida, wewe tu na ubavu wako; ila ukipata mtaa wenye wakazi wengi au sehemu yenye movement nzuri ya watu - hususan akina dada basi umewin. Iwe ni njia ya kwenda university, mtaa wenye biashara ambazo wateja wake wengi ni wanawake, mtaani wanakokaa hao akina mama, mjini, sokoni nk. Zingatia sheria za TFDA, kuna baadhi ya maeneo hutakiwi kuweka duka la vipodozi (mfano karibu na kituo cha mafuta) hata kama kibiashara ni strategic location (Please kabla ya kulipia fremu kaonane na TFDA, eneo lako lisije kukataliwa wakati umeshalipia)!

6.Sehemu nzuri ambayo naweza fungasha mzigo kwa bei rahisi sana( iwe nje au hata ndani ya nchi hapa mkoa wowote ule) = Kariakoo is the best (ila usipokuwa makini inawezakuwa the worst)! Siku za kwanza nenda na mwenyeji tu hadi utakapomaster, vinginevyo utanunua kwa walionunua na hivyo kupata vipodozi kwa bei mbaya na kuuza kwa bei mbaya - kumbuka akina mama ni very sensitive kwenye suala la bei kwa hiyo ukiuza bei juu hata kwa tofauti ya Tsh 500/= tu basi watapita duka lako na kwenda kununua kwa jirani yako au hata mbali sana; unaweza kuhisi umerogwa, ila 500/= mwenzako anapata vocha!
Ila kitu kimoja - changieni maduka ya jumla ya mikoani kwenu. Kwa hiyo kama haupo Dar es salaam basi usinunue kutoka Kariakoo, tafuta maduka ya jumla hukohuko mkoani kwenu.

I am done & Out!

Ukihitaji kujua zaidi ya hayo basi karibu nitakupa darasa zaidi maana kuna mambo kama 21 hivi ambayo nitakufundisha kwa wiki 1 (Kila siku nitakufundisha mambo matatu makubwa) kuhusu kuanzisha, kusimamia na kuendeleza duka lako la vipodozi (Ila utanipodha soda mbili 😂😂😂 maana ni consultancy eti :):):))

Viva JF!

AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS
0719326693 | 0743422883 | afyazaidi@gmail.com
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA

Ni wazo zuri jaribu sana kuzingatia

i. Bidhaa zinazohitajika kwa sana mahali hapo
ii. Huyo dogo ana uzoefu wa kusimamia biashara?
iii. Je nidhamu ya fedha anayo?
iv. Biashara na ndugu siku zote asilimia za kuendelea ni ndogo sana ivyo uwe unafuatilia kwa karibu sana
v. Pia kuna bidhaa ambazo zinapigwa vita kuuzwa kwenye maduka ya vipodozi jaribu kuzingatia ilo pia
vi. Pia isajili biashara yako (Jina la biashara-BRELA)
vii. Pia mtoa huduma awe na kauli nzuri kwa wateja
viii. Pia jaribu kuwa na mpango kazi hili ukuongoze katika biashara yako

Hayo ni machache tu ya kuzingatia na mengine wadau watakuja nayo
ENEO LA KUPATA MZIGO KWA DAR ES SALAAM
Biashara yoyote, ianza kutokana na mtaji wako ila kiukweli biashara ya vipodozi unahitajika uwe na mtaji mkubwa kidogo ili uwe japo na kila aina ya kipodozi, lakini pia ni vyema ujue ni aina gani ya kipodozi vinatoka sana!

Pale Kariakoo, wanapo nunua vipodozi vya jumla ili kwenda kuviuza rejareja mtaani, taratibu ukizoea na wakikuzoea utapata na vile vipodozi vilivyopigwa marufuku, ambavyo kikweli ndio vinafaida kubwa ukienda kuuza dukani kwako!

Swala la leseni zake, kwa maduka ya rejareja hilo silijui lipo vipi, nadhani watakuja wanaojua zaidi watakupa majawabu!

Fanya hivi;-

Nenda Kariakoo, kuna eneo linaitwa Sabasaba lipo oppst na fuel station ya Bigbon ukivuka ukiuvuka mtaa wa msimbazi (ulizia maduka ya mama mmoja anaitwa Sharifa) yeye ni importer mkubwa sana wa vipodozi nchini!

Na ni Muislam safi mcha Mungu!

Usipomkuta yeye, basi vijana wake wapo, waulize chochote watakupa msaaada unaoutakankama ni aina gani ya vipodozi vya kuanza navyo kuvinunua kwa bisahara yako, na ni sh ngapi at least uanze nayo!

Pale Sabasaba, kuna maduka mengi sana, ila nimekuelekeza kwa huyo mdada kwakua yeye au vijana wake hawata take advantage ya ugeni wako wa biashara ili wakuuzie vipodozi ambavyo haviuziki sana au wakulalie bei ila kwa kadiri siku zinaenda utazidi kuyajua maduka mengi, na utafahamiana na watu wengi na mbinu nyingi!

Mwisho, nikutakie kila la kheri kwa biashara yako mpya unayotaka kuianza, ila kuwa mwangalifu na expire date at all time!
ZINGATIA HAYA

Nakushauri:

1. Vipodozi utavipata kutoka kwenye maduka ya jumla ya vipodozi ambayo yamejaa pale Kariakoo mtaa wa Msimbazi. Kuwa makini sana na vipodozi feki, vilivyopigwa marufuku na visivyosajiliwa

2. Andaa business card, begi la kubebea vipodozi vyako na mifuko ya kuwawekea wateja wako bidhaa utakazowauzia

3. Sana sana lenga kuuza. Utaanza kukopesha mtu akishakuwa mteja wako tayari na ashaanza kukuingizia faida kiasi. Pia utakopesha watu ambao una uhakika nao sio wasumbufu na wale ambao watakuwa referred na wateja wako wengine.

4. Vipodozi vipo vya aina nyingi sana. Lakini ambavyo vitaweza kukutoa haraka kwa hapa Dar ni Perfume, Deodorants na Lotion. Changamoto ni kila mteja kutaka perfume au deodorant au lotion ya aina yake, na tofauti na zile ambazo wewe unazo. Hapa utakuwa unachukua order na kumuahidi kumletea huyo mtu siku inayofuata, na usikose kumpelekea.

5. Jenga network nzuri kwa ajili ya biashara yako. Jichanganye sana na watu na omba watu hao wawajuze watu wengine kuhusu wewe na wakusaidie wewe kuwafikia watu wengine. Chukua namba za wateja wako na wafahamishe ukiwa na mzigo mpya, bidhaa zingine na hata ukiona muda mrefu umepita hawajanunua chochote.

6. Anza na vipodozi vya bei ya wastani (Sh 5,000/= - 20,000/=). Hivyo wateja wake ni wengi zaidi na mzunguko wake ni mkubwa zaidi.

7. Wasome vizuri na kuwa makini na wateja wako. UKICHEKA NA NYANI UTAVUNA MABUA

Mimi nafanya biashara ya uzuri, urembo na vipodozi. Ingawa kwa mtindo mwingine.

Nakutakia kila la kheri!
UNDANI WA BIASHARA YA VIPODOZI TANZANIA

Ndugu msomaji wetu, mfanyabiashara na Mjasiriamali.

Leo tunataka kukujuza juu ya undani wa biashara ya vipodozi hapa Tanzania. Biashara ilioyoenea sana lakini wengi kwa kutokutambua, huifanya bila kufuata utaratibu..na matokeo yake huwa si rafiki hata kidogo kibiashara.

ELIMU hii, kama si wewe, basi inaweza kumsadia ndugu, rafiki au jamaa.

KARIBU SANA.

Kwa Tanzania, na kwingineko duniani, vipodozi hujumuishwa ndani ya kundi kubwa la bidhaa za afya (Healthcare products). Biashara ya vipodozi ni moja kati ya biashara zinazodhibitiwa kisheria (regulated business), na usimamizi wa biashara ya bidhaa hizi kwa Tanzania bara unafanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Biashara hii ya vipodozi pia ni moja kati ya biashara zilizoenea sana hapa nchini; karibu kila mtaa (hasa maeneo ya mijini), hutapita hatua chache bila kukuta duka la vipodozi. Na ni biashara ambayo soko lake ni kubwa na linaendelea kukua siku hadi siku.

Kwa bahati mbaya, maduka haya mengi yamekuwa yanauza vipodozi ambavyo havijasajiliwa na TFDA, ukiachilia mbali maduka yenyewe pia mengi kutokutambuliwa na Mamlaka.

Na kama nilivyogusia hapo juu, biashara hii ni “regulated business” hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za Tanzania, kuuza vipodozi visivyosajiliwa ama kuuza vipodozi bila kibali ni kosa kisheria. Mimi na wewe ni mashaidi kwani mara nyingi tumeona na kusikia maduka mengi ya vipodozi yakifungwa na bidhaa kuharibiwa na Mamlaka husika, sababu mojawapo ikiwa ni kufanyika kwa biashara hii kinyume na taratibu.

Mbali na uvunjaji wa sheria, pia ni muhimu tukajua ya kwamba, uuzaji huu wa VIPODOZI visivyosajiliwa una madhara makubwa sana yakiwemo yale ya kiafya kwa jamii yetu ya watanzania.
Kwa haraka haraka, inaweza kuonekana kwamba kukwepa kufuata utaratibu na kuifanya biashara hii kinyemela haina shida sana, LAKINI shida ipo, tena kubwa sana; mojawapo ni hiyo ya kukamatwa kwa kuvunja sheria na biashara yako inaweza ikawa ndo mwisho wake.

Njia pekee ya kuepukana na haya yote ni kuhakikisha UNARASIMISHA biashara yako.

Sasa basi, pamoja na kupata TIN na lesseni ya biashara, mchakato wa urasimishaji wa biashara ya vipodozi una mambo mengine mawili (02) muhimu ya kufuata.

(1) JAMBO LA KWANZA: Kusajili bidhaa zako, ama kuhakikisha unauza bidhaa zilizosajiliwa na TFDA.
(2) JAMBO LA PILI: Kupata kibali cha biashara kutoka TFDA.

Ukifanikiwa kuyafanya mambo haya mawili, basi utafanya biashara yako raha mustarehe bila bugdha yoyote ile.

Hata hivyo, utafiti wetu mfupi ulionesha kwamba, UGUMU uliopo katika zoezi zima la usajili wa bidhaa hizi za afya pamoja na upatikanaji wa vibali ndiyo umekuwa sababu kuu ya wajasiriamali na wafanyabiashara wengi kushindwa kusajili bidhaa zao na kurasimisha biashara zao pia.

Kufuatia changamato hii, tumeona, kama kampuni ni vyema kufanya juhudi za dhati kutoa elimu, ufafanuzi na msaada wa kitaalamu utakao kusaidia wewe msomaji wetu na mfanyabiashara katika zoezi zima la usajili wa biashara yako na bidhaa zako.

Makala hii ni ndefu sana, hatuwezi kuiweka yote hapa, hata hivyo usijali ndugu msomaji wetu tunanjia mbili za wewe kuweza kuipata kwa urefu wake;

(1) Ya kwanza, fuata hii link inakupeleka moja kwa moja.. http://pharmaregtz.com/sites/default/files/Mambo Makuu 2 lazima kuyajua..pdf

(2) Ya pili-- Comment email address yako au tutumie kwenye sms au email yetu ya support@pharmaregtz.com nasi tutakutumia makala yote ndani ya muda mfupi. Pia, tukipata email yako tutakuunganisha moja kwa moja na mtandao wetu wa email na hivyo utakuwa unapata taarifa mbalimbali zitakazo kusaidia wewe, au jamaa yako katika biashara hii ya VIPODOZI na bidhaa nyingine za afya (kama vile dawa, vifaa tiba na vyakula).
ANZA NA BIDHAA HIZI

Hongera, ukianza na 1milioni si vibaya hata chini ya hapo kinachotakiwa fungua mlango ili ujue watu wanahitaji nini. Anza na pafyumu, lotions, brazilian hairs, shapoo.

Njia rahisi ya kujua mahitaji ni kufikiria kama kuna saloon za kike jirani zingehitaji vitu gani vya haraka haraka. Pia fikiria hasa akina dada ili wapendeze wanapendelea watoke vipi, e.g mikoba, viatu, bangili, hereni, mikufu-hivi utakuwa unaviongeza dukan kwako siku zijazo kadri ya uhitaji sio mwanzoni kwani ni gharama kubwa kiasi.

Kwa hapo Dar maduka ya jumla ya vipodozi nenda Kariakoo ukifika kituo cha mafuta cha Big bon vuka barabara upande wa pili kuna gorofa linatazamana na hicho kituo, usifike msimbazi polisi station (sijashika jina la mtaa) nyuma ya hilo ghorofa kuna kabaraba kana maduka kibao. Zamani kidogo ilikuwa ni stand ya kushushia abiria wanaotokea mwenye na ubungo-sijaja Dar muda.

NB: Unaponunua au kuuza vipodozi:
  • Hakiki expire date
  • Uwe na vibali au jitahidi ukamilishe mchakato miezi michache ijayo kibali toka TFDA. Hii isikuzuie kufungua sasa lakini
  • Ujikite kujua vipodozi ambavyo nchini vimepigwa marufuku tusije tukakukosa JF kisa vipodozi haramu mfano Carolite, epiderm. Wengine wataongezea.
All the best
 
Fanya biashara ya vipodozi vya bei nafuu. Ukitarget akina mama wa nyumbani, wanafunzi wa vyuoni uta win. Sehemu yako ya soko iwe ni ya mkusanyiko wa watu wengi kama stendi ya basi, sokoni n.k
 
Habari zenu wadau. Nafikiria kuanzisha biashara ya kuuza vipodozi sehemu ya Sinza Madukani. Lakini sina uzoefu na biashara hii.Nina mtaji wa shilingi milioni tano. Bahati nzuri fremu sio ya kupangisha, nimepewa na father. Naomba mnichangie mawazo Je inalipa kweli? Changamoto zake zipi? Au kama kuna wazo zuri zaidi ya biashara hii tujuzane wadau.Naombeni mawazo yenu wadau.
 
Biashara hiyo siyo mbaya inategemea na location na aina ya vipodozi unavyotaka kuuza coz kuna mapambo ya kike kuna mafuta na lotion na kuna pafryum na urembo mwengine so unataka kuweka kipi ama vyote.
 
Baada ya kukaa na kufikiria kwa muda mrefu na kupata maoni mbalimbali hasa kutoka humu JF sasa nahisi ni wakati wa kuweka wazo langu hapa mnipe ushauri. Nafikiria kufanya biashara ya kuuza vipodozi kwa jumla na rejareja. Sehemu ninayofikiria kufungua ni Mbeya. Sasa nahitaji kusaidiwa ktk mambo ya fuatayo:

1. Utaratibu wa kuprocess kibali unaanzia wapi.
2. Sehemu (miji) za kuchukulia mzigo kwa kuzingatia unafuu wa kuchukulia na kusafirisha.
3. At least mtaji kwa kuanzia (kwa sasa nina 10M)
4. Napenda pia kujua rate ya profit
5. Nahitaji kujua risks ninazotarajia ku-encounter mbele ya safari.

Naomba kuwasilisha.
 
Mimi nakushauri tafuta fedha ya maana ya kufungulia biashara, 10m inaweza kuwa nyingi lakini si kwa magnitude hiyo, badala ya kutaka kuagizishia nunua wanaponunua wenzio slowly mtaji utakua na tayari itakuwa ushapata na akili yako mwenyewe.
 
Mimi nakushauri tafuta fedha ya maana ya kufungulia biashara, 10m inaweza kuwa nyingi lakini si kwa magnitude hiyo, badala ya kutaka kuagizishia nunua wanaponunua wenzio slowly mtaji utakua na tayari itakuwa ushapata na akili yako mwenyewe.

Thanks bro.
 
Vipodozi pia ukikamatwa na customs siku moja tu, unafilisika.

Mkuu kwa kuanzia nilikusudia kuchukulia hapa hapa nchini na nilidhani natakiwa kupata kibali cha kufanya biashara hiyo,so mambo ya customs sikuyaconsider sana.Mimi pia nafikiri biashara ya vipodozi haina tofauti sana na biashara ya dawa za binadamu.
 
Wakuu za wikiendi,

Poleni mfungo wale ndugu waislam na pia wale wenzetu wa upande pili najua mnaburudika jumapili hii. Nipo maeneo ya Dar es Salaam nilikuwa naomba kujua location gani ipo vizuri kwa ajili ya kufungua duka la vipodozi nina mtaji wangu wa millioni tatu nahitaji kujua wakuu manake kuajiriwa ni utumwa.
 
Mjasiriamali usikwepe ushindani, maeneo ntayokushauri ni buguruni, tandika, mwananyamala, na mtongani na mbagala mwisho,
 
Ujasiliamali ndiyo maisha ya leo, ukizingatia kuwa ajira ni janga kwa Tanzania na Dunia kwa ujumla. Nisiwachoshe sana kwa maneno mengi mnayoyajua.

Nina pesa kiasi cha Tshs milion 5 (Tshs. 5,000,000/-). Ambayo ninafikiria kuitumia kuanzisha biashara ya "VIPODOZI" DODOMA MJINI, ili wife apate pakutokea badala ya kukaa nyumbani tu. Hapa lengo ni kuchanga nguvu ili tujikwamue kwa namna moja ama nyingine.

Ninaomba ushauri wenu wadau kwa mambo yafuatayo:-

1. Je, kiasi hiki cha pesa kinafaa kwa kuanzia?

2. Na kama 1 ni ndiyo, je, vitu gani vya mhimu kuvifanya ktk kuanzisha hiyo biashara? (namaanisha kama kuna documents za mhimu ninazopaswa kuwa nazo kama watu wa afya i.e maduka ya dawa)

3. Kama 1 ni ndiyo, ni wapi naweza nunua mzigo(bidhaa) nami nikapata chochote kama lengo lilivyo?

NB: Ushauri wako ni mhimu sana, pia kama hicho kiasi kitakuwa hakitoshi nishauri ni kiasi gani niongeze/nitafute ili kufikia lengo.

NAWASILISHA.
 
Habari wana JF napenda kuuliza na kupata ushauri toka kwenu kuhusu soko la vipodozi nataka kuchukua toka Tunduma nilete Dar kuuza kwa jumla kwa maduka nitakayochukua oda. Je, naweza pata mchanganuo wa hii biashara maana ndio nataka nijalibu na mtaji wangu wa kuunga unga. Natanguliza shukrani na mawazo yenu.
 
Habari wana jf napenda kuuliza na kupata ushauri toka kwenu kuhusu soko la vipodozi nataka kuchukua toka Tunduma nilete Dar kuuza kwa jumla kwa maduka nitakayochukua oda. Je naweza pata mchanganuo wa hii biashara maana ndio nataka nijalibu na mtaji wangu wa kuunga unga. Natanguliza shukrani na mawazo yenu

Mkuu hii biashara inatakiwa ujue aina ya vipodozi.vile vinavyolipa ni vile ambavyo serikali imepiga marufuku. Vingine ambavyo vinaruhusiwa havilipi ila ukivileta vile vinavyolipa biashara yake ni kama kuuza unga vile.kuanzia kuvisafirisha toka huko mpaka dar.wenye mabasi ndiyo, wanaoongoza kuchomea kwa police halafu wanapatagao. Kiufupi tafuta biashara nyingine mkuu. Maana unaweza kata mtaji wako trip ya kwanza tu.
 
Hiyo biashara inalipa sana cha muhimu ujue vipodozi vilivyoruhusiwa ili usishikwe na kuchomewa. Cha kwanza zunguka maduka ya vipodozi uhulize vip vinavyouzika. zunguka kwa zahidi ya maduka 40 ili ujue.

Kuna mdada namjua ila yeye alikuwa anatoa Congo ya mashariki akipitia Uganda, kisha anapanda bus za Dar kupitia Bukoba, sasa hiv ni tajiri mkubwa.

Fanya nilivyokwambia utafanikiwa.
 
Mimi nina saloon ya kike niko Kilimanjaro vipi unaweza kufanya bussnes na mm, saloon kwangu nauza urembo na vipondozi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom