Nina mpango wa kumfungulia kesi aliyekuwa kaka mkuu shule ya msingi kipindi nasoma shule

sontable

JF-Expert Member
Apr 13, 2018
228
500
Corona ipo tuchukue tahadhari!

Nimekaa nimefikiria nimeona huu ni muda muafaka wa kumfungulia mashtaka ya unyanyasaji aliyekuwa kaka mkuu shule ya msingi kipindi nasoma ,back 14yrs nipo darasa la 5 Kuna kiongozi aliyekuwa ni kiranja wa shule alikuwa akininyanyasa Sana mbali na vipigo lakini alikuwaakiniambia niende nikapige simu chooni (kwa wale ambao hawajui kupiga simu chooni ni Nini yaani unapigwa viboko kwanza then unapelekwa chooni ukainamie tundu la choo huku mashavu yakigusa Yale mabanzi ya pale kweye tundu huku uso wote ukiwa umefiti kwenye lile tundu ukiangalia kinyesi ndani Kisha unaanza kusema baba Mimi nateseka huku njoo uniokoe na maneno mengine mengi atakayokuongoza useme) Sasa kupitia unyanyasaji huu Nina mpango wa kwenda kufungua kesi

Sasa nilikuwa naomba msaada kwa wanasheria nianzie wapi na je itawezekana na Sina ushahidi wa picha au video Ila karibia wenzangu wote tuliosoma nao kipindi kile wanajua kuwa hio Hali ilikuwa inafanyika pale shule

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Willard Jonnes

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
346
1,000
Mimi mwenyewe nina mwalimu wangu huyo wakati niko form 3 alininyanyasa sana kwa sababu form 1 na form 2 sikuwa mkondo A ivo kufika form 3 tukapangwa kwa ufaulu na nikaingia Form 3 A yule mwalimu wakati tupo form one Na two tulikuwa Mkondo C ivo alikuwa ana tu ignore kwamba huko C hakuna kitu na watoto wake ni wa A wakati hatukupangwa based on perfomance sasa ile kukutana nae mkondo A form 3 tulikuwa kama watu tisa ivi wa kutoka C alitunyanyasa wale top ambao tulikuwa kama hatupo nae pamoja wakati anakuja mkondo C, alifanya hio humiliation publicly kabisa na iliniathiri sana niliampa nitamtafuta tu hata ipite miaka mingapi labda nimkute ni marehemu, Pain niliyo feel lazima nae aexperince miaka mingi imepita ila plan yangu iko pale pale its matter of time na lazima nifanye execution, Nimesamehe mengi ila hilo nimeshindwa kabisa
 
Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
230
250
Hayo mateso ulopata hayana ushahidi, hivyo, ni vigumu kutoa ushahidi labada kama kuna wanafunzi wenzio watakokuwa tayari kueleza mlivyokuwa mnateswa na huyo Kiranja mkiwa Shuleni.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
4,750
2,000
Ilaumu jamii yako tu kwa kushindwa kukulinda dhidi ya bullying ila huyo bull huwezi kumfanya kitu kisheria kwa sasa.
 
King snr

JF-Expert Member
May 25, 2015
1,105
2,000
Too late ilibidi wakati unafanyiwa huo unyama usifiche ulipaswa kutoa taarifa hata kwa walimu wako ila kwa sasa ukimshtaki ushahidi utapata wapi.?
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
4,417
2,000
Corona ipo tuchukue tahadhari!

Nimekaa nimefikiria nimeona huu ni muda muafaka wa kumfungulia mashtaka ya unyanyasaji aliyekuwa kaka mkuu shule ya msingi kipindi nasoma ,back 14yrs nipo darasa la 5 Kuna kiongozi aliyekuwa ni kiranja wa shule alikuwa akininyanyasa Sana mbali na vipigo lakini alikuwaakiniambia niende nikapige simu chooni (kwa wale ambao hawajui kupiga simu chooni ni Nini yaani unapigwa viboko kwanza then unapelekwa chooni ukainamie tundu la choo huku mashavu yakigusa Yale mabanzi ya pale kweye tundu huku uso wote ukiwa umefiti kwenye lile tundu ukiangalia kinyesi ndani Kisha unaanza kusema baba Mimi nateseka huku njoo uniokoe na maneno mengine mengi atakayokuongoza useme) Sasa kupitia unyanyasaji huu Nina mpango wa kwenda kufungua kesi

Sasa nilikuwa naomba msaada kwa wanasheria nianzie wapi na je itawezekana na Sina ushahidi wa picha au video Ila karibia wenzangu wote tuliosoma nao kipindi kile wanajua kuwa hio Hali ilikuwa inafanyika pale shule

Ahsante

Sent using Jamii Forums mobile app
Ohh 😲 Inasikitisha mno. Naunga mkono pia usiache kumfungulia mwalimu mkuu kajalada kake manake naye anahusika na ufedhuli huu.
 
jaywacnza

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
899
1,000
Aisee pole sanaaa, mimi mwenzako nilikua nakataa kufanyishwa adhabu za kishenzi

1) Nkiwa darasa la nne walimu walikuja kutuchapa mande kisa hatujalipa mchango, ilipofika zamu yangu nlikataa nkasema sio kosa langu, mama yangu hana pesa, wakataka kunibananisha nkachomoka mlangoni.

2) Nkiwa darasa la tano nlishawahi kukataa kuchapwa na waya wa umeme( darasa zima walichapwa) nakumbuka darasa zima walipewa amri wanivute kunitoa kwenye dawati cha moto walikiona

3) Darasa la saba, nlichelewa kipindi asubuh, tuliochelewa wote tukaambiwa tuchapane fimbo nlikataa, nkasema siwezi kichapwa fimbo na mwanafunzi mwenzangu.
Namatukio mengi tu mpaka namaliza form four
Nlikuwa mkorofi sana, hao viranja siwacheleweshi kuwazibua....naokota taka kwa hiari yangu, nafagia kwa hiari yangu....

Asante sana mama, uliniokoa kwenye masoo yangu yote mpaka sasa nna familia yangu safiii.

Ila noma mazee mtoto wangu wa kwanza dalili zote naziona kama mimi vile, dah sijui nifanyeje??

Respect!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom