Nina mpango wa kuhamia Morogoro kwa nia ya kutafuta maisha

Wakuu heshima zenu!!!

Bila kupoteza wakat niende kwenye point ya muhimu ilionifanya kufungua hii mada,, mm ni kijana mwenye miaka 20 na kwasasa nipo mwanga kilimanjaro,,,,, mpango wangu hasa ni kuhamia morogoro kwa nia ya kusaka life wazee na kiukweli huku mwanga hamna cha maana kabsa!!!

Acc ya bank inasoma 2.5mil tu na hio ndio nmepanga nikaanze nayo maisha hata kama nikipanga chumba bila godoro n fresh tu nitalala hata chini ila hio pesa nataka iende shambani.

Morogoro sina ndugu ila nmeichagua kwa sababu zifuatazo
1.ni mkoa wenye fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo
2.living cost NIMESIKIA kwamba iko chini
3.usalama ni mzuri

NB: Naombeni ushauri wenu ndugu zangu na pia ikitokea nikapata mwenyeji wa huko ntashkuru sana na MUNGU AWABARIKI.
Sawa KAMBI POPOTE!
 
Ana utajiri wa karibu gram 26 aanze mdogo mdogo: naamini kila akipileka dar atakuwa hakosi walau 150k. Kwa mwezi akienda round 4
atakosa kweli total ya laki 6. Take home ya mtu wa mshahara wa laki 9 serikalini.

Uko kwako panamfaa sana atakuza mtaji haraka akiwa makini; ndondo si chururu.
Ww ndio nilikua nakuxubiri nilipita uzi fln iv nkaxoma kwamba upo mbaral unapiga hzi mixhe,,, embu nipe mwanga
 
Mwanga!!! Kimbia Apo Mara moja niliwai kwenda hapo kikazi aisee sijui watu wanapaweza vipi Apo mji umetapanya office za Mana na huduma za bank ziko mbali hii ilikua mwaka2010 afu maji Apo Ni changamoto
 
Ni wilaya nzuri kwa kilimo cha mpunga na pia wenyeji wa wilaya hiyo ni wakarimu sana kwa wageni. Kila la heri. Nimeishi huko miaka mingi. Kuanzia Mkamba, Kidatu, Sanje, Mkula, Sonjo, Mang'ula, Kiberege, Ifakara, Mbingu, Mngeta, Chita, hadi Mlimba; Kote huko kunafaa kwa bishara, kilimo na fursa nyinginezo nyingi.

Pia unapoingia msimu wa mavuno kuanzia mwezi wa 6 hadi wa 12, huwa kunanoga sana huko mahali. Full sherehe, full kujiachia, nk.
Haaaaa mkuu mbona umetaja mitaa yangu hiyo mbingu, Chita,mlimba na hapo home sweetie mngeta!! Braza ingia wilaya ya KILOMBERO fanya utafiti km unataka kulima au kununua mazao maana risk zinatofautiana
 
Mi namchagulia malinyi kwa mtaji wake utamtosha
Kwa nini usiwekeze huko huko Mwanga Kilimanjaro ambako kimsingi mazingira yake umeshayazoea?

Morogoro ni moja ya mikoa mikubwa nchini mwetu, hivyo ungekua pia specific, unataka ukaishi wilaya gani? Moro mjini, vijijini, Kilombero, Mvomero, Turiani, Kilosa, Ulanga, Malinyi, nk.
 
Haaaaa mkuu mbona umetaja mitaa yangu hiyo mbingu, Chita,mlimba na hapo home sweetie mngeta!! Braza ingia wilaya ya KILOMBERO fanya utafiti km unataka kulima au kununua mazao maana risk zinatofautiana

Niliishi wilaya zote mbili (Kilombero na Ulanga+Malinyi miaka hiyo) Huko mahali huwa nakukubali sana kutokana na ukweli kwamba ni kuzuri kwa kuishi.

Mngeta yote kuanzia Mkusi, Lukolongo, Mchombe, Kotako mpaka Mkangawalo; kote huko nilishatembelea miaka ya mwishoni mwa 90!

Treni ya TAZARA ndiyo kabisaaa, nimeipanda sana kuanzia Dar mpaka Iyunga. Siyo Ordinary, Kipisi, Express, nk. maana ndiyo mkombozi wa wakazi wengi wa wilaya ya Kilombero.
 
Wakuu nia yangu hasa n kwenda kupiga ishu ya kununua mpunga then nakoboa na kuuza mchele ila kwasababu sina uzoefu na hio biashara nitaenda kulima heka 1 huku nikisoma hio biz ya mpunga 2 mchele inaendaje ili niweze kuanza,,,
Anza na kununua mchele kisha peleka kwenye masoko kama dar,dom na kwingineko au nunua mpunga na baadae kuuza

kama ni kilimo cha hiyo ekari moja hakikisha ni cha umwagiliaji
 
Sema hata kukusanya mchele siku hiz haupandi km zaman..hukuti sasa hv mchele wa 2300 sokoni..unajikuta unahangaikia sh 200@! unajua hata km una 5m kama huna akili ya kujiongeza unaweza jikuta inaishia tu...shida inakuja hapo...!
Suala la mipaka kufungwa ni ishu sana aisee vyakula vimekua vigumu sana kupanda bei.
 
Back
Top Bottom