Nina mpango wa kuhamia Morogoro kwa nia ya kutafuta maisha

4rever young

Senior Member
Jul 26, 2019
136
125
Wakuu heshima zenu!

Bila kupoteza wakati niende kwenye point ya muhimu ilionifanya kufungua hii mada, mimi ni kijana mwenye miaka 20 na kwasasa nipo Mwanga Kilimanjaro, mpango wangu hasa ni kuhamia Morogoro kwa nia ya kusaka life wazee, na kiukweli huku Mwanga hamna cha maana kabsa!

Account ya bank inasoma 2.5mil tu na hio ndio nimepanga nikaanze nayo maisha hata kama nikipanga chumba bila godoro ni fresh tuu nitalala hata chini ila hio pesa nataka iende shambani.

Morogoro sina ndugu ila nmeichagua kwa sababu zifuatazo
1.Ni mkoa wenye fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo
2.Living cost nimesikia kwamba iko chini
3.Usalama ni mzuri

NB: Naombeni ushauri wenu ndugu zangu na pia ikitokea nikapata mwenyeji wa huko nitashkuru sana na Mungu awabariki
 
Nashkuru kwa ushauri,, mara zote cpend kukaa na kiasi kikubwa cha fedha,, naziwekaga bank
 
Morogoro pako vizuri kibiashara lakini hio 2.5milion kwa kuanza kila kitu ni ndogo tafuta mradi mwingine utakapofika na ili kujipanga kwaajili ya hicho kilimo na kufanya utafiti halisia washuhuli yako
 
Kwa nini usiwekeze huko huko Mwanga Kilimanjaro ambako kimsingi mazingira yake umeshayazoea?

Morogoro ni moja ya mikoa mikubwa nchini mwetu, hivyo ungekua pia specific, unataka ukaishi wilaya gani? Moro mjini, vijijini, Kilombero, Mvomero, Turiani, Kilosa, Ulanga, Malinyi, nk.
 
Nataka nije kilombero ndugu

Ni wilaya nzuri kwa kilimo cha mpunga na pia wenyeji wa wilaya hiyo ni wakarimu sana kwa wageni. Kila la heri. Nimeishi huko miaka mingi. Kuanzia Mkamba, Kidatu, Sanje, Mkula, Sonjo, Mang'ula, Kiberege, Ifakara, Mbingu, Mngeta, Chita, hadi Mlimba; Kote huko kunafaa kwa bishara, kilimo na fursa nyinginezo nyingi.

Pia unapoingia msimu wa mavuno kuanzia mwezi wa 6 hadi wa 12, huwa kunanoga sana huko mahali. Full sherehe, full kujiachia, nk.
 
Nashkuru sana kwa kunipa moyo,,, sehemu hasa ni mngeta,,,
 
Najua hilo ila nia ya kufanya hzo kaz ni kwa ajili ya kusurvive katika hzo siku za hasara ili kujipanga upya katika mapambano,,, na ninachoamini zaidi kwenye maisha ni hutakiwi kukata tamaa
Haha mzee hii njia nilikuwa natumia chuo Boom lote nimelipeka kufanya biashara alafu majanga sipokei hata faida hata 1000/= kwasiku mzee usiombe ikutokee nilifanya idalali mpaka vibaya ili nipate pesa yaku survival kwa miezi minne 4 yaani nikiamka na 3000/= nyingi.
 
Back
Top Bottom