Nina mpango wa kuhamia Morogoro kwa nia ya kutafuta maisha

wasikujaze woga mm nilipotoka shule miaka ya 2000 mwanzoni,nilizamia huko mlimba Nina 20000 tu mfukoni.nilikomaa kule nalima huku nawinda nyama pori kwa mwaka 6 nikawa mwenyeji nikajenga na kakibanda nikatoka shavu.mpaka Leo Nina nyumba kule na ardhi.usiogope
Mkuu ulikuwa unawinda nyati,sheshe,njapuli, au boko? Mlimba upo mitaa gani hapo mjini,kamwene au matangini?
 
Morogoro ni kubwa jipe muda wa kufanya research unataka kulima nini na morogoro sehemu gani inafaa kwa kilimo unachotaka binafsi nipo morogoro ila eneo nililopo kilimo sio kihivyo ila hapa ufugaji nikama wote.... Fanya utafiti morogoro kubwa mno kuna sehemu nauli ni zaidi ya 20k kutokea morogoro mjini...
Mkuu nauli inafika Hadi elfu 50 ndani ya Moro tu,.
 
We kweli kilombero uliitembea, kuanzia ifakara adi mlimba pako vizur kwa kilimo ndo maaneo yangu ya kutafuta tonge
Haaaaaa mkuu, unapita maeneo mazuri hivyo.....Ifakara,lumemo, namawala, luipa, idete, kisegese, mbingu,mofu,njage,mngeta,Ikule,Chita,chisano,mlimba,tanganyika masagatiii......
 
Hujakosea, Karibu Mji kasoro bahari. Kutokana na standard zako ulizo orodhesha ziko makini. Maeneo ambayo utaweza kupanga kwa unafuu mzuri na ukaribu wa mjini ni Mkundi, Kihonda na Nane Nane. Kuhusu maswala ya kilimo ni kweli haswaa tena unaweza kuaanza kujifunza biashara ya kuuza mazao ya vyakula kwa jumla kama maharage, mchele, dagaa, vitunguu n.k. Ni vyema ukiaanza biashara rasmi utege ofisi yako maeneo ya mjini "centre" au karibu na soko kuu.
mkuu vipi soko la biashara ya mazao morogoro mjini ni la uhakika
 
Wakuu heshima zenu!

Bila kupoteza wakati niende kwenye point ya muhimu ilionifanya kufungua hii mada, mimi ni kijana mwenye miaka 20 na kwasasa nipo Mwanga Kilimanjaro, mpango wangu hasa ni kuhamia Morogoro kwa nia ya kusaka life wazee, na kiukweli huku Mwanga hamna cha maana kabsa!

Account ya bank inasoma 2.5mil tu na hio ndio nimepanga nikaanze nayo maisha hata kama nikipanga chumba bila godoro ni fresh tuu nitalala hata chini ila hio pesa nataka iende shambani.

Morogoro sina ndugu ila nmeichagua kwa sababu zifuatazo
1.Ni mkoa wenye fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo
2.Living cost nimesikia kwamba iko chini
3.Usalama ni mzuri

NB: Naombeni ushauri wenu ndugu zangu na pia ikitokea nikapata mwenyeji wa huko nitashkuru sana na Mungu awabariki

Kwa kweli cost of living ipo chini Sana! Ila pia Hakuna hela; kuna mazao, Kama wayauza kwingine Kwa kweli utafanikiwa.

Tukuku tea kienyeji bei Rahisi Sana !
 
Mzee baba kama unataka kuanza maisha Moro usiende town, hakuna mzunguko wa pesa hakuna kazi za kuajiriwa nakushauri uende vijijini huko kama dumila, mgeta matombo, mvomero, kisaki na mkuyuni na ukifika huko fanya biashara ya kununua mazao usilime utafeli mjomba, ama fungua hata banda la kunesha mpira..kilimo kwa mtaji ulionao ni oesa ndogo, moro kutafta pesa kwa njia za halali ni mtihani mzee baba nimekaa hapo si chini ya miaka sita napafaham vizur na maraia wa hapo hawapendi watu watoboe, kama wewe ni mtu wa kaskazini tafta watu waliotokea pande hizo watakupa mwanga kwa maana wanaushirikiano sana na hawawezi kukupoteza lakini wenyeji si watu poa kwa kukushauri wengi wanapenda kuona unaanguka ama unakuwa kama wao.
Duh kumbe watu wa moro town roho zao zimejikunja
 
Account ya bank inasoma 2.5mil tu na hio ndio nimepanga nikaanze nayo maisha hata kama nikipanga chumba bila godoro ni fresh tuu nitalala hata chini ila hio pesa nataka iende shambani.
Hivi ndo mnajazana huko ATM kumbe acc ina 2.5m 😂 hivi milion mbili Ni hela ya kuweka bank
 
Wakuu heshima zenu!

Bila kupoteza wakati niende kwenye point ya muhimu ilionifanya kufungua hii mada, mimi ni kijana mwenye miaka 20 na kwasasa nipo Mwanga Kilimanjaro, mpango wangu hasa ni kuhamia Morogoro kwa nia ya kusaka life wazee, na kiukweli huku Mwanga hamna cha maana kabsa!

Account ya bank inasoma 2.5mil tu na hio ndio nimepanga nikaanze nayo maisha hata kama nikipanga chumba bila godoro ni fresh tuu nitalala hata chini ila hio pesa nataka iende shambani.

Morogoro sina ndugu ila nmeichagua kwa sababu zifuatazo
1.Ni mkoa wenye fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo
2.Living cost nimesikia kwamba iko chini
3.Usalama ni mzuri

NB: Naombeni ushauri wenu ndugu zangu na pia ikitokea nikapata mwenyeji wa huko nitashkuru sana na Mungu awabariki
kwa hiyo hela unaenda kulima au kubet?
 
Back
Top Bottom