Nina Milioni 7, natafuta gari ya kupigia Misele

Kama mada inavyojieleza hapo juu.. ninakaribia 40yrs nmetembea kwa miguu about 30s sasa nisije nikatembea 40yrs kama wana wa Israel.

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
Kwenye haya mambo ya magari kuna watu wanapigwa sana yaani wanauziwa gari mbovu iliyopigwa rangi. Kama utanunua kwa mtu zingatia haya
1. Tafuta fundi gari ukajaribu naye hilo gari.
2. Hilo gari lina document zote zinazotakiwa? Usikubali kuuziana uchochoroni.

Mfano hai.
Jirani yetu alinunua Corona, ukiona nje kana rangi nzuri unaweza fikiri mpya. Ndani ya miaka 2 akaweka juu ya mawe mpk leo tangu 2004. Mwingine alinunua gari, ndani ya mwaka 1 akaweka juu ya mawe mpk leo.
 
Hao hawakufikia uwezo wa kumiliki usafiri.
 
Back
Top Bottom