Nina milioni 45, nifanye biashara ipi kati ya hizi?

Vipi mkonge maeneo ya mkuranga waweza stawi
mkuranga una stawi kwa maeneo ambayo ni makame zaid mana huwa haupnd maji meng (ni zao la ukame), lkn hapa utapata shida kidogo mana dar na pwani mashine za ku produce mkonge hazipo, na wafanyakaz utawatoa wapi wa kukuvunia jibu ni hapana....

Unatakiw kulima maeneo ambay yapo karb na shamba la mkonge ili waje kukuvunia na wakfnyie kila ktu.ww kaz yko ni kusoma account na kuagiza wa2 wakufyekee majani shambani tu....kama upo ofisini, burdaaaan unaznguka na kiti tu, huku account balance ikiwa high...huna presha..hutotaman kfny biashara mana utaona inakupa stress tu (sijasema biashara ni mbaya nieleweke)....mana huk hakuna mambo cjui nitafilisika cjui kuibiwa cjui kupata hasara..hiyo sahau.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalamu,kwa kuuza daladala zangu mbili sababu ya usumbufu wa kissing garage,plus mkopo nawezapata kama m45 nipo na mawazo kama matano hivi,ushauri muhimu ili nisiangamie maana pesa ikishapotea hairudi unabaki na majuto na maradhi ya moyo tu.

1. Nitafute eneo nijenge frem za kupangisha hapa takula hadi uzeeni shida utapata kodi itakayokusaidia kula na sio kukua haraka kibiashara lkn ni ya uhakika yaani ufi njaa.Mungu akijalia wawezazifungulia biashara zako kadri utakavyo na maisha yakaenda.

2. Ninunue trekta mpya zero kilometer katu sitonunua chombo cha moto used nchini tena kwa hasara nilizopata za kushinda garage kuliko kushinda barabarani.Trekta ni tegemeo ni johndeer,Massey,case,deutz ukitanguliza 45 anakupa inayobaki na riba ndani ya mwaka kwa mnyama deer miaka miwili yaani,zinauzwa kati ya 55m hadi 65m plus jembe.Niingie pori nikachane mbuga nalimia watu nami nalima yangu mazao tegemeo ni karanga,alizeti,mtama,mhogo,viazi,mahindi,mpunga nategemea kulima ekari 500 kwenda juu mashine Yangu nguvu yangu nasimamia mwenyewe iwe jua au mvua ni kula mbuga tu.

3. Nimpe muhindi 45m anipe tata marcopolo ya mkopo zero kilometa nikae mlangoni nipige ndefu sio daladala yaani ruti za nje ya mji nauli isiyo chini ya elf 15 yaani kupakia kwa foleni mfano moro ifakara,mbagala kusini,kambi popote.

4. Niagize fuso mnyama au scania kipisi nikae mwenyewe naenda shamba kununua mizigo mixer mfano viazi chips,ndizi,miwa,nyanya,vitunguu,ngombe,mbuzi,nk chochote kiuzwacho sokoni nakujauza bei ya jumla narudi shamba tena kwa kusomba mizigo ya duka kurudi shamba.

5. Nifungue kiwanda cha kusaga chupa na mifuko ya plastic kisha nauza viwandani.

6. Ninunue shamba nipande miti niendelee na umasikini wangu nisubirie miaka 10 hadi 15 niwe milionea baada ya kuvuna miti.

Naombeni idea kwa kuangalia risk,faida,mda,usalama wa fedha,uhakika wa kuishi, stress,nk
Usinunue mpunga kama sio mzoefu maana utauziwa mpunga ulivunwa kwenye maji na mchele wake uwe biliani , nakushauli nunua trekta iliotumika toka nje Massey 165 hii NI ndogo sana lkn unauwezo wa kulima Shamba lako ekari 100 kwa mwaka na ukawalimia na majirani zako, biashara ya kilimo ukiwa na trekta anza na mashamba yako kwanza, hiyo Massey 165 unaweza pata kwa 21 milioni tafuta ile ya muingeleza , pesa inayobaki unaanzia kilimo na nakushauli ukitaka kulima anza na ekali chache kama 10 ili uwangalie changamoto za kilimo na mengeneyo ,sasa hapo ndio unaweza kulima mpunga baada ya kununua , au fungua duka la jumla la bidhaa mabali mbali , kama mafuta ya kula, sukari , nk, ukishindwa kabisaaa tengeneza chakula cha kuku au saga sembe uwe na mashine yako, hapa unaweza kuja mp nikakupa muongozo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom