Nina milioni 22, nahitaji wazo zuri la biashara kwa mkoa wa Arusha

Niko na business plan ambayo ndio niko nayo na nimeshanunua baadhi ya mitambo bado inaitajika kiasi flani kukalilisha baadhi ya machine nyingine kama uko tayari joint venture 60/40 tunauhakika wa 100, 000Tsh kwa kila siku kiwango cha chini, tunaweza tengeneza mpaka 500,000Tsh kwa siku provided good marketing and plans

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Habari wanajukwaa.

Ee Bwana ee, nimekuja kwenu wana jukwaa, kuomba tusaidiane mawazo kama kichwa cha habari kinavyosomeka.

Baada ya kumaliza chuo 2019, Mungu alinifungulia mlango nikapata kazi ya miaka miwili na NGO x hapa Nchini, kutokana na msoto uliopo kitaa niliona ni vyema nijibane niweze kusave pesa walau nifanye kitu kitakacho nisaidia. Mkataba wangu umefika tamati na namshukuru Mungu nimeweza kusave takribani milion 22.

Nilikuwa na mawazo mawili, la kwanza ni kujenga nyumba kwa kuwa nilishanunua kiwanja.

La pili, ni kufanya biashara, ila kwa bahati mbaya bado sijawa na wazo zuri la biashara.

Naombeni mawazo yenu, nijenge au nifanye biashara, kama ni biashara Je, unahisi biashara gani nzuri katika mkoa wa Arusha?

========
Baadhi ya mawazo ya wadau

Pia soma:
Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo
Nashukuru kwa mawazo yako kiongozi
 
Nakushauri vet mechi za champions league wiki ijayo.
- jumanne na jumatano kutakuwa na champions league , mpe man City, mpe Bayern, alafu weka over 1.5 kwenye mechi ya Madrid vs liver.
Hapo hukosi odds ya 2.5 ambapo ukiweka mil 22 inakuja mil 45.
Fanya hivyo and thank me later
 
Chukua milioni 18 weka fixed account mwaka mmoja. Baki na milioni 4 ambazo ndio utafanyia pilot.

Ingia chimbo tafuta elimu, maarifa, taarifa sahihi na kila kitu kuhusu biashara flani. Ukishapata kwa kushirikiana na waozefu na wadau wengine (ambao hawajui kama una hela) anza hiyo biashara kwa kiasi kidogo ulichobakiza.

Ukishapata uzoefu nido baada ya mwaka utoe kiasi flani kati ya hizo 18M ndio uendelee.
Nashukur kwa wazo lako mkuu.
 
Ushawahi kufanya biashara? Kutumbukiza mzigo wote huo kwenye biashara yanaweza kuja kuwa majuto baadae.

Weka lengo anza na biashara ya mtaji usiozidi mil5 kwanza uusome mchezo. Me si mtaalamu wa biashara, ila kazi kwako kutafuta biashara isiyozidi mtaji wa hiyo mil5. Ila kwa siku ikuingizia faida ya walau 20k na kuendelea.
Barikiwa mkuu
 
Fanya mchakato wa tin namba na leseni ya biashara. Tafuta kijiwe kilicho changamka, anzisha biashara ya miamala ya huduma nyingine za kibenki. Simamia mwenyewe. Kila mwezi utakuwa unakula tu kamisheni.

Katika hicho kijiwe, uza na vitu vingine vya ziada kama kuuza na akubadilisha mitungi ya gesi, weka friji yenye mlango wa kioo kwa ajili ya kuuza vinywaji baridi, nk.

Usiwe na uoga wa maisha kwa kukimbilia kujenga nyumba, kama sisi watumishi wa umma wenye umri mkubwa na tulio na wategemezi lukuki. Nyumba haizalishi! Na kama utajenga ya kukuzalishia, bado itakuzalishia kiasi kidogo sana kwa mwezi ukilinganisha na pesa uliyo izika!
Nashukr kwa Wazo zuri, nmejarb kufuatilia CRDB na NMB kupata kibali chao na vifaa vya kazi, majibu yao ni lazima uwe umedumu kwny biashara atleast 2yrz kiongozi.
 
Niko na business plan ambayo ndio niko nayo na nimeshanunua baadhi ya mitambo bado inaitajika kiasi flani kukalilisha baadhi ya machine nyingine kama uko tayari joint venture 60/40 tunauhakika wa 100, 000Tsh kwa kila siku kiwango cha chini, tunaweza tengeneza mpaka 500,000Tsh kwa siku provided good marketing and plans

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
Naomba business plan yako niione
 
Fanya mchakato wa tin namba na leseni ya biashara. Tafuta kijiwe kilicho changamka, anzisha biashara ya miamala ya huduma nyingine za kibenki. Simamia mwenyewe. Kila mwezi utakuwa unakula tu kamisheni.

Katika hicho kijiwe, uza na vitu vingine vya ziada kama kuuza na akubadilisha mitungi ya gesi, weka friji yenye mlango wa kioo kwa ajili ya kuuza vinywaji baridi, nk.

Usiwe na uoga wa maisha kwa kukimbilia kujenga nyumba, kama sisi watumishi wa umma wenye umri mkubwa na tulio na wategemezi lukuki. Nyumba haizalishi! Na kama utajenga ya kukuzalishia, bado itakuzalishia kiasi kidogo sana kwa mwezi ukilinganisha na pesa uliyo izika!
Watumishi wa umma ni waoga
 
Nashukr kwa Wazo zuri, nmejarb kufuatilia CRDB na NMB kupata kibali chao na vifaa vya kazi, majibu yao ni lazima uwe umedumu kwny biashara atleast 2yrz kiongozi.
Hakuna linalo shindikana chini ya jua. Ukiongea nao vizuri, unaweza ukazipata hizo mashine hata kabla ya hiyo miaka miwili.

Wakati unaendelea kuwasubiria hao jamaa wa benki, unaweza ukaanza na miamala ya simu ambayo inapatikana ndani ya mwezi mmoja tu.
 
Fanya mchakato wa tin namba na leseni ya biashara. Tafuta kijiwe kilicho changamka, anzisha biashara ya miamala ya huduma nyingine za kibenki. Simamia mwenyewe. Kila mwezi utakuwa unakula tu kamisheni.

Katika hicho kijiwe, uza na vitu vingine vya ziada kama kuuza na akubadilisha mitungi ya gesi, weka friji yenye mlango wa kioo kwa ajili ya kuuza vinywaji baridi, nk.

Usiwe na uoga wa maisha kwa kukimbilia kujenga nyumba, kama sisi watumishi wa umma wenye umri mkubwa na tulio na wategemezi lukuki. Nyumba haizalishi! Na kama utajenga ya kukuzalishia, bado itakuzalishia kiasi kidogo sana kwa mwezi ukilinganisha na pesa uliyo izika!
Fact mzee
 
Back
Top Bottom