Nina milioni 20, nataka nianzishe biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Gambamala

JF-Expert Member
May 13, 2014
1,045
766
Wadau, nina mtaji wa milioni 20, eneo la ekari 1 Kibaha. Nataka nianzishe ufugaji wa kuku wa mayai. Tayari nimejenga nyumba ndogo ya kuishi mfanyakazi. Bado naendelea na ujenzi wa mabanda ya kuku.

Ingawa tayari nimefanya maamuzi, lakini naomba mwenye uzoefu anipe mchanganuo wa faida, pia nianze na kuku wangapi.

Ushauri wako ni muhimu tafadhari. Ikiwemo changamoto za upatikananji wa soko
 
Nakushauri usitumbukize m20 yote kwa pamoja. Tumbukiza m10 batch ya kwanza then wakianza production baada ya miezi 5 mpaka 6, weka batch ya pili. Uzoefu utakaoupata kutoka kwenye changamoto za batch ya kwanza utakusaidia kuendesha batch ya pili vizuri na kuepuka gharama zisizo na ulazima.
 
Tha
Nakushauri usitumbukize m20 yote kwa pamoja. Tumbukiza m10 batch ya kwanza then wakianza production baada ya miezi 5 mpaka 6, weka batch ya pili. Uzoefu utakaoupata kutoka kwenye changamoto za batch ya kwanza utakusaidia kuendesha batch ya pili vizuri na kuepuka gharama zisizo na ulazima.
Shukran mkuu, wazo lako nimelichukua
 
Kam unapresha ya kupanda wacha io kitu.tfta kingine cha kufanya.fuga hats kitimoto
 
Kuna thredi nyingi humu zinazohusu ufugaji wa kuku, nenda jukwaa la ujasiriamali.
 
M20 ni pesa nyingi sana for a start up bsn kama huna insight ya kutosha kuhusu potential risks za hiyo biashara, anza na pilot test before your roll out to a large scale.
 
Kama mkuu hapo juu alivyokushauri hakikisha unakumbuka kuwekeza katika security,jenga mabanda imara na yanayozingatia kanuni za ufugaji,hakikisha unamshirikisha daktari wa mifugo katika hatua zote,hakikisha unatunza kumbukumbu zako vizuri,mwisho kabisa ni vyema kuanza kidogo lakini ukifikiria makubwa baadae,all the best
 
Mhh Na Mimi ndo wazo langu la kufuga kuku wa mayai hivi ndo nimenunua kiwanja hapa madale nimechanganyikwa kutokana Na negative feedback kutoka Kwa watu
 
Back
Top Bottom