Nina milioni 20 je nifanye nayo biashara gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina milioni 20 je nifanye nayo biashara gani?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Apolinary, Jun 29, 2012.

 1. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Naam ndugu naomba mnipe mchanganuo wa milioni 20, je nifanye nayo biashara gani? Nb.kama huna cha kuchangia ni bora zaidi kuliko kuponda! NAWASILISHA!
   
 2. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  FURSA YA BIASHARA NI NINI?

  Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara (mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya.

  Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara (Business idea) huanza kwanza kwa kuchunuguza fursa zilizopo katika eneo husika. Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan).

  Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo, naomba kuorodhesha baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji:

  1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi?
  2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi?
  3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko vipi?
  4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya kutosha?
  5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila siku?
  6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani?
  7. .............................
  8. .............................

  Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza kutokana na mazingira husika.

  Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika jamii kuwa ni kawaida, kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida, lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza wazo la biashara.

  Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo.

  Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua.

  Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi.
   
 3. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 4. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Biashara ambayo unaweza kufanya na kutajirika kwa haraka endapo utapata sehemu ni kufungua studio kwa mtazamo wangu
   
 5. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 6. chash

  chash JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Upo mji gani na sasa hivi unajishughulisha na nini? una elimu kiasi gani? usione vibaya kuulizwa maswali haya kwa sababu inaweza kusaidia mtu anayetaka kukushauri.

  Kuna biashara nyepesi kama za kutoa bidhaa point A na kupeleka point B na hizi zinaweza kutegemea mahali ulipo. Kuna biashara zinazo hitaji taaluma, accounts nk unaweza pia kuanzisha kiwanda kidogo au labda upo shambani ukaweza kuingia kwenye kilimo cha kisasa cha ufugaji au kilimo.

  Mara nyingi unapata biashara inayotoa mtu ni ile alikuwa tayari na ufahamu kiasi au inayo eleweka kwa wepesi. Kuingilia kitu ambacho hauna experience nacho inaleta hasara kutokana na learning curve au kutojua.

  Pia kama una hiyo hiyo m20 ni muhimu labda ulenge kuanzisha biashara inayo hitaji m10 sababu biashara nyingi uzidi budget na hela inahitajika zaidi.
   
 7. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 8. chash

  chash JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Mkuu, nimefikiria nikupatie ushauri gani, yaani hali sasa hivi sio kama zamani. Nafasi za biashara, ukilinganisha na miaka yazamani ni chache mno. Watu wengi wanajua biashara ni duka hili au lile, kwa hiyo maduka yamekuwa mengi sana. Kwa mtazamo wangu mtu anaye jishughulisha na mambo mapya yanao tumia technologia ya kisasa ana uwezo mkubwa wa kufaulu kwa sababu ndio mambo hayo yana anza anza. Tukizungumzia viwanda hela yako ni ndogo mno. Biashara ya importation tena hela yako bado haitoshi. Kama unapenda shule ungelitafuta kozi ambayo utapata hadi degree na ikiwezekane masters kwa sababu watu wenye vyeti hivyo wataendelea kuwa na maisha mazuri sana Tanzania. Ninge washauri walio kuwa shuleni au wenye uwezo wa kuongeza masomo wasome kwa bidii kwa kuwa knowledge is power na mtu mwenye vyeti vizuri au knowledge nzuri hata akishindwa kwenye biashara maisha yake hayawi mabaya.
  Biashara ambayo ina future kwa mtazamo wangu sasa hivi na siku zijazo na ambayo itakuwa inahitajika na watu wengi ni kilimo hususan cha umwagiliaji wa matone au drip irrigation. Hiki unahitaji uwe na shamba yenye maji karibu au kisima cha maji. Utaweka green house kubwa ya 100m x 50m kama zile unazo ziona arusha kwa maua lakini upande mboga za hybrid ambazo zina mavuno makubwa kama vile nyanya, pili pili hoho, bamia, nk Kingine pia ni kuku wa kienyeji wa hybrid. Hawa hawatofautiani sana na wakizungu kwa sababu wanataga mayai daily isipokuwa mwezi moja kwa mwaka. Wanakuwa hadi kilo 4-5. Ukiamua kuuza nyama utauza baada ya miezi miwili na gharama zao zipo chini kwa ajili hawahitaji chakula spesheli, kwa hiyo faida ni kubwa. Zingatia pia watu ni wengi na wanazidi kuongezeka hiyo biashara zinazo husu chakula zitaendelea kufanya vizuri tu.

  Kwa biashara yeyote hapo juu nadhani hela yako itatosha na itabaki ya kukuwezesha kufuatilia ufahamu wa biashara yenyewe kama vile kusafiri nk.
   
 9. Mjamaica

  Mjamaica Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ushauri mzuri mkuu CHASH, tafadhali mimi naomba unisaidie kama unaelewa naweza pata wapi mbegu ya kuku wa kienyeji wa HYBRID nataka nianze ufugaji wa kisasa maana nina kaeneo kangu ka kama ekari moja na pana kisima chenye maji ya kutosha kwa mwaka mzima.
   
 10. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ushaurh wa CASH HAPO JUU UMENIGUSA SANA! ITABIDI NIINGIE KWENYE KILIMO CHA NYANYA AU UFUGAJI WA KUKU WA KISASA.PAMOJA NA KILIMO
   
 11. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuku wa kienyeji wa hybrid wanapatikana wapi jamani ? kama kunamtu anajua kwa hapa Dsm anijuze na kwa bei gani ?
   
 12. chash

  chash JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. t

  truckdriver JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 504
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Tuna shamba wilaya mpya ya kilindi tunataka tuanze kulima. Kuna miti mingi ya mbao(hard wood) inabidi tuikate ili kusafisha shamba kama unaweza fanya biashara ya mbao (au unafahamiana na wanaofanya biashara ya mbao) tupo tayari kwa maongezi jinsi ya kushirikiana.
   
 14. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 15. t

  truckdriver JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 504
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
   
 16. K

  Kidogo chetu JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 771
  Trophy Points: 280
  Be careful hiyo ni pesa nzuri kuanza biashara nakuombea usjeingia mikono ya matapeli
   
 17. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
   
 18. Fasouls

  Fasouls JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 922
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Unaweza pia kuongeza kipato chako kwa kunidhamin mimi ama kunikopesha sh ml 5 then baadaya kuandikishia nitakuripa baada ya miaka 3,yaan baada ya masomo yangu ya degree ya kwanza.
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu.@Apolonary Kama ni mimi ninazo hizo shs millioni 20 Biashara nitakayoifanya, nitanunuwa TV 20 na 20 Play station Game Machine [​IMG]

  na kukodisha Sehemu chumba kikubwa kwa ajili ya kuwaingiza Watoto wadogo kuja kuchezea Game kwa kila saa unamlipisha mtoto shilingi Elfu 1 na utakuwa unaingiza kila siku Maxmum shilingi laki 1 na unaweka Umeme wa Solar sio umeme waTanesko. Unaionaje hiyo biashara yangu?
  [​IMG]
   
 20. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Nataka/nimeamu kufanya uamuzi wa kufanya kilimo sasa wadau nifanye kilimo cha aina gani ukizingatia na hali ya ukanda wa kaskazn?
   
Loading...