Nina mil 12. Je, inatosha mimi kuhamia Marekani au Canada?

music mimi

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
441
758
Wakuu mimi nna ndoto ya kuishi nje ya nchi haswa Marekani au Canada.

Nimepambana kwa muda mrefu nipate scholarship za huko ila ni tough haswa kwa sisi wenye GPA za lower second.

Nna million 12 fulani kibindoni vipi inatosha kutimiza ndoto? Njia ya kwenda huko nyepesi ni hipi?
 
Nakazia.

Lema ana konekshoni za Gari, Nyumba...

"Mtoto, ni mtoto tu" -- Dr. Remmy.

Connection ni connection tu hata iwe ya gari, nyumba au ugali wa kizungu.

Usimkatishe tamaa mdau maisha ni popote ndiyo uraia wa ulimwengu unavyoanza huo.

Leo Rusesabagina yuko huru toka kwenye meno ya paka shukurani kwa kuwa raia wa ulimwengu. Makapuku wangapi madhila yao hayatakaa yajulikane?

Aende kamanda yeye ni hazina.
 
Ina weza kusaidia...

Fanya upembuzi yakinifu wa....
1. Nauli

2. Sehemu ya kulala kama utapanga angalau miezi mitatu au minne nyumba au chumba cha dolla 500 kwa mwezi Au kama utapata pungufu, tafuta mitandaoni kama Air BnB nk

3. Angalia vyakula

4. Nauli za kutembea mitaani kwenda kutafuta michongo na watu tofauti

5. Angalia mawakala wa kazi waliopo huko na eneo utakalo fikia na gharama zao kama utamudu kuwa lipa ili uweze kupata kazi

6. Angalia wana sheria kama utawahitaji na gharama zao uweze kusaidika kutafuta permit mbalimbali kwa kupitia hadhi mbalimbali kama hadhi ya ukimbizi ambayo itakuwezesha kukupa manufaa zaidi

7. Mavazi kama nguo za baridi na viatu vizito Au mabuti makubwa ya baridi nunua mtumba Au vya dukani bongo kwa bei nafuu

8. Tafuta barua ya mwaliko mitandaoni zipo zina patikana vizuri tu na zisizo na magumashi

9. Tafuta Bima ina patikana vyema kabisa bila shida kwa gharama nafuu

10. Tafuta vitu ambavyo vitakuwa kama dhmana yako kuonesha utarejea na hauendi kuzamia, kama una kiwanja Au viwanja kwa majina yako, Au nyumba, kama ni mfanyakazi pia, kama una milki gari Au magari, kama una familia au mtoto/watoto

11. Bank statement zina patikana bila shida

Uki shindwa kuingia marekani Au Canada kutokea bongo basi jaribu nchi nyingine alafu upitie katika hizo nchi kuingia marekani

Mfano
Omba Australia, Germany, Poland, Turkey, Ubelgiji, Sweden, China nk

Kila la kheri


music mimi ingia hapo ila nunua ticket upate barua ya mwaliko kuingia Ugiriki

Ukikosa visa wana kurejeshea pesa yako, maelezo yote yapo huko, una weza kuwa mwanzo wa Safari yako ya unapo pafikiria huko duniani na kupata connection mbalimbali

Mialiko ya hivi ipo mingi sana huko Duniani... jitahidi kutembelea site mbalimbali

Pia tumia sites mbalimbali za watembezi kama CS (couch surfing) hii itakusaidia kwa eneo unalo taka kwenda duniani, ita kuunganisha na watu mbalimbali huko ulimwenguni

Jisajiri na uweze kutafuta watu wa kukuhost kwa muda fulani kama week week kadhaa au mwezi na wewe una changia kama vitu chakula nk

Download hiyo app itakusaidia... tafuta na app zingine za kukuunganisha na watu wa mataifa mbalimbali
 
Hakimbii anaenda kama sehemu katika ndoto zake...!

Wewe kama ndoto yako mfano ni kujenga nyumba basi haimaanishi una mkimbia baba mwenye nyumba au una kimbia kwenu kwa baba yako na mama yako nk
Sijajua watu wana tatizo gani aisee why wakisikia US au nchi zilizopiga hatua wanakuwa wakali sana?

Maana sijaona mantiki ya watu kunikejeli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom