Nina Miaka 26, lakini Usoni utafikiri nina miaka 35

hiden

JF-Expert Member
Sep 28, 2015
376
691
Wakuu na wataalam wa Ngozi naombeni msaada.
Nina miaka 26, nimezaliwa 1992. Tatizo langu ni uso wangu kujaa mikunjo hasa mikunjo ya ndita kwenye paji la uso.

Sijajua tatizo ninini, yani nikikaa na baba angu utafikiri yeye ni kaka angu.

Mikunjo yangu ni kama ya Stive Nyerere, yani nikikaa na vijana wa umri wangu sifanani nao na ambao hawanifahamu hunisalimia wakidhani mi ni mkubwa.

Ni hospitali ipi naweza kwenda kutibiwa?
Au ni hospitali gani ina wataalam wa ngozi hapa nchini?

Naombeni msaada.
 
ningekua nasoma ningekutumia sana pale nlipokua narudishwa kwa makosa mbali mbali bangala seminary kuna mtu alishawahi kumleta mdogo wake kama mzazi wake na akafanikiwa but nnachotaka kukushauri ni jikubali! unaonekana hujipendi hiyo ni fursa jikubali fikiria juu ya fursa iliyopo moyoni mwako
 
Angalia ndugu zako km wapo ambao sura zao hazilingani na umri wao basi huo ni ugonjwa wa kifamilia hakuna kitakacho kusaidia. Kama hamna ndugu wa namna hiyo basi huenda ikawa huli vyakula vizuri(Mboga n.k.) au hulali masaa yanayostahiki.
 
Mkuu tafuta mafuta yanaitwa habat soda au black seed oil.
Kariakoo yanapatikana sana.

Waweza kuyatumia kwa kupaka kama mafuta au waweza kuwa unayatumia kijiko kidogo cha chai kwenye juice kila siku.
Ladha ya mafuta haya ni uchungu kwa mbali, ila sio mbaya sana, waweza changanya na asali kidogo kupunguza makali yake.

Ni mwezi mmoja tu utaona mabadiliko.
Utaleta ushuhuda hapa
 
Aisee pole

Fanya mazoezi
Usipende kukunja sura
Kunywa maji kwa wingi na ule matunda kwa wingi

Huo uso wako kama ni binti uwe na mazoea ya kuupaka ute wa alovera wenye mchanganyiko wa asali na manjano walau Mara mbili kwa week...utaona mabadiliko

Kama ni wakiume pendelea kupakaa mafuta ya olive oil..au vaseline
 
Ndugu mm nalingana na wewe kiumri.Mimi mwenyewe ninaonekana kuwa na umri mkubwa kwa sababu sina pesa.Nikipata pesa Nile nnachotaka, nivae nguo nzuri niwe na miradi kadhaa kiasi kwamba uhakika wa kupata pesa upo, basi mwili utaonekana wa kijana mdogo.Tumuombe Mungu tuu nadhani mambo yatakuwa poa maana kuwaza maisha, ajira hakuna n.k ndo vinavyotufanya kuonekna hivi.
 
Mkuu tafuta mafuta yanaitwa habat soda au black seed oil.
Kariakoo yanapatikana sana.

Waweza kuyatumia kwa kupaka kama mafuta au waweza kuwa unayatumia kijiko kidogo cha chai kwenye juice kila siku.
Ladha ya mafuta haya ni uchungu kwa mbali, ila sio mbaya sana, waweza changanya na asali kidogo kupunguza makali yake.

Ni mwezi mmoja tu utaona mabadiliko.
Utaleta ushuhuda hapa
naam..

pia afanye mazoezi aepuke kula hovyo na ahakikishe anakunywa maji walau 4 litres per day...

asubuhi alfajiri kabla ya mswaki aanze na walau nusu lita...
 
ningekua nasoma ningekutumia sana pale nlipokua narudishwa kwa makosa mbali mbali bangala seminary kuna mtu alishawahi kumleta mdogo wake kama mzazi wake na akafanikiwa but nnachotaka kukushauri ni jikubali! unaonekana hujipendi hiyo ni fursa jikubali fikiria juu ya fursa iliyopo moyoni mwako
Mkuu ndita ya usoni ina fursa gani kwa mfano?
 
Huu uzi umekaa ki comedy sana ,yaani unajizuia kucheka lakini unajikuta umecheka tu ..Japo sikucheki ndugu yangu nimecheka ulivyo wasilisha.
 
Wakuu na wataalam wa Ngozi naombeni msaada.
Nina miaka 26, nimezaliwa 1992. Tatizo langu ni uso wangu kujaa mikunjo hasa mikunjo ya ndita kwenye paji la uso.

Sijajua tatizo ninini, yani nikikaa na baba angu utafikiri yeye ni kaka angu.

Mikunjo yangu ni kama ya Stive Nyerere, yani nikikaa na vijana wa umri wangu sifanani nao na ambao hawanifahamu hunisalimia wakidhani mi ni mkubwa.

Ni hospitali ipi naweza kwenda kutibiwa?
Au ni hospitali gani ina wataalam wa ngozi hapa nchini?

Naombeni msaada.
Ndita sio ugonjwa wa ngozi ni wa akili wewe ni ke au me
 
Hivi vipimo vya maji vizingatiwe, wapendwa lita za Maji zinaendana na uzito wa mwili wako,

Mtu hawezi kua na kilo 50 akanywa maji lita 4 kwa siku maji yakizidi mwilini ni tatizo.

Kwa haraka haraka najua kilo 50 anakunywa lita 2 kwa siku, kilo 75 anakunywa lita 3 kwa siku na kilo 90 mpk 100 anakunywa lita 4 kwa siku.

Mengine mnaweza kugoogle.
 
Back
Top Bottom