Nina mchumba nataka kumuoa, lakini ana mtoto wa miezi 6 je nitaruhusiwa kufanya naye mapenzi?

MoonBoy

Senior Member
Jul 15, 2016
195
133
Habari zenu ndugu zangu wataalamu wa masuala ya kiafya na wengine wote

Naombeni ushauri wa kiafya. Nina mchumba wangu, nilikuwa mbali naye kulingana na utafutaji wa maisha, ila ahadi yetu ni kuoana. Juzi tarehe 6 mwezi wa 12 mwaka 2019. Nilikwenda nyumbani kwao Dar es Salaam. Lakini nilishtushwa kwa kumkuta ana mtoto wa miezi sita. Nampenda sana mchumba.

Kuwa kwake na mtoto, imeniuma lakini pamoja na hayo, bado namuhitaji. Sasa ushauri wa kitaalamu ninaoutaka, mtoto yule haiwezekani kuachwa mahali, hivyo lazima nikaishi naye, sijakataa hilo.

Sasa je, itawezekana kufanya tendo la ndoa na mke wangu, ingali mtoto ni mdogo? Angelikuwa wangu, najua hakuna madhara, ila sio wangu. Je, kuna athari gani zitamtokea mtoto au ni maneno tu? Na kama kuna athari zozote, basi nitamuoa na kumuangalia tu mpaka aachishe kunyonyesha, maana siwezi kutoa nje au kutumia kondomu.

Naomben ushauri wenu. Bado sijamuoa, ila nataka kumuoa.

Ahsanteni na Mwenyezi Mungu awabariki wote mtaonipa ushauri juu ya hili.
 
Kama una mpenda na yeye anakupenda, anzisheni familia hata usiogope ushauri wa wengi humu. Maana wengi watakukebehi na kukudharau, hayo ni maisha yako live it.
 
Yaani kutusumbua kote huku kumbe mwisho wa siku wataka tu kujua kama unaweza kujig jig na mkeo mtarajiwa au lah...hehehe

Jibu ni kuwa hakuna madhara...
 
Muache aowe, ila dhambi yake ni pale akija kuanza kumsuta huyo binti kwa hicho kitendo mbeleni.
Kisa katambua uzuri wa mwanamke sio muonekano.
Tafuta mwingine, wanawake wapo wengi.
Kama kakusaliti na hakukuambia kuwa ana ujauzito hadi Umekuja muona live ana mtoto ina maana hana upendo nawe.
 
Kama hamko tayari kupata mtoto mwingine mpate ushauri wa nyota ya kijani.
 
Mechi kabla haijaanza unaongozwa 1-0 ....natania boss ndio unaruhusiwa
 
Inaonyesha una mapenz ya dhati na huyo mchumba wako,heko kwa hilo... Madhara hamna ila kuna umuhim wa uzazi wa mpango kama ulivyoshauriwa na hapo na Sky Eclat ili asije pata mimba nyingne while mtoto bado mdogo
 
Habari zenu ndugu zangu wataalamu wa masuala ya kiafya na wengine wote

Naombeni ushauri wa kiafya. Nina mchumba wangu, nilikuwa mbali naye kulingana na utafutaji wa maisha, ila ahadi yetu ni kuoana. Juzi tarehe 6 mwezi wa 12 mwaka 2019. Nilikwenda nyumbani kwao Dar es Salaam. Lakini nilishtushwa kwa kumkuta ana mtoto wa miezi sita. Nampenda sana mchumba.

Kuwa kwake na mtoto, imeniuma lakini pamoja na hayo, bado namuhitaji. Sasa ushauri wa kitaalamu ninaoutaka, mtoto yule haiwezekani kuachwa mahali, hivyo lazima nikaishi naye, sijakataa hilo.

Sasa je, itawezekana kufanya tendo la ndoa na mke wangu, ingali mtoto ni mdogo? Angelikuwa wangu, najua hakuna madhara, ila sio wangu. Je, kuna athari gani zitamtokea mtoto au ni maneno tu? Na kama kuna athari zozote, basi nitamuoa na kumuangalia tu mpaka aachishe kunyonyesha, maana siwezi kutoa nje au kutumia kondomu.

Naomben ushauri wenu. Bado sijamuoa, ila nataka kumuoa.

Ahsanteni na Mwenyezi Mungu awabariki wote mtaonipa ushauri juu ya hili.
Ukuu utakuja unalia hapa
 
Back
Top Bottom