Nina matatizo ya kifedha na sina msaada wowote. Nimepanga kuwatelekeza mke na watoto

Nimeshafanya booking, nitaondoka na bus la Kidia One kwenda mkoani Arusha nikatafute maisha. Ninasikitika kwakua nitaondoka bila kuaga na ninaiacha familia yangu katikati ya ukata mkubwa wa kifedha huku ikishindwa kumudu mahitaji yakila siku. Lakini kuliko nibaki tufe wote acha nijiendee Arusha nikabangaize maisha.

Januari hii mwanangu mkubwa Zawadi alitakiwa kwenda shule tar 7 na ada mkononi Sh.680,000 tasilimu. Hata mahitaji mengine madogomadogo kama sweta la shule na viatu navyo vimeshindikana. Kodi ya nyumba itaisha tar 23 na mwenyenyumba amedai nihame kwakua nyumba yake anabadili matumizi, hapangishi.

Mimi na mke wangu wote tulikua tunafanya kazi. Mimi kwenye kiwanda cha Gypsum na mke wangu kampuni kubwa ya Vinywaji. Lakini kama mnavojua kikiri na kakara za kampuni binafsi hasa uzalishaji unapopungua, alianza mke wangu kufukuzwa nikafuata mimi.

NSSF wananipa elfu 24,500 kila mwezi fao la kukosa ajira, huu ni mwezi wa 4 na watalipa ndani ya miezi 6 tu. Mke wangu yeye hakua anachangia.

Nimejaribu kumshauri mke wangu tu-downgrade maisha hataki. Kodi kwa mwezi tunalipa 180,000 chumba masta, sebule na jiko Mburahati. Mtoto anasoma darasa la tatu ada kwa mwaka jumla 1,550,000. Nimeshakopa sana, nimejaribu vibarua lakn kazi nzito siwezi nina matatizo ya kifua.

Ninamuacha mke wangu mama zawadi, zawadi na Taia mtoto wetu wa mwisho kwenye nyumba ya kupanga na hali mbaya ya kiuchumi. Lakini sina namna. Mimi na mke wangu tulishapitia matatizo na migogoro mingi sana lakini kwa sasa imeisha na tulishasameheana. Ugumu wa maisha ndio unanifanya nikimbie Dsm

Kama kuna msamaria anaweza kunipokea na kunipa hifadhi ya siku mbilitatu Arusha tafadhali sana aje PM na nitashukuru sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Weka namba mkuu wasamalia wema watatoa kwa nafas zao
 
Back
Top Bottom