Nina matatizo ya kifedha na sina msaada wowote. Nimepanga kuwatelekeza mke na watoto

Acha ufala,tafuta chumba cha bei nafuu hata elf 20.vipo vingi tu kiwalani,yombo hata huko huko mabibo,mtoto muhamishie shule ya serikali.wewe ni mwanaume ingia mtaani piga hata debe au biashara ndogondogo.ila kamwe usiikimbie familia utajuta maisha yako yote utakaposikia mkeo anajiuza mjini na mwanao ni teja/kibaka au ombaomba.yakishindikana yote rudi kijijini kuna fursa
 
Nunua mchele kilo 10 shs 20,000. machinjioni nyama ya kichwa cha ngombe shs 10,000 sokoni mboga mboga na viungo shs 5,000. mkaa 3,000. jumla 38,000/= mwambie shemeji apike kilo 5 weka kwenye ndoo ya lita 20. mboga weka kwenye kisado. jumatatu saa 7 kamili mchana uwe umefika pale ubungo kampuni ya wachina wanapojenga barabara ya kimara. beba sahani 10 bila vijiko wala vibakuli. wauzie vibarua wanaojenga bara2 sahani 1500. sahani 80 ni 120,000/= faida haitapungua 50,000/= jaribu utaniambia. Mimi niliwahi kuanza maisha hivyo wakati kampuni ya MOWLEM Construction wanajenga barabara ya port access sasa hivi mandela road sasa hivi nipo vizuri usipime. ondoa unishoo kaza buti broo utaona matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngararimu nza mbala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah nataman nimlaumu JIWE kwa kuyaleta haya ila nawaza siye anaeleta fedha nyumbani ila nafikiria zaidi labda anahusika namna moja au nyingine(nadhani nimepatia hapa)

Real JF sa hivi imekuwa sehem ya watu kueleza shida kuliko habari.
pole mkuu kila la heri

Mkuu jiwe anahusika kwa 10000%.
Maamuzi yake yasiyo na hekima ndiyo yameleta haya yote bila kumsahau bashite


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mwanaume mzima unakuja kuandika vitu kama hivi humu jf??? Hivi kweli kama mwanaume aliyekamilika kabisa unaweza kufanya maamuzi ya kipumbavu kama hayo? Lemme tell you something
Kuna mdogo wangu wa kike (undugu wa manati) alishoboka na mchaga mmoja hivi alikua na duka lake kubwa kariakoo la vitu vya ndani yaaan decoration za ndani ya nyumba, wakaoana fastaaaa maisha enzi za Kikwete yakawa bomba dogo akanona acha tu. Sasa hali ikawa upside down mume akafilisika ila akafanya maamuzi kama yako bila kushirikisha mtu yeyote. Aliacha mkewe na mtoto wa kiume kwenye nyumba kodi laki tatu kwa mwezi imagine. Ye akakimbilia Msumbiji machimboni huko bila taarifa, eeeeeeh bwana weeeee dogo aligongekaaaaaa ili atunze mtoto wake na kulipa kodi.
Unakumbuka wakati wa fukuza fukuza kule Msumbiji hadi jeshi likaingilia kuwaleta wahanga makwao?! Basi naye alikua mmoja wao aliyebebwa toka Mtwara hadi mjini kapauka peeeee hana kitu halafu now mke wake amekaa vizuri ana biashara yake na maisha safi ila akamkataa mumewe wakaenda mahakamani wakavunja ndoa rasmi...now huyo jamaa yupo kitaa anahangaika tu na maisha haya
Usifanye makosa kama ya namna hiyo mkuu, kaa shirikisha watu wazima na wakubwa wa dini yako msikitini au kanisani utapata ufumbuzi

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekupa “like” lakini naona una ushauri wa kwenye vitabu, mimi namini mleta mada mpaka kafikia kiwango hiki jua kunaishu kubwa sana , siyo rahisi mwanaume kufikia uamuzi huu kirahisi, hata yeye angekuwa ana mshauri mtu asingempa ushauri wa kukimbia familia, siungi mkono ukimbiaji wa familia lakini nadhani shida ni kubwa sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pole bro,usiwatelekeze,utawatesa sana kisaikolojia watoto wako,ni bora walale njaa,lakini upo wanakuona,kuriko kulala njaa,harafu wanaambiwa baba yao kawaterekeza,inauma sana.
Kama wakwe kijijini,au wazazi wako wapo vzr kiasi,ni bora uwaperekee mjukuu kwanza,harafu wewe komaa mjini mpaka kieleweke,wewe unaujuzi gani wa ufundi,unayo driving licence?

Sent using Jamii Forums mobile app
Me ninaa driving licence halii na me ninzito saaanaaa. Nipee mchongo basii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo hivyo hayo ndo maisha
Afadhali ya wewe mambo yakigoma unaenda kwa mzazi, umebarikiwa! Akina sie inabidi upambane kwa namna zote, wewe na Mungu hadi kieleweke, uzuri upate mke na watoto waelewa, vinginevyo waweza toroka kama jamaa yetu, ila nitamtorokaje mke? Mtoto wangu? Hapana! Tena bila kuaga huku ukiacha hujui wataishije?
Hapa nawaza tu hivi nikifa watoto wangu wataishije? Watasomaje? Je mali nilizoacha zitawafikisha mbali hadi wajitegemee?

Maisha ni fumbo ila kutoroka hapana lazima kuonesha uanaume.
''No situation is permanent''

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada sorry, Wewe ni mwenyeji wa mkoa gani?

Ila kama ni mimi ningempeleka wife na watoto home kwa maana kwa wazee wangu. Mie nabaki mjini najipanga.

Mie nilishapitia hayo, na kuna story nilishaiweka hapa kwenye uzi flani hivi unaoenda kwa jina la "WALE TUNAODAIWA MADENI MAKUBWA TULIWAZANE HAPA" nikajipanga na maisha yakaendelea.

Ref hakuna tatizo jipya. Tatizo ulilo nalo sasa, Millions of people walishakutana nayo matatizo wakasolve na maisha yanaendelea.
Kaza Jogoo hafi kwa utitiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom