Nina Mashaka sana kuwa kupotea kwa Ben Saanane ndiyo operesheni UKUTA

Vyovyote itavyokuwa kama pande hizi mbili zimehusika basi ni moja ya mikakati mibovu kufanyika nchini bila kusoma nyakati..... kwa fikra yakinifu dhana huongeza pande nyingine katika hili

[HASHTAG]#GodblessBen[/HASHTAG]
 
Umefikiria vizuri sana mkuu....Pia unaweza fikiri zaidi nje ya BOX na kusema ya kuwa TAASISI YAKE NDIO ilikuwa inamtumia VIBAYA kutoa kashfa kwa MKUU WA NCHI ili hali wao wana lao jambo juu ya BEN....ILI mwisho wa siku baya lolote litakalo mtokea BEN ionekane ni serikali ndio imehusika.....SASA kibaya zaidi hii MISSION YA CHADEMA IMEBUMA tuliowengi tunawanyooshea VIDOLE wao juu ya UPOTEVU WA HUYU KIJANA....ndio maana hata viongozi wao wanabaki kubwabwaja juu ya hili jambo.......
Yaan nyie watoa post mnaakili finyu sana na ili kuthibitisha hilo labda nuwaulize usalama wa taifa ni chombo cha serikal au chadema. kama ni chombo cha selikali kinafanya nn ili kugundua hili. mana wai ndio wanawataalamu na vyombo vya kufanya kujua huyu mtu yuko wapi sio chadema wala mwingine asa mi nashangaa wa tz mnaongea sana wakat wenye mamlaka ya kusemea hili yaan chombo cha serikali hakijasema lolote. hebu tusiruhusu akili ndogo itawale akili kubwa. inshu za kisiasa hata kama zimetumika wapo watu maalumu wa kufuatilia hilo hebu tuache wao ndio wawe wasemaji. naamini dhambi ya hisia ni mbaya kuliko dhambi ya zinaa tuache hisia tofauti kwa vyama vya siaasa na selikali pia tuone kama ni tatzo limetokea linahitajika kutatuliwa na vyombo husika. haina mana tuwalipe pesa zetu hawa halafu washindwe cha muhimu wao watafute yuko wapi kisha watueleze nan kahusika ndio la maana hiyo habari ya kuhususanisha hituba au operation mbona hujasema kabla ya kupotea kwa huyo saanane kama ww ulikua unajua kutabiri. tusikubali ukada wa vyama ukatupa hisia za kitoto
 
Sijui ni kwa nini vyombo vya dola vinashindwa kufuata ushauri wa Lissu wa kuchunguza mawasiliano yaliyofanywa na Ben dakika za mwisho kabla ya kupotea ambayo yangeweza kusaidia kuleta mtiririko wote wa tukio,matokeo yake mtoa ushauri ana kamatwa na kuhojiwa utafikri kuna kitu wanakifahamu ambacho hawataki kijulikane.
 
Unafahamu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na vyombo vya usalama!?
 
Yaan nyie watoa post mnaakili finyu sana na ili kuthibitisha hilo labda nuwaulize usalama wa taifa ni chombo cha serikal au chadema. kama ni chombo cha selikali kinafanya nn ili kugundua hili. mana wai ndio wanawataalamu na vyombo vya kufanya kujua huyu mtu yuko wapi sio chadema wala mwingine asa mi nashangaa wa tz mnaongea sana wakat wenye mamlaka ya kusemea hili yaan chombo cha serikali hakijasema lolote. hebu tusiruhusu akili ndogo itawale akili kubwa. inshu za kisiasa hata kama zimetumika wapo watu maalumu wa kufuatilia hilo hebu tuache wao ndio wawe wasemaji. naamini dhambi ya hisia ni mbaya kuliko dhambi ya zinaa tuache hisia tofauti kwa vyama vya siaasa na selikali pia tuone kama ni tatzo limetokea linahitajika kutatuliwa na vyombo husika. haina mana tuwalipe pesa zetu hawa halafu washindwe cha muhimu wao watafute yuko wapi kisha watueleze nan kahusika ndio la maana hiyo habari ya kuhususanisha hituba au operation mbona hujasema kabla ya kupotea kwa huyo saanane kama ww ulikua unajua kutabiri. tusikubali ukada wa vyama ukatupa hisia za kitoto
Ukweli ni kwamba wapo wanasiasa wanafanya siasa za kimafia.. Kutesa, kuteka, kuua kwao sio issue.. Ref. Issue ya Lwakatare
 
Ndugu zanguni,

Hili jambo la kupotea kwa Ndg. Ben Saanane, kwa sasa huenda ndiyo Drama Kali zaidi Kisiasa na Kiusalama. Kwa binadamu yeyote lazima linapotokea jambo lisilo la kawaida kama hili ni lazima ajiulize maswali mengi kuwa inawezekana ni hivi au ni vile.

Katika kadhia hii, kuendana na mijadala inayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali watoa maoni wanaonekana kuamini kati ya mawili. Ben kutekwa na vyombo vya serikali kwa ajili ya 'kumshikisha adabu' au kutoa onyo kwa wakosoaji wengine au Ben kufichwa na Viongozi wa taasisi anayofanyia kazi ya CHADEMA kwa ajili ya kuionyesha dunia kuwa Serikali haitaki kukosolewa. Kwa maana ya kuipakazia serikali imemteka, lakini katika maudhui hiyo ya pili wapo wanaofikiri kuwa huenda alitofautiana na viongozi wake wakaamua kumfanyia 'Umafia'.

Dhania zote hizi zinaibuka kwa sababu tulio wengi hatujui kabisa ukweli wa jambo hili ukiacha waandaaji na watekelezaji wa jambo lenyewe, na Mungu aonaye sirini. Na huwezi kumzuia binadamu kuwaza sana sana aamue tu kutokuyatoa hadharani mawazo yake.

Katika kila kundi la dhania hapo juu ni lazima mtu yeyote wa kizazi cha kuhoji ajiulize maswali mengi kabla ya kuipa dhana yake asilimia kubwa zaidi ya nyingine.

Mimi nimepembua na kuchanganua na kujikuta nashawishika kuamini kuwa kupotea kwa Ndugu yetu Ben Saanane ndiyo haswa Operesheni UKUTA ambayo siku Mwenyekiti anatangaza kuiahirisha alisema itafanyika kivingine.

Nimejiuliza yafuatayo:

1. Kwa nini Ben!?
Je, Ben ndiye mtoa Kashfa na mkosoaji wa serikali kuliko wengine!? Mbona wengine walifunguliwa mashtaka ya makosa ya Mtandao!?

2. Kwa nini CHADEMA wanatumia nguvu kubwa ya kutaka kuuaminisha Umma kuwa Serikali imehusika na jambo hili badala ya kushirikiana na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi?

3. Kwa nini Mwajiri wake amekuwa na kigugumizi kuzungumzia sakata hili!?

4. Kama Taasisi hii hii iliweza kutengeneza mikakati ya kuwateka watu na kuwapa mateso makali kwa vile tu walitishia maslahi yao, watashindwaje kwa Ben!?

5. Hotuba ya Ndugu Mwenyekiti Mbowe huko ughaibuni aliyeelezea kuwa alilengwa na maguruneti na serikali ili atolewe uhai lakini watu waliompenda wakaamua kuwa ngao ili wafe badala yake.. (hotuba ile ilinishawishi nitamani kujua hatima ya uchunguzi wa ni nani aliyelipua lile bomu kule Arusha) nimejiuliza hili la Ben haliwezi kuwa ni maandalizi ya hotuba nyingine ughaibuni!?

Haya pamoja na mengine mengi yanayonizunguka kichwani yananishawishi niamini kuwa hii ndiyo operesheni UKUTA vol. 2, naomba kwa Mungu vyoyote iwavyo kijana huyu aliyetumika kama Starring kwenye Tamthiliya hii amalize salama, na arejee kuungana tena na familia yake, ndugu na marafiki zake katika kuchangia ujenzi wa nchi yake!!

Wakatabahu
Ben hajapotea, angekuwa amepotea na yupo kwenye mazingira ya hatari, mbowe na chadema wangeshakuja juu muda mrefu. lakini wanalazimishwa hata kuongea jambo linalotufanya tuelewe kuwa labda wanajua alipo.
 
Kapotea kivipi? Kwani alikuwa anaenda wapi,sema tu haijulikani yuko wapi.
 
Kama aliweza kummwagia mwandishi flani tindikali, na baadae kumpa zawadi, atashindwa kumteka huyu dogo kwa maslahi yake?
 
Serikali inataka kutua zigo CHADEMA?

Serikali inawajibu wa kulinda raia wake maana ina uwezo huo.

Ben awe ametekwa na Mbowe ama Baba yake mzazi, sisi tunaitaka serikali iturejeshee Ben Saanane akiwa hai.

Exactly, this is the point!

Kama kweli serikali na vyombo vya uchunguzi vinajua kufanya kazi yake ipasavyo wamtafute Ben na kumrejesha awe yumo ndani ya nyumba ya Mbowe ama ktk ofisi za CHADEMA!

Unajua kuna watu wanataka kufanya watanzania ni watu wajinga sana kwamba wanaweza kuwageuza geuza kama chips za viazi zinavyokaangwa ktk flying pan....

Yaani serikali hii yenye fedha, TISS, Polisi, Secret Service, Magereza, JWTZ yaani ishindwe kutambua aliko Ben ama mtu yeyote aliyepotea!!??

Hakuna kitu hapo, hili ni jibu la moja kwa moja kuwa serikali yenyewe is responsible na sasa wanatumia mbinu zile zile zilizowahi kushindwa kwa kishindo kikuu miaka ya nyuma kwa kuihusisha CHADEMA ili sijui iweje.....

Soma maelezo ya Waziri anayehusika na ulinzi na usalama wa raia na mali zao aliyoyaandika yeye mwenyewe three or five days ago na kuyatupia humu utagundua mengi sana nyuma ya pazia ya utetezi binafsi wa mtu huyu...

Then, rejea historia yake ya nyuma huyu mtu ya siasa chafu huko, you will understand what I
mean!!

Halafu huyu huyu mtu kakabidhiwa wizara inayohusika na mambo ya usalama wetu na mali zetu, si ujue tutakwisha wote tulio against their political wish??

Wasitubabaishe wala kutuzuga hawa, the guy is being held by a secret service somewhere and they are waiting for perfect time to strike him as they promised....

Kazi yetu sisi tuendelee kupaza sauti na kupiga kelele sana ili wasije kumfanya kitu mbaya ikiwemo kuutoa uhai wake kama si miongoni mwa zile maiti 8 za kule mto Ruvu zilizozikwa fasta fasta!!
 
Ndugu zanguni,

Hili jambo la kupotea kwa Ndg. Ben Saanane, kwa sasa huenda ndiyo Drama Kali zaidi Kisiasa na Kiusalama. Kwa binadamu yeyote lazima linapotokea jambo lisilo la kawaida kama hili ni lazima ajiulize maswali mengi kuwa inawezekana ni hivi au ni vile.

Katika kadhia hii, kuendana na mijadala inayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali watoa maoni wanaonekana kuamini kati ya mawili. Ben kutekwa na vyombo vya serikali kwa ajili ya 'kumshikisha adabu' au kutoa onyo kwa wakosoaji wengine au Ben kufichwa na Viongozi wa taasisi anayofanyia kazi ya CHADEMA kwa ajili ya kuionyesha dunia kuwa Serikali haitaki kukosolewa. Kwa maana ya kuipakazia serikali imemteka, lakini katika maudhui hiyo ya pili wapo wanaofikiri kuwa huenda alitofautiana na viongozi wake wakaamua kumfanyia 'Umafia'.

Dhania zote hizi zinaibuka kwa sababu tulio wengi hatujui kabisa ukweli wa jambo hili ukiacha waandaaji na watekelezaji wa jambo lenyewe, na Mungu aonaye sirini. Na huwezi kumzuia binadamu kuwaza sana sana aamue tu kutokuyatoa hadharani mawazo yake.

Katika kila kundi la dhania hapo juu ni lazima mtu yeyote wa kizazi cha kuhoji ajiulize maswali mengi kabla ya kuipa dhana yake asilimia kubwa zaidi ya nyingine.

Mimi nimepembua na kuchanganua na kujikuta nashawishika kuamini kuwa kupotea kwa Ndugu yetu Ben Saanane ndiyo haswa Operesheni UKUTA ambayo siku Mwenyekiti anatangaza kuiahirisha alisema itafanyika kivingine.

Nimejiuliza yafuatayo:

1. Kwa nini Ben!?
Je, Ben ndiye mtoa Kashfa na mkosoaji wa serikali kuliko wengine!? Mbona wengine walifunguliwa mashtaka ya makosa ya Mtandao!?

2. Kwa nini CHADEMA wanatumia nguvu kubwa ya kutaka kuuaminisha Umma kuwa Serikali imehusika na jambo hili badala ya kushirikiana na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi?

3. Kwa nini Mwajiri wake amekuwa na kigugumizi kuzungumzia sakata hili!?

4. Kama Taasisi hii hii iliweza kutengeneza mikakati ya kuwateka watu na kuwapa mateso makali kwa vile tu walitishia maslahi yao, watashindwaje kwa Ben!?

5. Hotuba ya Ndugu Mwenyekiti Mbowe huko ughaibuni aliyeelezea kuwa alilengwa na maguruneti na serikali ili atolewe uhai lakini watu waliompenda wakaamua kuwa ngao ili wafe badala yake.. (hotuba ile ilinishawishi nitamani kujua hatima ya uchunguzi wa ni nani aliyelipua lile bomu kule Arusha) nimejiuliza hili la Ben haliwezi kuwa ni maandalizi ya hotuba nyingine ughaibuni!?

Haya pamoja na mengine mengi yanayonizunguka kichwani yananishawishi niamini kuwa hii ndiyo operesheni UKUTA vol. 2, naomba kwa Mungu vyoyote iwavyo kijana huyu aliyetumika kama Starring kwenye Tamthiliya hii amalize salama, na arejee kuungana tena na familia yake, ndugu na marafiki zake katika kuchangia ujenzi wa nchi yake!!

Wakatabahu

Asim bip Mungu, atapotea kweli, ohoooo!!!
 
Hata baba'ke Ben amemtaka Mbowe aseme mwanawe alipo.

Unajua msinifanye niamini kuwa serikali pamoja na jeshi lake kubwa lenye jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao imeshindwa kujua Ben alipo...that's very fearful and terifying. kama kweli imeshindwa kupitia mafunzo yalokubuhu ya kiinterijensia kujua nani anahusika! then we are not safe anymore. kwangu mimi cha mhimu ni kujua nini kimempata Ben na nani mhusika wa hilo. yaani iwe chadema ama mtu mwingine amehusika katika hili bas serikali ama dola kwa ujumla wake wafanye kazi yao kujua ukweli. na kwa vile tumeshuhudia miili saba mto ruvu ikizikwa kinyama vile na pia kauli za wahusika kwamba ni wahamiaji haramu na mengine, inatia shaka kwa nia ya dola katika kuyapa kipaombele mambo yanayogusa maisha ya raia wake. naamini maisha ni zaidi ya itikadi za vyama maana leo yamempata Ben kesho huwezi jua nani yatampata kisa siasa.ningeweza kusema mengi ila ngoja tu niishie hapo tuu maana inatia kichefuchefu .
 
Exactly, this is the point!

Kama kweli serikali na vyombo vya uchunguzi vinajua kufanya kazi yake ipasavyo wamtafute Ben na kumrejesha awe yumo ndani ya nyumba ya Mbowe ama ktk ofisi za CHADEMA!

Unajua kuna watu wanataka kufanya watanzania ni watu wajinga sana kwamba wanaweza kuwageuza geuza kama chips za viazi zinavyokaangwa ktk flying pan....

Yaani serikali hii yenye fedha, TISS, Polisi, Secret Service, Magereza, JWTZ yaani ishindwe kutambua aliko Ben ama mtu yeyote aliyepotea!!??

Hakuna kitu hapo, hili ni jibu la moja kwa moja kuwa serikali yenyewe is responsible na sasa wanatumia mbinu zile zile zilizowahi kushindwa kwa kishindo kikuu miaka ya nyuma kwa kuihusisha CHADEMA ili sijui iweje.....

Soma maelezo ya Waziri anayehusika na ulinzi na usalama wa raia na mali zao aliyoyaandika yeye mwenyewe three or five days ago na kuyatupia humu utagundua mengi sana nyuma ya pazia ya utetezi binafsi wa mtu huyu...

Then, rejea historia yake ya nyuma huyu mtu ya siasa chafu huko, you will understand what I
mean!!

Halafu huyu huyu mtu kakabidhiwa wizara inayohusika na mambo ya usalama wetu na mali zetu, si ujue tutakwisha wote tulio against their political wish??

Wasitubabaishe wala kutuzuga hawa, the guy is being held by a secret service somewhere and they are waiting for perfect time to strike him as they promised....

Kazi yetu sisi tuendelee kupaza sauti na kupiga kelele sana ili wasije kumfanya kitu mbaya ikiwemo kuutoa uhai wake kama si miongoni mwa zile maiti 8 za kule mto Ruvu zilizozikwa fasta fasta!!
Tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani, nilijua mambo lazima yaende mrama.

Pengine mteuzi wake mwenye allergy na upinzani alimtea kutokana na kazi 'nzuri' aliyoifanya Arusha.

Lakini kwenye issue ya Ben namtupia Mbowe lawama zote kwa 100%,....kwanini hadi wakati huu hajaitisha maandamano ya kumtaka Ben akiwa hai?
Propaganda kama za huyu mleta mada zinataka kuwaziba wapinzani wasiandamane kumdai Ben.

Ben yupo kwenye orodha ya viongozi wa upinzani, amepotea na haijulikani aliko, hivyo viongozi waliobaki wanatakiwa waishinikize serikali kwa namna yoyote ile hadi Ben apatikane.

Hata kama Ben yupo ndani kwa Mbowe, bado Mbowe anayao haki ya kuishinikiza serikali imtafute Ben maana ina nyenzo zote za kufanya hivyo.
Ben ni kiongozi wa upinzani wa pili baada ya Mawazo kukumbana na dhahama kwenye awamu ya tano lakini CDM hawaoneshi shinikizo lolote,......kweli upinzania Tanzania bado mnoo.
 
Unajua msinifanye niamini kuwa serikali pamoja na jeshi lake kubwa lenye jukumu la kulinda usalama wa raia na mali zao imeshindwa kujua Ben alipo...that's very fearful and terifying. kama kweli imeshindwa kupitia mafunzo yalokubuhu ya kiinterijensia kujua nani anahusika! then we are not safe anymore. kwangu mimi cha mhimu ni kujua nini kimempata Ben na nani mhusika wa hilo. yaani iwe chadema ama mtu mwingine amehusika katika hili bas serikali ama dola kwa ujumla wake wafanye kazi yao kujua ukweli. na kwa vile tumeshuhudia miili saba mto ruvu ikizikwa kinyama vile na pia kauli za wahusika kwamba ni wahamiaji haramu na mengine, inatia shaka kwa nia ya dola katika kuyapa kipaombele mambo yanayogusa maisha ya raia wake. naamini maisha ni zaidi ya itikadi za vyama maana leo yamempata Ben kesho huwezi jua nani yatampata kisa siasa.ningeweza kusema mengi ila ngoja tu niishie hapo tuu maana inatia kichefuchefu .

Serikali ni wewe pia, au wewe si serikali? Unajuwa alipo?

Mbowe ambae ni muajiri wa Ben mbona hamumuulizi yuko wapi Ben?
 
Back
Top Bottom