Nina Mashaka sana kuwa kupotea kwa Ben Saanane ndiyo operesheni UKUTA

Dec 10, 2016
27
45
Ndugu zanguni,

Hili jambo la kupotea kwa Ndg. Ben Saanane, kwa sasa huenda ndiyo Drama Kali zaidi Kisiasa na Kiusalama. Kwa binadamu yeyote lazima linapotokea jambo lisilo la kawaida kama hili ni lazima ajiulize maswali mengi kuwa inawezekana ni hivi au ni vile.

Katika kadhia hii, kuendana na mijadala inayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali watoa maoni wanaonekana kuamini kati ya mawili. Ben kutekwa na vyombo vya serikali kwa ajili ya 'kumshikisha adabu' au kutoa onyo kwa wakosoaji wengine au Ben kufichwa na Viongozi wa taasisi anayofanyia kazi ya CHADEMA kwa ajili ya kuionyesha dunia kuwa Serikali haitaki kukosolewa. Kwa maana ya kuipakazia serikali imemteka, lakini katika maudhui hiyo ya pili wapo wanaofikiri kuwa huenda alitofautiana na viongozi wake wakaamua kumfanyia 'Umafia'.

Dhania zote hizi zinaibuka kwa sababu tulio wengi hatujui kabisa ukweli wa jambo hili ukiacha waandaaji na watekelezaji wa jambo lenyewe, na Mungu aonaye sirini. Na huwezi kumzuia binadamu kuwaza sana sana aamue tu kutokuyatoa hadharani mawazo yake.

Katika kila kundi la dhania hapo juu ni lazima mtu yeyote wa kizazi cha kuhoji ajiulize maswali mengi kabla ya kuipa dhana yake asilimia kubwa zaidi ya nyingine.

Mimi nimepembua na kuchanganua na kujikuta nashawishika kuamini kuwa kupotea kwa Ndugu yetu Ben Saanane ndiyo haswa Operesheni UKUTA ambayo siku Mwenyekiti anatangaza kuiahirisha alisema itafanyika kivingine.

Nimejiuliza yafuatayo:

1. Kwa nini Ben!?
Je, Ben ndiye mtoa Kashfa na mkosoaji wa serikali kuliko wengine!? Mbona wengine walifunguliwa mashtaka ya makosa ya Mtandao!?

2. Kwa nini CHADEMA wanatumia nguvu kubwa ya kutaka kuuaminisha Umma kuwa Serikali imehusika na jambo hili badala ya kushirikiana na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi?

3. Kwa nini Mwajiri wake amekuwa na kigugumizi kuzungumzia sakata hili!?

4. Kama Taasisi hii hii iliweza kutengeneza mikakati ya kuwateka watu na kuwapa mateso makali kwa vile tu walitishia maslahi yao, watashindwaje kwa Ben!?

5. Hotuba ya Ndugu Mwenyekiti Mbowe huko ughaibuni aliyeelezea kuwa alilengwa na maguruneti na serikali ili atolewe uhai lakini watu waliompenda wakaamua kuwa ngao ili wafe badala yake.. (hotuba ile ilinishawishi nitamani kujua hatima ya uchunguzi wa ni nani aliyelipua lile bomu kule Arusha) nimejiuliza hili la Ben haliwezi kuwa ni maandalizi ya hotuba nyingine ughaibuni!?

Haya pamoja na mengine mengi yanayonizunguka kichwani yananishawishi niamini kuwa hii ndiyo operesheni UKUTA vol. 2, naomba kwa Mungu vyoyote iwavyo kijana huyu aliyetumika kama Starring kwenye Tamthiliya hii amalize salama, na arejee kuungana tena na familia yake, ndugu na marafiki zake katika kuchangia ujenzi wa nchi yake!!

Wakatabahu
 
Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,000
Umefikiria vizuri sana mkuu....Pia unaweza fikiri zaidi nje ya BOX na kusema ya kuwa TAASISI YAKE NDIO ilikuwa inamtumia VIBAYA kutoa kashfa kwa MKUU WA NCHI ili hali wao wana lao jambo juu ya BEN....ILI mwisho wa siku baya lolote litakalo mtokea BEN ionekane ni serikali ndio imehusika.....SASA kibaya zaidi hii MISSION YA CHADEMA IMEBUMA tuliowengi tunawanyooshea VIDOLE wao juu ya UPOTEVU WA HUYU KIJANA....ndio maana hata viongozi wao wanabaki kubwabwaja juu ya hili jambo.......
 
Hili ni miongoni mwa mengi ya kufikirisha.. Time will tell
 
Macos

JF-Expert Member
May 12, 2008
1,934
2,000
Umefikiria vizuri sana mkuu....Pia unaweza fikiri zaidi nje ya BOX na kusema ya kuwa TAASISI YAKE NDIO ilikuwa inamtumia VIBAYA kutoa kashfa kwa MKUU WA NCHI ili hali wao wana lao jambo juu ya BEN....ILI mwisho wa siku baya lolote litakalo mtokea BEN ionekane ni serikali ndio imehusika.....SASA kibaya zaidi hii MISSION YA CHADEMA IMEBUMA tuliowengi tunawanyooshea VIDOLE wao juu ya UPOTEVU WA HUYU KIJANA....ndio maana hata viongozi wao wanabaki kubwabwaja juu ya hili jambo.......
Wewe unagikiri infekua chadema wanajua na serikali haijui chochote pangekalika hapa, sio ndio ingekua nafasi ya prpopaganda ? Hapa kuna mchezo. , ila time will tell nani anahusika, . Mfano sasa hivi mada zake kutoka facebook zimefutwa zile za october. Kama serikali inataka kujua ni nani anayo acess ya FB basi infeomba mahakama kuiomba FB itoe ushirikiano kujua location ya mwisho ilikua wapi na ip address ilotumika wakati wa kufuta mada hizo.
 
Milindi

JF-Expert Member
Mar 3, 2009
1,332
2,000
Alikuwa ni rafiki yangu! Watoto wangu wanamfahamu vizuri! Tulikuwa tunawasiliana.........
1.Mheshimiwa waziri je alikuwa akikuambia hata siri za Mbowe?
2.Je alikuwa ni pandikizi?
3.Mheshimiwa waziri Ben alitishiwa na akakueleza ulichukua hatua gani kumlinda?
Maswali ni mengi kuliko majibu.Only God knows! Lets wait until the end!
It seemed that we are using the same method as used by 2K of east africa!
 
Kazwala mkuu

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,012
2,000
Siasa ni mchezo mchafu n a ina mengi mabaya katika giza ili kuonyesha mema adharani, sijawahi kuwa mfia chama chochote cha siasa sababu sipendi kufanywa zuzu, lolote linawezekana kwa kijana wetu na linaweza kutokea upande wowote kwa maslahi yao.
 
gogo la shamba

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
6,674
2,000
Ndugu zanguni,

Hili jambo la kupotea kwa Ndg. Ben Saanane, kwa sasa huenda ndiyo Drama Kali zaidi Kisiasa na Kiusalama. Kwa binadamu yeyote lazima linapotokea jambo lisilo la kawaida kama hili ni lazima ajiulize maswali mengi kuwa inawezekana ni hivi au ni vile.

Katika kadhia hii, kuendana na mijadala inayoendelea kwenye majukwaa mbalimbali watoa maoni wanaonekana kuamini kati ya mawili. Ben kutekwa na vyombo vya serikali kwa ajili ya 'kumshikisha adabu' au kutoa onyo kwa wakosoaji wengine au Ben kufichwa na Viongozi wa taasisi anayofanyia kazi ya CHADEMA kwa ajili ya kuionyesha dunia kuwa Serikali haitaki kukosolewa. Kwa maana ya kuipakazia serikali imemteka, lakini katika maudhui hiyo ya pili wapo wanaofikiri kuwa huenda alitofautiana na viongozi wake wakaamua kumfanyia 'Umafia'.

Dhania zote hizi zinaibuka kwa sababu tulio wengi hatujui kabisa ukweli wa jambo hili ukiacha waandaaji na watekelezaji wa jambo lenyewe, na Mungu aonaye sirini. Na huwezi kumzuia binadamu kuwaza sana sana aamue tu kutokuyatoa hadharani mawazo yake.

Katika kila kundi la dhania hapo juu ni lazima mtu yeyote wa kizazi cha kuhoji ajiulize maswali mengi kabla ya kuipa dhana yake asilimia kubwa zaidi ya nyingine.

Mimi nimepembua na kuchanganua na kujikuta nashawishika kuamini kuwa kupotea kwa Ndugu yetu Ben Saanane ndiyo haswa Operesheni UKUTA ambayo siku Mwenyekiti anatangaza kuiahirisha alisema itafanyika kivingine.

Nimejiuliza yafuatayo:

1. Kwa nini Ben!?
Je, Ben ndiye mtoa Kashfa na mkosoaji wa serikali kuliko wengine!? Mbona wengine walifunguliwa mashtaka ya makosa ya Mtandao!?

2. Kwa nini CHADEMA wanatumia nguvu kubwa ya kutaka kuuaminisha Umma kuwa Serikali imehusika na jambo hili badala ya kushirikiana na vyombo vya usalama kufanya uchunguzi?

3. Kwa nini Mwajiri wake amekuwa na kigugumizi kuzungumzia sakata hili!?

4. Kama Taasisi hii hii iliweza kutengeneza mikakati ya kuwateka watu na kuwapa mateso makali kwa vile tu walitishia maslahi yao, watashindwaje kwa Ben!?

5. Hotuba ya Ndugu Mwenyekiti Mbowe huko ughaibuni aliyeelezea kuwa alilengwa na maguruneti na serikali ili atolewe uhai lakini watu waliompenda wakaamua kuwa ngao ili wafe badala yake.. (hotuba ile ilinishawishi nitamani kujua hatima ya uchunguzi wa ni nani aliyelipua lile bomu kule Arusha) nimejiuliza hili la Ben haliwezi kuwa ni maandalizi ya hotuba nyingine ughaibuni!?

Haya pamoja na mengine mengi yanayonizunguka kichwani yananishawishi niamini kuwa hii ndiyo operesheni UKUTA vol. 2, naomba kwa Mungu vyoyote iwavyo kijana huyu aliyetumika kama Starring kwenye Tamthiliya hii amalize salama, na arejee kuungana tena na familia yake, ndugu na marafiki zake katika kuchangia ujenzi wa nchi yake!!

Wakatabahu
hata kwa Mwangosi ulisema hayohayo kwamba,kilichomuua Mwangosi kilitupwa kutoka katika kundi la wafuasi wa chadema,lakini picha zikakuumbua
 
Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,044
2,000
Duh yaani kweli MTU Unaweza ukajenga theory za kijinga hivi?? Ccm wanahusika kwa namna yoyote ile iwayo na mhusika mkuu alishatajwa hapa na akaja kutuzuga. Mbona Iko wazi tu??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom