Nina mashaka na uwezo wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina mashaka na uwezo wa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Jul 25, 2012.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Msomi Mh. Waziri wa Mawasiliano, sayansi na Teknolojia kashindwa kabisa si tu kuwakumbuka Wabunge bali hata kusoma toka kwenye karatasi yake majina yao. Je huyu anawezaje kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia nchini?

  Baadaye katika kujibu ilifikia kipindi akasema, "Silvesta Mapumbu, oh! samahani Mabumbu" LOL!!!:yawn:

  Je ni kupaniki au ni uwezo mdogo au ni kusoma kupitiliza hadi kuchanganyikiwa?
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kujua kusoma vizuri majina hakuna uhusiano na uwezo wa kufikiri na kutenda.
   
 3. rfjt

  rfjt Senior Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nimegundua mawaziri wengi hawawezi kusoma kwa usahihi. Sijui wanawezaje kuleta tija kwa ufanisi katika nafasi zao.

  Serikali ya awali hii tunaona mengi ya kushangaza...!!!!
   
 4. suleym

  suleym JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,716
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  huyu waziri ni janga, hata anavyojibu 2 inaonesha ni hakuna ki2, heb mlinganishe na naibu wake makamba jr. alivyokuwa anajibu hoja za wabunge. wazir hawez kujieleza had asome kile 2 alichoandikiwa.
   
 5. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli sijui ni vigezo gani vinatumika kuwateua hawa Mawaziri!!Huyu profesa Mbarawa ameonyesha mapungufu na udhaifu mkubwa sana katika kujibu hoja za wabunge waliotoa michango yao ktk Wizara yake tofauti kabisa na Naibu Waziri wake Mh.Makamba ambae kwa kweli nampongeza kwa uwezo mkubwa wakujibu hoja nakutoa ufafanuzi wakuridhisha.

  Mapungufu yake:

  1.Anakosea sana kusoma kutokana nakutojiamini nakutetemeka.
  2.Anasoma kila kitu kwenye karatasi.
  3.Anaonyesha kabisa hata majibu anayotoa hana uhakika nayo coz ameandikiwa tu.
   
 6. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hamna kitu hapo
   
 7. m

  magohe JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  pengine hajakulia nchi hii kwani hata kutaja majina ya wtz wenzake hawezi au katokea ughaibuni nini?
   
 8. Wilbert1974

  Wilbert1974 JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 1,607
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hata kusoma majina ya kawaida kabisa yanamchanganya jamani!
  Ongezea ulivyomsikia nawe?
   
 9. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Acha suala la kutenda ambalo tunasubiri tuone: Je una uhakika hakuna uhusiano kati ya kusoma na kufikiri? Toa somo hapa tukuelewe; ili mtu aweze kusoma ni nini kinatokea katika mwili na viungo vyake.

  Unajua hapa sisemei mtu kukosea majina matano-sita tu yaani karibu 80% ya majina yote anakosea vibaya na mengine si majina magumu kuyasoma. Pili badala ya Tuzo anasema Tunzo wakati wote, tatu mtu akimpelekea ki- note anaacha anachosoma kwa ghafla na kusoma alicholetewa. Jamani watu wanakutathimini kufuatana na mambo mengi sana!
   
 10. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli hata mimi amenishangaza na anaendelea kunishangaza!!Utekelezaji mzuri wa jambo lolote unatokana na uelewa wa mtu katika sekta husika sasa huyu waziri anayesoma kila kitu tena kwakutetemeka namakosa mengi unaweza kusema anauelewa kweli kuhusiana hii Wizara yake!!
   
 11. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0

  CCM tunajimaliza wenyewe. Unaibu waziri umepewa juzi. Leo umeanza majungu kwa bosi wako. Kijana January Marope punguza majungu. Hauna tofauti na Zitto. Wote manafiki

  Umepiga majungu Ikulu, ukampiga Ngeleja hadi katolewa, leo kwa bosi wako. Kha
   
 12. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  atakuwa ni wale wasomea GPA aka STUDY HARD GET GOOD GRADES GET GOOD JOB
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Kama jamaa ana PHD basi hakuna kosa hapo bali kisomo ndo kimemfikisha hapo.
  WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
   
 14. m

  mzee wa busara Senior Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 161
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  teh teh teh,hii kali katamka Silvesta Mapumbu? Kweli Bunge ni zaidi ya The commedy ya kina Masanja,kila burudani utaipata mjengoni.
   
 15. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Acha kutumia Masaburi wewe nadhani unifahamu...kwanza sipo chama cha magamba na kamwe siwezi kuwa magamba afu pia yawezekana hufuatilii bunge ndomana unaongea haya.
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  As long as ni mwanachama wa thithiemu, sishangai kwani ndege wanaofanana hupaa pamoja. Ukimshangaa huyo, alomteua je?
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..inawezekana hana uzoefu na mambo ya public speaking.

  ..kwa uelewa wangu jamaa ana PhD, amesoma ktk nchi zaidi ya moja, na amefanya kazi ndani na nje ya Tanzania.
   
 18. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nafikiri kujua kupiga longolongo bungeni si kwamba wewe ndo mtaalam. huyo waziri nimemuona, ndiyo anakosea kusoma majina na kumbuka huyu yuko kiutendaji zaidi na siyo kisiasa zaidi, ndo maana JK hawezi kuwaondoa watu kama hao bali anawaongeza kama vile prof muhongo wa nishati na madini.
  mimi ni mwanasayansi na mtafiti, kwangu ni matokeo zaidi ndo nahitaji na wala si longolongo za kisiasa. jamaa toka aende pale wizara ya sayansi vitu vinasonga na bahati mbaya watu wengi ni mangwini hapa tz sayansi kwao zero, hivyo wizara kama ya sayansi ambayo iko more technical hawawezi kujua inafanya nini.
   
 19. b

  bob giza JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  skieni nyie mapoyoyo..ivi kwann mnakuwa na dhana kuwa anayeweza kupiga domo mbele ya watu na kujieleza ndiye kiongozi mzuri??ivi nyie wabongo mmerogwa eehh??uongozi mzuri sio kujua kujieleza mbele za watu..zama izo kwishnei tunaangalia performance..mngesema prof kachemsha kwenye ufuastiliaji wa masuala ya msingi pale wizarani tungeelewa..,mmekalia ooh hajui mara sio kiongozi mzuri acheni ushamba wenu..yule ni mwanasayansi na sio sociologist au sijui yeyote mnayedhani..wizara ya sayansi akipewa sociologist mnapiga kelele ooohh hajui leo kapewa mwanasayansi mnapiga kelele kisa kakosea kutaja jina..wee bwana ni mweupe kabisa kichwani kwako..na ndo maana linchi hili haliendelei kwa sababu ya watu kama wewe ambao hutumia vigezo rahisi rahisi kumpima mtu..acheni upumbavu sawa
   
 20. b

  bob giza JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wee chizi yule mwanasayansi na sio msoma taarifa ya habari tbc au itv sawa..yule ni prof wa sayansi alobobea na kaongoza idara nyeti za kimataifa zenye uzito kuliko huo uwaziri wenu sijui wa nn na nn...uwe na heshima kwa prof wee chizi ivi kwa akili yako unadhani unawezakuwa na uwezo kuliko yeye kwa sababu anakosea kusoma majina??
  mind yako ni very simple...yaani unaongelea vitu vidogo vidogooo...**** wewe
   
Loading...