Baada ya kukaa kwa muda nikizunguka maeneo mbali mbali ya Tanzania, nimeona kuna ombwe kubwa sana la uwezo wa kufikiri ndani ya jamii yetu na uwezo huo umegawanyika katika makundi makuu matatu.
1. Masuala ya kiuchumi
2. Masuala ya kijamii
3. Masuala ya kisiasa
1. MASUALA YA KIUCHUMI
Katika hili ambalo ndo msingi wa hayo mengine watanzania wana uwezo mdogo wa kuona fursa zinazowazunguka, uwezo mdogo wa kutafuta, na kutaka kupata habari za kiuchumi, uwezo mdogo wa kutumia rasilimali za nchi yetu kwa hili wageni wanatushangaa.
Achilia mbali serikali ambayo tunaitupia lawama kila kukicha lakini watanzania wengi tunatafuta mchawi wa kumlaumu kwa kila kitu, utakuta mtu kama hajasoma analaumu wazazi au ndungu na hiyo inakuwa sababu tosha ya kukaa na kubweteka.
Kama amesoma anaitafuta serikali na kiulaumu na hiyo inakuwa sababu ya kupata kisingizio.
Ukimwuliza bei ya shamba hajui, bei ya kuku hajui, bei ya mazao, hajui bei ya vitu vya kimaendeleo, ila mwulize Rihanna na Mess anakutajia mpaka aina ya chakula wanachokula anajua historia ya team zaidi ya anavyowaza maendeleo yake biunafsi.
Mbaya zaidi hata mawazo ya nini afanye hana, anasubiri pesa ambazo hata hajui zitatoka wapi.
Ni vema watafiti wa akili wakaangalia kama njaa ya mwaka 1994 na miaka iliyofuata kama ilisababisha madhara kwenye ubongo wetu, au mlo usiotosheleza ndio sababu maana hali inatisha saana yaani mtu anafuga ng'ombe na analima bila mbolea ya samadi.
Kijiji kizima kinakosa kuku au bata wa kununua, kijiji ukitaka nyama unasafiri na wakati kuna mahitaji ya nyama ila watu wanalia umasikini.
Hata kama Magufuli akipiga kelele kama ujinga haujatoka kwenye vichwa vya watanzania hakuna kitu kitakachofanyika yaani kutakuwa na afya, maji, shule
ila hakuna maendeleo kwa jamii iliyokubwa kwa sababu ya ubongo mgando
mpaka sasa ni wananchi wachache wanaofanya kilimo kwa kupiga hesabu ya faida na hasara.
Sasa mtu asiyejua faida na hasara kwa namba unategemea aendelee yeye ni wa kuamka na kwenda kazini na jioni kurudi hajui ameingiza au ametoa.
2. MASUALA YA KIJAMII
Jamii ya watanzania bado inaigiza linapokuja masuala ya afya, elimu na masuala ya maisha ndani ya jamii. Ni jamii ambayo mara zote inatafuta short cut au majibu rahisi kwa maswali magumu.
Ndio maana utashangaa ikifika muda wa kupeleka mtoto shule baba anakosa shilingi elfu 5000 za sare na daftari, hayo ni matokeo ya kutokujitambua na kuto kujua wajibu.Yaani mtoto anazaliwa anakua mpaka muda wa kwenda shule alafu familia inakosa viatu. Wakati huo huo kuku kijijini ni shilingi elfu 10, hiyo ndo jamii kubwa tuliyonayo Tanzania.
Jamii ambayo inaishi kimungu Mungu kirejareja bila mipango wala malengo ni jamii kubwa ya wapenda simulizi tamu kama ambavyo wanapenda sasa hadithi za majipu kuliko kuhoji na kuchambua.
3. MASUALA YA KISIASA
Jamii haijui nini mchango wa siasa na nini siyo mchango wa siasa kwenye maisha ya mtu mmoja mmoja na hilo ndilo limekuwa mtaji wa wanasiasa wa kuhadaa uma kwa kujificha kwenye huu ujinga totoro.
Jamii inaamini na imeaminishwa propaganda kama hizi, serikali ni kila kitu mpaka ukikosa sabuni ya kuogea serikali inahusika.
Serikali ina solution za kila tatizo la mwananchi, chama fulani au kundi fulani ndio chanzo cha matatizo yote uliyonayo hata kama mengine yamesababishwa na uzembe wako mwenyewe. Kwa mfano mtu kabisa kapelekwa shule tena private hata kama ni ya kata halafu kazi yake ni kamari, akifeli analaumu serikali kwamba kwa nini haikumbana kubaki darasani halafu ikimbana anakuja na kusema kila mtu ana haki ya kuchagua nini afanye.
Matatizo yoote yataisha kama chama fulani kikipewa madaraka tena au chama kipya kikipata madaraka hata yale ambayo ni juhudi za mtu kuyatoa.
Kwa ule uwezo duni wa kufikiri, hawafikirii kwamba mbona chama hicho kilipewa kuongoza muda mrefu na kikashindwa vibaya. Au kwa nini chama kipya tunachokisema kilipata viti vya wabunge na bado maisha hayakubadillika.
Hawajui kwamba matatizo ya nchi ni zaidi ya tatizo la chama. Matatizo ya maisha magumu ni matokeo ya maamuzi yako kwa kiwango kikubwa kuliko ya serikali na chama.
Kwa uwezo huo kazi bado tunayo, wanasiasa wataendelea kuneemeka kwa sababu matatizo yetu ni mtaji kwao.
Kama isipofika watanzania kuwa na roho ya uwajibikaji binafsi kwa ajili ya maisha ya kila mmoja mmoja bila kulalamika basi wanasiasa watakuwa wanatuchezea akili kama ambavyo wanaendelea kufanya.