Nina Mashaka na Upadri wa Dr. Slaa

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Kwa wasomaji wa maandiko wanakumbuka tukio moja la Yesu kristo pale waandishi na mafarisayo walipomtuhumu kwamba imekuwaje Yeye kula na kujichanganya na wenye dhambi, wakiwemo watoza ushuru waliotuhumiwa kwa kula rushwa ( sawa na TRA hapa TZ. ila TRA sio wala rushwa). Yesu kristo aliwajibu kwamba waliowazima hawahitaji daktari.

Dr. Slaa amedai kwamba Chadema aliyoijenga ni ya waadilifu. Kwa maana hiyo, kwa falsafa ya Yesu kristo, Dr. Slaa alipasa kumpokea Edward Lowassa na kisha amwadilishe. Tofauti na mafundisho ya kanisa katoliki, Dr. Slaa anawakimbia wenye dhambi kisha anasimama majukwaani akiwatuhumu wenye dhambi hao.

Aidha, Dr. Slaa ameonesha kuwa mwongo kabisa. Amehusisha suala la ubomomoaji wa mabucha ya nguruwe na uvamizi wa polisi ndani ya msikiti wa Mwembechai (1999) na Mh. Sumaye. Kwa kumbukumbu zangu,(niko tayari kusahihishwa) miaka ile Rais wa Tanzania alikuwa Mzee Mwinyi na kipindi hicho Mh. Sumaye hakuwa Waziri Mkuu.

Lakini pia, kitendo cha Dr. Slaa kuingiza udini katika hoja zake pale Serena Hotel juzi, hakutumia hekima. Ameongea kwamba eti wachungaji na maaskofu 30 wamehongwa na Mh. Lowassa; akaenda mbali zaidi akisema eti hata kanisa la KKKT liko nyuma ya Lowassa. Kauli hizi ni hatari mno, hazipaswi kuachwa pasipo kukemewa.

Yamkini, labda, ni mkakati wa makusudi kutumia dini ili kumbomoa Mh. Lowassa kwa maana siku tatu kabla ya Dr. Slaa kujitokeza pale Serena Hotel, ndugu Mpanju naye alisikika huko mkoani Njombe akimnadi mgombea urais wa CCM; akisema Masheikh wa Zanzibar ambao wako mahabusu Segerea walihusika na mauaji ya Padri kule Zanzibar lakini pia akasema eti masheikh hao walihusika na uchomaji wa makanisa kule Mbagala.

Kauli za jinsi hii, kama hiyo ya ndugu Mpanju, haikustahili kusemwa kwa kuwa kesi ya masheikh hao ingali mahakamani na ni mahakama ambayo inaweza kuthibitisha uhusika wa masheikh hao na tuhuma hizo juu yao.

Tuongee yote majukwaani lakini tuchunge ndimi zetu. Hata kama tumedhamiria kwa dhati kuwafurahisha mabwana zetu, kwa kusema kile tudhaniacho kina (kita) wapendeza na kuwafurahisha; tusiingize kauli zinazoweza chochea uvunjifu wa amani kiimani.
 
Padre ana wake kadhaa...wengine wamemuanika Leo alivyotelekeza familia,nasikia kuna masista wanafata
 
Ninyi team EL acheni kuweweseka.

Jibuni hoja za Dr kwa hoja na si vihoja, Nitaendelea kumheshim mtu huyu hata kama ametofautiana na msimamo wa chama. Kazi aliyoifanya kukifikisha chama hapa kilipo haina mfanowe.
 
Kweli nimechoka kabisa...mwanaume umekuwa unamwita mwanamke kahaba hadharani kwa zaidi ya miaka saba...umeapa mbele ya hadhara kuwa katu kamwe huwezi kushiriki naye au kumuoa...leo mshenga anakuja na kukuambia yule mwanamke kavunja ndoa yake ya awali na anataka kushiriki na wewe vipi nikuunganishie...unakubali ila unatoa sharti kuwa aje amevaa gold na silver nitampoke....hii imenitatiza sana...
 
Ninyi team EL acheni kuweweseka.

Jibuni hoja za Dr kwa hoja na si vihoja, Nitaendelea kumheshim mtu huyu hata kama ametofautiana na msimamo wa chama. Kazi aliyoifanya kukifikisha chama hapa kilipo haina mfanowe.

Kaongea upuuzi,hana hoja
 
Lowasa awe fisad au asiwe fisadi...mm ni mabadiliko tu...nataka kuonyesha dunia kuwa tz kuna vyama vingi ......lowasa mbele.
 
Ninyi team EL acheni kuweweseka.

Jibuni hoja za Dr kwa hoja na si vihoja, Nitaendelea kumheshim mtu huyu hata kama ametofautiana na msimamo wa chama. Kazi aliyoifanya kukifikisha chama hapa kilipo haina mfanowe.

Tutakujibu Novemba
Sasa hivi majibu yetu ni
Elimu bora
Kilimo
Afya
Nidhamu na uwajibikaji
Mawasiliano
 
Hivi nawezaje kuona dhambi ya wizi, rushwa kwa mwenzangu, wakati dhambi ya uzinifu, uongo, uzushi, matusi, ulaghai, uuaji iliyo kwangu siioni?.

Wenye dhambi wote ikiwepo wazinifu, waongo,wezi, matapeli, wapotoshaji nk wote Mungu atawahukumu na sehemu yako ni ziwa liwakalo moto milele na milele. Hawana nafasi kwenye ufalme wa Mungu

Kila dhambi afanyayo binadamu ikiwepo ufisadi, wizi, ulevu anafanya nje ya mwili wake lakini aziniye, huzini juu ya mwili wake mwenyewe
Yesu akasema "sleeping with another man's wife will cost you your life". Methali 6:26

Yesu akasema "Anyone who sleeps with another one mans one will be severely punished by HIM" Methali 6:29

Yesu anatuasa tuache dhambi zetu zote tumrudie yeye leo. Tusipotubu siku ya mwisho tutachomwa milele. Nawashauri wote mmpokee YESU na muache dhambi zenu zote. Dhambi zote ni mbaya, uzinzi ni mbaya zaidi, hebu kila atafakari leo na kumrudia YESU Kristo, kabla ya kufa kwake. Huwezi kujua umebakisha masaa mangapi kuishi. Inaweza ikawa leo ndio siku yako ya mwisho

Yesu akasema itanifaa niipate ulimwengu wote, na kupoteza nafsi yangu jehanamu ya moto?
 
Kwa wasomaji wa maandiko wanakumbuka tukio moja la Yesu kristo pale waandishi na mafarisayo walipomtuhumu kwamba imekuwaje Yeye kula na kujichanganya na wenye dhambi, wakiwemo watoza ushuru waliotuhumiwa kwa kula rushwa ( sawa na TRA hapa TZ. ila TRA sio wala rushwa). Yesu kristo aliwajibu kwamba waliowazima hawahitaji daktari.

Dr. Slaa amedai kwamba Chadema aliyoijenga ni ya waadilifu. Kwa maana hiyo, kwa falsafa ya Yesu kristo, Dr. Slaa alipasa kumpokea Edward Lowassa na kisha amwadilishe. Tofauti na mafundisho ya kanisa katoliki, Dr. Slaa anawakimbia wenye dhambi kisha anasimama majukwaani akiwatuhumu wenye dhambi hao.

Aidha, Dr. Slaa ameonesha kuwa mwongo kabisa. Amehusisha suala la ubomomoaji wa mabucha ya nguruwe na uvamizi wa polisi ndani ya msikiti wa Mwembechai (1999) na Mh. Sumaye. Kwa kumbukumbu zangu,(niko tayari kusahihishwa) miaka ile Rais wa Tanzania alikuwa Mzee Mwinyi na kipindi hicho Mh. Sumaye hakuwa Waziri Mkuu.

Lakini pia, kitendo cha Dr. Slaa kuingiza udini katika hoja zake pale Serena Hotel juzi, hakutumia hekima. Ameongea kwamba eti wachungaji na maaskofu 30 wamehongwa na Mh. Lowassa; akaenda mbali zaidi akisema eti hata kanisa la KKKT liko nyuma ya Lowassa. Kauli hizi ni hatari mno, hazipaswi kuachwa pasipo kukemewa.

Yamkini, labda, ni mkakati wa makusudi kutumia dini ili kumbomoa Mh. Lowassa kwa maana siku tatu kabla ya Dr. Slaa kujitokeza pale Serena Hotel, ndugu Mpanju naye alisikika huko mkoani Njombe akimnadi mgombea urais wa CCM; akisema Masheikh wa Zanzibar ambao wako mahabusu Segerea walihusika na mauaji ya Padri kule Zanzibar lakini pia akasema eti masheikh hao walihusika na uchomaji wa makanisa kule Mbagala.

Kauli za jinsi hii, kama hiyo ya ndugu Mpanju, haikustahili kusemwa kwa kuwa kesi ya masheikh hao ingali mahakamani na ni mahakama ambayo inaweza kuthibitisha uhusika wa masheikh hao na tuhuma hizo juu yao.

Tuongee yote majukwaani lakini tuchunge ndimi zetu. Hata kama tumedhamiria kwa dhati kuwafurahisha mabwana zetu, kwa kusema kile tudhaniacho kina (kita) wapendeza na kuwafurahisha; tusiingize kauli zinazoweza chochea uvunjifu wa amani kiimani.

Slaa ni Dokta sio padri ....... Alishaachana na upadri miaka 20 iliyopita
 
Dr.Slaa alijenga chama kwa tamaa ya madaraka, mbona mwanzilishi wa chana Edwin Mtei amekaa kimya, ? Babu kazeeka huyu ngozi imejikunja huku bado anakuwa Na wanawake! Atubu Na aombe Msamaha, kwanza ana laana kwani alikimbia Upadre.
 
Back
Top Bottom