nahavache
JF-Expert Member
- Apr 3, 2009
- 871
- 246
Kwa sababu huwezi hata siku moja kusifu mawazo ya Mbowe, basi utaendelea kupinga. Safari ya Mbowe na wabunge wote wa CHADEMA Arusha ni ya muhimu sana kuliko hata hilo bunge. Pale bungeni hoja za upinzani hata siku moja zinapingwa na hivyo hata wao kukaa pale ni jambo la kupoteza muda. Hivi ushaona wapi mchango wa wabunge wa maana ukabadilisha au ukaboresha bajeti ya serekali? Au unataka uendelee kudanganywa kuwa tumeongeza hela kwenye bajeti ya maji alafu mwaka unapita hela iliyotengwa kwa ajili ya wizara ya maji imetolewa chini ya 50%.
Bomu limetokea wakati wa mkutano wa CHADEMA na hivyo wabunge wa CHADEMA lazima waonyeshe solidarity na sympathy kwa watu wa Arusha. Au unadhani hao waliofariki si wamaana kuliko wale waliofariki kule Mtwara wakati bajeti ya wizara ya madini na nishati ikisomwa?
MImi kwa kweli nina mashaka na uzalendo wako pamoja na fikira zako