Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,395
Sikutegemea uamuzi mbovu kama huu unaweza kufanywa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni-KUB ya kuwalazimisha wabunge wote wa CHADEMA wasitishe kuhudhuria vikao vya bunge la bajeti vinavyo endelea na kwenda jijini Arusha kuhudhuria maziko ya wananchi waliofariki kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea kwenye Mkutano wa CHADEMA.
Kuna haja gani ya wabunge wote kwenda Arusha na kukaa kusubiria maziko ambayo hayaeleweki yanafanyika lini?? Bila shaka huu ni mtaji wa kisiasa unatafutwa kupitia vifo vya watanzania wenzetu. Mh Mbowe yawezekana kasahau kabisa kazi ya Kambi ya Upinzania Bungeni-KUB?? Au ndiyo kusema wenzetu mmelidhishwa na bajeti hii iiyosomwa bungeni?? Kwa hili sisiti kutamka wazi wazi huu uamuzi ni wa kipuuzi na hauna tija kabisa mbele ya watanzania, waacheni wabunge wafanye kazi zao za kibunge kwa kuhakikisha wanawatetea na kuwatumikia watanzania waliowapa fursa ya kuingia bungeni.
KWA HAYA NAANZA KUONA UMUHIMU WA WAGOMBEA BINAFSI HAPA NCHINI AMBAO HAWATAPELEKESHWA NA VIONGOZI WAO