Nina mashaka kuna kikundi ndio kinaendesha nchi kwa sasa


Katuacha pabaya kwakweli kimyakimya
Sijawahi kusikia Rais yeyote ambaye alipata kuongoza hii nchi... Na hakupata lawama... Hata mmoja...! Mwinyi alionekana hana lolote, anaendeshewa nchi na "familia" yake, Mkapa aliitwa mbabe, na akakosolewa sana na sera ya ubinafsishaji, kuuza nyumba za serikali bei chee,Kikwete aliwahi kusemwa kuwa ni kama boksi tu, au nazi, aliyefuata naye alikuwa haambiliki, asiyetumia ushauri wa wanataaluma, katili, aliyenyima uhuru wa vyombo vya habari... Na sasa huyu mama...

Hitimisho weka mwenyewe hapo.
 
Hakuna rais atakayekuja kuwa maarufu na kupendwa hadi amzidi hayati Magufuli, Samia yuko poa ila hamfikii Magufuli lakini mama hana tatizo, msimlinganishe na viwango vya wengine
Kipimo cha mapenzi ya watu kinapimwaje... Hebu fafanua hapo mkuu!
 
Sio mashaka ndivyo ilivyo
Huyu anafanya a mild to highly rated investigation juu ya kujua kinachoendelea baada ya kazi yao kufanikiwa. Inatengenezwa cover kuwalinda wahusika wakuu kwa kuforge narrative za kuongoza mawazo ya watu juu jambo fulani wanalolijua barabara.

Ukirejea posts zake za 2019-2020 utaelewa ninachokieleza!!!

Ha ha ha aaaaaa! Naona kastuka, huyo huyo...anachungulia ha ha haaaa tumekwishakuona ha haaaa!
 
Pamoja na mapungufu yake, JPM alikuwa ana uwezo wa kumiliki maamuzi yake katika kila jambo. Hili lilimfanya ajiamini na kusimamia mawazo/maamuzi yake hata kama yalipingwa na ulimwengu mzima.

Sasa kwa mama yetu ni kama vile haamini bado kuwa yeye ndie raisi, ni kama vile hajui nguvu aliyokuwa nayo na mbaya zaidi ni wazi kaweka bayana kwa washauri wake kuwa hana dira. Hili linawapa nguvu wasaidizi wake kufanya maamuzi bila kumshirikisha ipaswavyo ama kupindisha uhalisia hasa wa athari ya maamuzi hayo. Hii inamgharimu mama pale athari inapokuwa hasi, inabidi kutoa kauli kutuliza jazba ambapo in reality linafikirisha juu ya alikuwa wapi mambo yakiamuliwa.

Japo kuna baadhi ya watu watapinga kwa vile wamampenda mama, ila ni wazi mama hajui anakokwenda, hana dira na hana kauli katika maamuzi yake.

Mama amekuwa mithili ya mtoto ambae kanunuliwa vitu vya kuchezea na kupangiwa leo utachezea hiki na kesho kile. Ni kwamba anamiliki vitu hivyo lakini hana mamlaka navyo mpaka mzazi aongee.

Kuna tofauti kubwa katika mazingira aliyoyapata madaraka JPM na Mama, Jaribu kupeleleza mara nyingi sana maraisi wanaongiani madarakani kwa njia kama aliyoingilia Mama ni ngumu sana kuweza kuiendesha serekali vizuri, huwa wanakosa ushawishi wa kutosha kwenye serekali ni lazima wa straggle.
 
nakubaliana na we

1-gazeti Uhuru rais hatagombea urais 2025

2-ugaidi wa kubuni wa bwana MBOWE

3-hamza hamza hamza

Jwt sijui wanasubiri nini wasomi kama wa guinea hawapo kweli watuokoe?

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Hitaji la Katiba Mpya mwangwi wake unazidi kusikika kuliko wakati mwingine wowote.

Kwa nje tu hivi ni kama kila kitu kinaenda sawa lakini kuna hali fulani ya taharuki ya kimya na sintofahamu kubwa ndani yake.

Ni kama kuna mambo yanapangwa huko halafu yanaletwa upenuni bila hata kueleweshwa vema

Kiongozi mkuu ni kama kawekewa mipaka mingi na kutengwa na hadhira.

Anahangaishwa huko na huko na kuwekwa busy kwa mambo ambayo yalistahili kufanywa na wasaidizi wake.

Kuna hofu fulani miongoni mwetu. Kuna uoga umewashika watu ni kama vile kuna jinamizi kubwa lisiloonekana linatuchungulia na kutufuatilia na kutusikiliza

Si kama nchi iko kwenye auto mode la hasha. Bali kuna kikundi cha wachache ndani ya mfumo pengine ndio kimeyateka mamlaka!
Watu hawasikiki lakini wapo

Watu hawaonekani lakini vitendo vyao unaviona!

Tunanyukwa kimyakimya!

Hii hali haina afya kwa taifa na haipaswi kuendelea kwa muda mrefu. Hawa wanaozungukana huko ndani hawana nia njema na taifa hili. Sinema si kwamba zimeisha bali zinaandaliwa zingine kutuweka busy tena tuyasahau haya!

Kama hizi hisia zangu ni kinyume na uhalisia basi napaswa kuonana na tabibu haraka! Ila kama si kinyume. MUNGU TUSAIDIE
Mabadiliko ya uongozi ni magumu kuliko unavyodhan..na pia kwa hii dunia ya 3 na mfumo dume unamfanya mama aongoze kwa tabu sana..kwa africa mama will always b mama hata ufanyaje...so ngumu kufurukuta huku kazungukwa na male dominance

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu,kuna kitu nahisi hakiko sawa kwa mama timu jk na magufuri camp,kuna za chini wanasema eti kuna timu ya pm inafanya kazi ya kumpangia hangaya safari nyingi haijajulikana kuna nini nyuma ya pazia

Kuna kitu kipo karibu kulipuka,kuna mgongano wa masirahi kila timu ina wakuu wa nchi

Tusubiri muda
 
Habari zenu wakuu,kuna kitu nahisi hakiko sawa kwa mama timu jk na magufuri camp,kuna za chini wanasema eti kuna timu ya pm inafanya kazi ya kumpangia hangaya safari nyingi haijajulikana kuna nini nyuma ya pazia

Kuna kitu kipo karibu kulipuka,kuna mgongano wa masirahi kila timu ina wakuu wa nchi

Tusubiri muda
Tulia wewe hayo ni maneno ya kimajungu tu
 
Back
Top Bottom