Nina mashaka kama wana-JF wanazijua kanuni za bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nina mashaka kama wana-JF wanazijua kanuni za bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisanduku, Nov 18, 2010.

 1. K

  Kisanduku Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua kuna tabia ya mtu kuwanyooshea vidole wengine bila kwanza kujiangalia. Nimeangalia thread nyingi zikieleza ukiukwaji wa kanuni za bunge hata kabla halijatimiza wiki mbili.

  Kweli spika na wenzake wanakosea. Nilidhani kukosea huko basi kila utaksoposoma post zetu basi tungeshuhudia vikimwagwa vifungu mbalimbali kuonyesha JF ni full thinkers and searchers kwelikweli.

  Badala yake vifungu ni haba na tunatajirishwa kauli nyingi za inferiority complex kama kusononeka, kukata tamaa, kuchukia, kusonya na mengine mengi ambayo hakuna mahala yaliwahi kuleta solution.

  Mimi naanza kwa na mashaka na uelewa wa kanuni hizi za bunge. Si mashaka kwa spika na wabunge. La hasha. Hao tumeshona Tundu Lissu, Mnyika, na Zitto walivyowaumbua na nina hakika wataendelea kuwaumbua waishie kutoa macho na kauli kali.

  Mashaka yangu ni kwa wengi wa wana-JF wenyewe humuhumu ambayo yataondolewa kwa kunimwagia jinsi tunavyopangua ukiukwaji wa bungeni kwa kujadili vifungu sahihi.

  Kwani nimeshuhudi humu mtu akileta vifungu tunakaa kimya kwa post ile na tunaendelea kujikita na yale niliyoyaeleza.
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hiyo ni sawa lakini kumbuka hii inahitaji muda na nia kuvijua,na hapo ndiyo tunapishana kutoka mtu mmoja mpaka mwingine!!
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wewe umenukuu kifungu gani kwenye mwanzo wa paragraph ya pili ya bandiko lako?

  Kama "great thinker", huwezi kuanza kwa kuandika kwa "ni kweli hivi na hivi.." halafu baada ya "nukta" unaanza sentensi nyingine kwa kuandika "nadhani hivi na hivi.."

   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wengi hatuzijui, ni ushabiki tu umetujaa
   
 5. K

  Kisanduku Member

  #5
  Nov 18, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ningeshangaa swali kama lako lisingekuja nidyo sababu nikafanya makusudi kusema nimerejea thread kadhaa zinazonyamazisha watu kwa sababu ya kanuni.

  Kwa kuanzia ninakupa thread moja ifuatayo:

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/88311-spika-huadhibiwa-kwa-utaratibu-gani.html

  Mkuu, kuhusu kukosea nadhani ukirejea alivyokiri Attonney General itamaliza kila kitu. na hata mzee wa vijisent hakukataa kwamba kanuni kupindishwa bali alimuelekeza Zitto na Mnyika wasome utaratibu wa kulalamika kwenye kanuni namba 5(4) inayosema hivi:

  ...Mbunge yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika anaweza kuwasilisha sababu za kutokuridhika kwake kwa Katibu wa Bunge ambaye atawasilisha malalamiko hayo kwa Spika....

  Baba_Enock, upo hapo?
   
Loading...