Nina laki 9, nifanye biashara gani?

Kijana kwanza hongera kwa mapambano hayo. Ningekushauri ufanye hili kama utapenda inaweza kukusaidia sana.
Nenda Mwanza, panga chumba miezi 3 cha elfu 15 kwa mwezi, chukua godoro la 50elfu. Hapo utakuwa umetumia laki moja.

Pesa iliyobakia nenda kisiwani, ulizia kisiwa cha Bwiro, nenda kule unakuwa unanua samaki wabichi kisha unawabanika, kuna wamama wanafanya kazi hiyo ya kubanika unawalipa kidogo sana.

Samaki wakavu utakuwa unawaleta Mwanza mjini kisha unawauza kwa bei ya JUMLA na kisha unarudi tena kisiwani kuchukua mzigo. Mtaji wa laki tano unatosha kabisa kufanya biashara hii na utapiga faida sana.

Unaweza pia kuwa unawabanika samaki kisha unawapeleka migodini Geita kule utawauzia mama Ntilie kwa faida nzuri sana.

Kama hii biashara utaiona ngumu unaweza kusema hapa kisha nitakushauri biashara nyingine.

Mungu akutangulie.
Hili jibu utakuwa umesaidia weng sana
 
Sijui ni kushauri ufanye biashara gani lakini ushauri wangu ukipata biashara ndogo ngogo(najua hio900k huwez kupata biashara kubwa) target ya biashara yako iwe ni kupata mtaji wa kiasi Fulani yaani hio biashara isiwe ndio kiendesha maisha yako utajikuta miaka kibao Upo na kabiashara hako hako hauendi popote

Sio kwamba usitumie laah tumia lkn kuwa na lengo kwamba hadi ukifika mwaka fulani au mwezi Fulani niwe na kiasi fulani nifanye biashara kubwa fulani
 
Kijana kwanza hongera kwa mapambano hayo. Ningekushauri ufanye hili kama utapenda inaweza kukusaidia sana.
Nenda Mwanza, panga chumba miezi 3 cha elfu 15 kwa mwezi, chukua godoro la 50elfu. Hapo utakuwa umetumia laki moja.

Pesa iliyobakia nenda kisiwani, ulizia kisiwa cha Bwiro, nenda kule unakuwa unanua samaki wabichi kisha unawabanika, kuna wamama wanafanya kazi hiyo ya kubanika unawalipa kidogo sana.

Samaki wakavu utakuwa unawaleta Mwanza mjini kisha unawauza kwa bei ya JUMLA na kisha unarudi tena kisiwani kuchukua mzigo. Mtaji wa laki tano unatosha kabisa kufanya biashara hii na utapiga faida sana.

Unaweza pia kuwa unawabanika samaki kisha unawapeleka migodini Geita kule utawauzia mama Ntilie kwa faida nzuri sana.

Kama hii biashara utaiona ngumu unaweza kusema hapa kisha nitakushauri biashara nyingine.

Mungu akutangulie.
Habari mkuu
Asante kwa kushare fursa na vijana wenzio
Hakika nami nimevutika na hii fursa uliyoshare hapa
Na nina mpango wa kwenda mwanza hv karibuni kwa sasa nipo dar
Nina maswali kidogo naomba kuuliza

Hiko kisiwa cha bwiro gharama kwenda huko ni kiasi gn tokea mwanza mjini

Na kinaitwa bwiro au bwiru
Nimejalibu uliza wenyeji wanashindwa tambua jina
Pia kama hutojali ungesaidia kuelekeza jinsi mtu akiwa pale mwanza mjini anaweza fikaje huko
 
Ingia kwenye maduka ya urembo, kama soksi za watoto, soksi za watu wazima, dai, rangi za viatu, kamba za viatu, vijiko, mafuta ya kujipaka, dawa za meno, miswaki, chujio,malapu lapu ya kuogea; brashi za viatu, jagi za plastic, karai ndogo, vikombe vya chai,kontena za chakula,

Vitu hivi vyote, nunua zile ambazo dazani yake yaani pc 12, haizidi 4500.

Ukishanunua hizo bidhaa, nenda katafute spika inauzwa kati ya shilingi 35,000/40000. Kuna za kuchaji na za kuweka betri, utachukua ambayo unaona ni rahisi kwako.
Kisha nenda sokoni na huo mzigo wako, Mwaga hizo bidhaa chini tangaza kila bidhaa 500, tu. Halafu ulete mrejesho.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Habari mkuu
Asante kwa kushare fursa na vijana wenzio
Hakika nami nimevutika na hii fursa uliyoshare hapa
Na nina mpango wa kwenda mwanza hv karibuni kwa sasa nipo dar
Nina maswali kidogo naomba kuuliza

Hiko kisiwa cha bwiro gharama kwenda huko ni kiasi gn tokea mwanza mjini

Na kinaitwa bwiro au bwiru
Nimejalibu uliza wenyeji wanashindwa tambua jina
Pia kama hutojali ungesaidia kuelekeza jinsi mtu akiwa pale mwanza mjini anaweza fikaje huko

-Kisiwa kinaitwa Bwiro siyo Bwiru
-Nauli kufika ni sh.5000/= ila ukilialia 4000 wanachukua
-Unapanda boat pale Mwaro wa Kirumba, boat zipo kampuni 2; Umia Ujae na Nyachijanja. Zote zimeandikwa Mwanza-Serema.
-Ukifika kule gharama ya kulala guest ni 3000 hadi 2000 unapata.

Jihadhari kuna mabinti sana kule kwa hiyo unaweza kuliwa pesa hadi ukarudi na shati tu na ndala.

Mungu akutangulie.
 
Kijana kwanza hongera kwa mapambano hayo. Ningekushauri ufanye hili kama utapenda inaweza kukusaidia sana.
Nenda Mwanza, panga chumba miezi 3 cha elfu 15 kwa mwezi, chukua godoro la 50elfu. Hapo utakuwa umetumia laki moja.

Pesa iliyobakia nenda kisiwani, ulizia kisiwa cha Bwiro, nenda kule unakuwa unanua samaki wabichi kisha unawabanika, kuna wamama wanafanya kazi hiyo ya kubanika unawalipa kidogo sana.

Samaki wakavu utakuwa unawaleta Mwanza mjini kisha unawauza kwa bei ya JUMLA na kisha unarudi tena kisiwani kuchukua mzigo. Mtaji wa laki tano unatosha kabisa kufanya biashara hii na utapiga faida sana.

Unaweza pia kuwa unawabanika samaki kisha unawapeleka migodini Geita kule utawauzia mama Ntilie kwa faida nzuri sana.

Kama hii biashara utaiona ngumu unaweza kusema hapa kisha nitakushauri biashara nyingine.

Mungu akutangulie.
Good idea
 
-Kisiwa kinaitwa Bwiro siyo Bwiru
-Nauli kufika ni sh.5000/= ila ukilialia 4000 wanachukua
-Unapanda boat pale Mwaro wa Kirumba, boat zipo kampuni 2; Umia Ujae na Nyachijanja. Zote zimeandikwa Mwanza-Serema.
-Ukifika kule gharama ya kulala guest ni 3000 hadi 2000 unapata.

Jihadhari kuna mabinti sana kule kwa hiyo unaweza kuliwa pesa hadi ukarudi na shati tu na ndala.

Mungu akutangulie.
Hahahaha umenifurahisha eti unaweza rudi na ndala

asante kwa maelekezo mazuri boss
Nitayafanyia kazi
Lkn kama hutojali nisaidie mawasiliano yako PM
 
Back
Top Bottom