Nina laki 9, nahitaji skrepa ya Prado niikarabati

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
May 4, 2022
1,181
1,574
Habari za majukumu, nina fedha isiyo taslimu shilingi laki tisa(900000 TZS), ambayo itakamilika kufikia mwezi wa 10 mwaka huu. Nimewiwa kununua usafiri wangu ila nimeamua kutumia njia tofauti kidogo.

Yaani kama ni hesabu za kugawanya, basi tungesema nimetumia njia fupi. Kwa jiji hili la DSM usafiri ni changamoto kubwa mno, hasa local transportation of passengers(usafiri wa hapa hapa Dar).

Naomba kama kuna mtu atakuwa na skrepa au anamfahamu mtu au taasisi yenye skrepa hizo, basi tuwasiliane na atoe details hapa. Ili kila mmoja aone na afahamu hivi vitu.

NB: nahitaji new model, au hata ya mwaka 2020 kulingana na series za matoleo yake.

Karibuni sana!
 
Boss, kwanini iyo mia 9 usingenunua Bodaboda tu ukaitumia kwa usafiri kama lengo ni kukwepa “kero” ya public transport.

Sijakukejeri pesa yako kubwa lakini nawaza kupata hiyo Prado, gharama za kuirepair, na uendeshaji wake, itakua bei juu.

Turudi kwenye topic: Jaribu tembelea sehemu zenye wanachinja magari au magereji kuna magari yaliopata ajali.
 
Habari za majukumu, nina fedha isiyo taslimu shilingi laki tisa(900000 TZS), ambayo itakamilika kufikia mwezi wa 10 mwaka huu. Nimewiwa kununua usafiri wangu ila nimeamua kutumia njia tofauti kidogo.

Yaani kama ni hesabu za kugawanya, basi tungesema nimetumia njia fupi. Kwa jiji hili la DSM usafiri ni changamoto kubwa mno, hasa local transportation of passengers(usafiri wa hapa hapa Dar).

Naomba kama kuna mtu atakuwa na skrepa au anamfahamu mtu au taasisi yenye skrepa hizo, basi tuwasiliane na atoe details hapa. Ili kila mmoja aone na afahamu hivi vitu.

Karibuni sana!
Imebidi nicheke Kwanza 😅😅

Una 900k alafu unataka Prado uvimbe nalo mtaani,umechoka usafiri wa udhalilishaji daladala 😅😅...Yani si Tu kwamba unataka kigari chochote cha bei rahisi km stallet,Bali wewe unataka Prado Kwa laki 9 hahaha..labda Prado la matope ndy utauziwa ukarikarabati
 
ukiwa na buku unapata hii gari na maongezi yapo,bei inapungua..pm ipo wazi
IMG_20220525_181905.jpg
 
Boss, kwanini iyo mia 9 usingenunua Bodaboda tu ukaitumia kwa usafiri kama lengo ni kukwepa “kero” ya public transport.

Sijakukejeri pesa yako kubwa lakini nawaza kupata hiyo Prado, gharama za kuirepair, na uendeshaji wake, itakua bei juu.

Turudi kwenye topic: Jaribu tembelea sehemu zenye wanachinja magari au magereji kuna magari yaliopata ajali.
Hata huko hapati hio ni mei ya bampa la nyuma bila reflectors tena liliotumika saana bongo
 
Mpaka muda huu sielewi kama Watanzania wengi ni mbumbumbu au la! Mada ni rahisi na ipo wazi mno, "nahitaji kwa mwenye kujua mahali wanauza skrepa za prado anielekeze" , ila bado watu wanatumbua tu macho na maswali ya kipuuzi.

Hivi WaTZ wamerogwa na nani? Au ulaji wa ugali ni chanzo? Yaani akili zimelala mno, na uchakataji wa taarifa ni 'very poor'.
 
Back
Top Bottom