Nina kinyongo muda mrefu sana moyoni, natamani kukitoa lakini sijui nifanyeje

Yaani bado. I am still grieving.

Sijui nifanyehe yaani. Ingekua naweza lipia pesa ili hii hali ipotee ningeshafanya hivyo. I feel sad about it.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pole sana pendomamtefu ila unakipaji cha uandishi na labda waweza kuwa mwandishi mzuri sana siku za usoni. Labda
By the way, pole tena kwa story yako na thats the pain of being a human, a phenomenal being. But why do you act that way? (Kumchukia sister Mary)... the answer is, “It suits you”
Ila nikusaidie.. talk to your inner YOU and tell your subconscious mind that you DONT HATE SISTER MARY ANYMORE. Not letting it go, that pain will torment your life forever and the worst part is, it wont kill you.

Do that and I tell you, it’ll be gone and finally finds happiness. All the best
 
Pole SANA...
Jaribu kutafakari...itapendeza ukisamehe...
Katika imani yako, omba na usali sana umsamehe...ikibidi shirikisha na viongozi wa dini...
Kinyongo ni cuando cha cancer, depression, heart diseases, high BP e.t.c

Msikilize T.D Jakes...
Msikilize Joel Osteen....
Wana clips nzuri sana...zitakazokufungua uone haina haja kuishi na kinyongo...

Besides, alishakufa..let it go!

Everyday is Saturday...................... :cool:
 
So niligraduate grade 7 mwaka 2004. Since ever sikuwahi wasiliana na Sista Shayo. Sista Mary nimekutana naye mara kama 3 hivi. Alihamishiwa shule ingine ya shirika huku Dar. Nikiwa chuo mwaka wa kwanza naingia U. E. 2011 nikapata taarifa kwa wenzangu kwamba Sista Mary amefariki. Yaani sikushtuka hata. Siku-blink hata jicho. Niliiogopa sana ile hali. Wenzangu wanahaha wataagia Luguruni Park pale kwa masista kwenda kuzika convent. Sikushtuka hataa wala kuhangaika. Moyo kama ulipata ganzi hivi. Wakaenda aga na wengine kuzika kabisa. Wala sikuwahi kuwazia kabisa msiba ule as if sitakufa pia.

Siku ya siku hatimaye ikafika nikawa nime-graduate chuo. Nikapata namba ya Sista Shayo. Nilitoka Dar na album yangu ya graduu. Just to go amd meet this woman. Nikaenda Christmas kijijini. It was amazing. Then sasa nikafunga safari to Arusha ambako alihamishiwa akiwa ameenda kuwa kama mhandisi kule. Yaani mbibi lakini balaa lake acha kabisa.

Nikanunua zangu vikoi viwili maana masista utawanunulia nini sasa? Nikafika nikapokelewa. Nililiaaa. Alifurahi mno kuniona nimefika angalau level aliyoitamani. She hugged me a lot. Tukapiga sana story. Anakumbuka watoto wote imagine. Wengine anajua progress zao wengine hajui na anashangaa kwanini hatukuwa in touch. Nikamfunika na moja ya kikoi nilichomnunulia. Akafurahi sana. Nami nikasema Mungu asante hata ninemkuta hai huyu bibi leo hii japo mimi siyo mpangaji wa uhai.

Katika story sijui ikawaje akamtaja Sista Mary. Nikawa mnyonge ghafla. Nikamwangalia kwa upole, nikamwambia, " UNAJUA NAMCHUKIA SISTA MARY JAPO AMEKUFA?" Alishtuka mno. Nikazidi kumsisitizia namchukia mno angali bado hayuko hai. Nikamwambia aliniumiza sana moyo wangu tukiwa shule. Alinidhulumu vingi vyangu. Aliinyanyasa nafsi yangu. Bado simpendi. Sista aliogopa mno. Nikamwambia kile kidonda bado kibichi sijui nitawezaje kumsamehe na kusahau. Nimejaribu sana lakini nimeshindwa. Nikamwambia pengine angekuwa hai ningemfuata nimweleze kuwa alinikosea jambo hili na lile na huenda angeniomba msamaha na mimi roho yangu ingekua nyeupe kabisa.

Nikaendelea kumwambia siwezi kudanganya nampenda wakati moyo wangu umejaa majeraha juu yake. Na hata sasa bado naumia. Sista alikosa la kuniambia. Akanambia jipe muda. Nikamwambia sawa. Basi bwana, last year tulitoka mzika babu kijijini tukapassby Arusha tumsalimie sista na hakuwepo alikua karudi convent coz alikua anaumwa sana na sukari na umri ukawa umeenda. Tumekuja kukaa kaa sijui August ile napokea taarifa za msiba wa Sista Shayo nikiwa ofisini. Jamani I cried kama mtoto na ukubwa wangu woote. Nililia sana sana sana. Nililia mnooo. Nilipewa mpaka ruhusa nikamzike sema home nako hapakua na watu walienda zika Moshi. I thank God I atleast wrapped her with those pieces of clothes. Walimu wangu wengi wema nao pale primary wamefariki wote kasoro wawili na sijui pa kuwapata niwashukuru angalau kwa kidogo. Most of them walikua tayari wameenda age.

SOMO LA KUJIFUNZA: WATOTO HAWASAHAU WEMA WALA UBAYA WALIOTENDEWA

USHAURI:
TUWE MAKINI SANA NA TUNAYOWATENDEA WATORO ZAIDI

MUDA NDIO KITU PEKEE HUPONYA JAPO SIJUI LINI NA SIJUI NIFANYE NINI ILI NILITOE JAMBO HILI MOYONI

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah... Touching ila kuna vitu vingine sio vya kufanyia kids, unakuwa unajenga moyo wa chuki na hasira, anyway huwezi deal nayo mara moja cz ni ya muda mrefu. Ila fanya hivi.

KILA SIKU TAFUTA UTULIVU WA PUMZI.
LIKE WAFANYA MEDITATION.

THEN SEMS NA NAFSI YAKO, NA MOYO WAKO, KUWA UNATAKIWA KUSAMEHE.

(JENGA REASON JI CONVINCE WEWE, Y UFANYE HIVO, MFANO, GOD AMESEM TUSAMEHEMEANE, USI MUUZI MUNGU, JIULIZ MASWALI NATAKIWA LIPA UBAHA KWA UBAYA? NTAKUWA NA TOFAUTI GANI NA GAIDI AU MCHAWI, MIM NI WEAK KIAS HIKO? ,etc)

FAnya hivo kila asubuhi, sio kwake tu. Kwa wote, ukiwa unasali pia. Weka kipengele cha KUTANGAZA MSAMAHA, KWA WALIO KUKOSEA.
 
Kwa sisi tulioishia la saba ina sound vizuri sana. yaani nimejiona nakijua kizungu hadi nikarudi kuangalia vizuri kumbe maneno mengi ni kiswahili ndo maana nimeelewa hivi.. Thank you sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, mim nilisomA seminari, mwanzo mwisho, kuna padre m1 alikua mnoko sana, simchukii ila simkubali had leo

Kuna clasmate wamekua mapadre ila haziiv had leo,

Am not regretin chochote, thats human nature
 
Mimi nimelelewa na bibi kuna aunt alikuwa ananitukana toka nikiwa mdogo yale maneno yalikuwa yananiumiza saana na siwezi yasahau siku moja nikiwa mkubwa hivi nilimtapikia yote yale maneno aisee hadi leo najisikia amani maana nilikuwa nikiyakimbuka nalia toka nimuambie moyo umekaa na amani

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha pole jaman na hongera umeweza kupona. Hongera sana. Poleee. Nami najua kwa wakati sahihi itakua poa tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana pendomamtefu ila unakipaji cha uandishi na labda waweza kuwa mwandishi mzuri sana siku za usoni. Labda
By the way, pole tena kwa story yako na thats the pain of being a human, a phenomenal being. But why do you act that way? (Kumchukia sister Mary)... the answer is, “It suits you”
Ila nikusaidie.. talk to your inner YOU and tell your subconscious mind that you DONT HATE SISTER MARY ANYMORE. Not letting it go, that pain will torment your life forever and the worst part is, it wont kill you.

Do that and I tell you, it’ll be gone and finally finds happiness. All the best
Yaan mpaka kesho najishangaaga kwanini nimekua hivi. Moyo wangu wa baridi saana juu yake. Ila all is well. Hakika ushauri wako ni mzuri na nitaufanyia kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole SANA...
Jaribu kutafakari...itapendeza ukisamehe...
Katika imani yako, omba na usali sana umsamehe...ikibidi shirikisha na viongozi wa dini...
Kinyongo ni cuando cha cancer, depression, heart diseases, high BP e.t.c

Msikilize T.D Jakes...
Msikilize Joel Osteen....
Wana clips nzuri sana...zitakazokufungua uone haina haja kuishi na kinyongo...

Besides, alishakufa..let it go!

Everyday is Saturday...................... :cool:
Tatizo niko sober balaa. Sijui naona kama bado yuko hai hivi. Lakini ni muda na mimi nipone na nimuachilie apumzike salama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah... Touching ila kuna vitu vingine sio vya kufanyia kids, unakuwa unajenga moyo wa chuki na hasira, anyway huwezi deal nayo mara moja cz ni ya muda mrefu. Ila fanya hivi.

KILA SIKU TAFUTA UTULIVU WA PUMZI.
LIKE WAFANYA MEDITATION.

THEN SEMS NA NAFSI YAKO, NA MOYO WAKO, KUWA UNATAKIWA KUSAMEHE.

(JENGA REASON JI CONVINCE WEWE, Y UFANYE HIVO, MFANO, GOD AMESEM TUSAMEHEMEANE, USI MUUZI MUNGU, JIULIZ MASWALI NATAKIWA LIPA UBAHA KWA UBAYA? NTAKUWA NA TOFAUTI GANI NA GAIDI AU MCHAWI, MIM NI WEAK KIAS HIKO? ,etc)

FAnya hivo kila asubuhi, sio kwake tu. Kwa wote, ukiwa unasali pia. Weka kipengele cha KUTANGAZA MSAMAHA, KWA WALIO KUKOSEA.
Asante sana mkuu. Ni vile labda hawana uelewa kwamba watoto pia huelewa wanayotendewa. Ubaya ni vile tunakua na hiyo mentality

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah, mim nilisomA seminari, mwanzo mwisho, kuna padre m1 alikua mnoko sana, simchukii ila simkubali had leo

Kuna clasmate wamekua mapadre ila haziiv had leo,

Am not regretin chochote, thats human nature
Speaking of that, kuna jamaa nakimbuka alikua anasomea upadre. Sikumbuki kama ni wa jimbo ama shirika. Kule alikosa kwa tabia zake mbaya. Sielewi mpaka leo imekuaje akaja pata upadre shirika lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pendomamtefu pole sana. Tujifunze kupitia andiko lako. Tuombe Mwenyezi Mungu atuepishe na dhambi hii ya kuwaumiza wengine kwa kuwanenea uwongo.

Nami hadi leo naishi kwa kuchukiwa na vijana ambao utotoni waliambia na wazazi wao kuwa mimi niliwaloga kwa kuwaendea kwa waganga, jambo ambalo sikulifanya.

Mwenyezi Mungu azidi kutupa nguvu na faraja wote ambao tumeteseka kihisia kwa kusingiziwa na binadamu wenzetu. Amin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa ulivyochanganya lugha,imekuwa tamu,jitahidi umsamehe,ukiwa kwenye maombi tamka msamaha kwake,mf mimi pendomamtefu nakusamehe sister mary kwa yote uliyonikosea,ukifanya hivyo kwa muda nafsi yako itamwachia nawe utakuwa huru( speak it loudly,announce the forgiveness, let your ears hear it)

Waseme, Ooh, thank you soo much dear. Umekua soo positive. Yaani sijuagi najisikiaje juu ya sista mary. Sijawahi kujua. Najua tuu moyo wangu uliingia baridi. Maybe siku nutaenda convent nukatembelee kaburini kwake huenda nitapata amani. I will go with flowers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom