Nina kazi lakini sina amani nayo...

Jing chu

JF-Expert Member
May 9, 2019
385
592
Wakuu bila shaka hamjambo!

Aisee! Mimi ni mfanyakazi wa shirika moja nafanya kazi kwa kuzunguka the whole week. Nachojishangaa hii kazi nahisi kabisa siitaki ila nafanya tu basi.

Kuna siku siendi nasingizia uongo wowote nashinda ndani. Kuna muda nahisi kama nimelogwa kabisa. Mshahara ni wa kawaida sio wa kulipa pango na kujenga yani ni hela ya kubadili mboga na kulipa kodi.

Sasa najiuliza nitaishi hivi hadi lini, nimejitahid kubalance angalau nifungue biashara lakini wapi. Kiufupi sina mood na kazi hii. Huu ni mwaka wa 2 tangu niajiriwe.

Najihisi vibaya kila ikifika asubuhi.

Wakuu naweza kuwa na tatizo gani?
 
Mkuu pole sana ni kawaida watu wengi wanafanya kazi ambazo hawapendi ila ni maisha tu inabidi ukomae. usiache kazi bila kazi maana utajua ni jinsi agani ilivyo kazi kuwa na stress wakati huna kazi.

Si unajua duniani usipojifunza utafunzwa, lakini usipojitunza hakuna atakayekutunza. Kuwa kama binamu usifanya move mpaka uwe na plan B, mkuu

Au ninasema uongo ndugu zangu?
 
Mkuu pole sana ... ni kawaida watu wengi wanafanya kazi ambazo hawapendi ila ni maisha tu inabidi ukomae. usiache kazi bila kazi maana utajua ni jinsi agani ilivyo kazi kuwa na stress wakati huna kazi.
Si unajua duniani usipojifunza utafunzwa, lakini usipojitunza hakuna atakayekutunza.
Kuna kama binamu usifanya move mpaka uwe na plan mkuu

Au ninasema uongo ndugu zangu?
Nimefarijika kusikia kwamba siko peke yangu.
 
Nimewaza weeee,,,,nimeandika nimefuta nimeandika nimefuta.....mwisho nimeamua niseme tu.

Kazi Kama huipendi Anza kutengeneza au kuandaa mazingira ya kuiacha ......Yani ufanye mpango wa mda mrefu wa kujiajiri
Ahsante mkuu yaani sina mood kabisa.
 
Yah ni wengi tu, mtu alikuwa na ndoto za kuwa engineer wa barabara, anaishia kuwa banker, mwignien alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa anaishia kuuza matunda, mwingine alikuwa ana ndoto za kuwa super model, ameishiwa kuwa bidada wa kupanda stejini akiwa amevaa kanga za wolper.
Kwa kweli ni utumwa aisee.
 
Vumilia kwa wakati huu lakini on the other side tafuta mbadala au kazi ambayo itakupa amani ya moyo, kumbuka makazini na mahali ambapo tunaspend muda mwingi kuliko nyumbani kwa hiyo kufanya kazi ambayo haikupi furaha its meaningless kwenye maisha, sema usiache kazi mpaka upate kazi nyingine
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom