Nina imani Yanga wataitoa Al Ahly kama watafanya yafuatayo

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Kwenye idara zote Yanga ina wachezaji wa viwango vya juu kabisa wa hadhi ya kiafrika. Haina tofauti na timu zote kubwa za Afrika ya weusi unazozifahamu kwa sababu wa viwango vya juu ya hapo tayari wako Ulaya.

Wanachopaswa kufanya Yanga ni :-
1) kutopumbazwa na magazeti yetu yanayitumia mbinu za kuiweka Yanga juu sana ya Al Ahly ili wauze magazeti kwa mashabiki wa Yanga ambao wengi hupenda sana kusoma mazuri ya timu yao. Yanga wanapaswa wajue Al Ahly ni timu kubwa na kali na hivyo waipe heshima inayostahili, wacheze nayo kwa umakini unaolingana na ukubwa na ukali huo lakini kwa kujiamini na bila kuwaogopa. Wasipumbazwe na magazeti kujiona wanacheza na timu ya kiwango cha Tanzania Prisons.

2) Kosa walilolifanya Yanga dhidi ya Watunisia mwaka jana lisirudiwe. Wageni walipokuwa baridi kutafuta sare ya ugenini na wenyeji Yanga wakawa na ubaridi huo huo, mechi ikamalizika kwa 1-1. Kwenye mechi ya marudiano ugenini, Yanga wakakipiga kweli kweli kwa sababu wenyeji walikipiga kweli kweli. Yanga ikalala 1-0 na kutolewa kwa 2-1 tu. Kama walivyocheza ugenini wangecheza hapa nyumbani, tungewatoa Watunisia.

3) Jumamosi Yanga wawe makini na tackling za ndani ya penalty box kwani wenzetu ni wajanja mno kumshawishi mwamuzi kwamba wamechezewa madhambi.

4) Wajiepushe sana kutengeneza mazingira ya kupata kadi nyekundu. Wenzetu ni wajanja sana kuchongea kwa mwamuzi kwamba kafanyiwa baya sana la kusababisha aliyemfanyia apate red card.

5) Mwisho tuwe waangalifu sana na offside zetu za kibongo. Wenzetu wanajua kuchomoka kasi wakishaona mpira umetoka mguuni mwa anayetanguliza pasi ya kwenda mbele. Tutabaki kunyoosha mikono, mtu anaenda kufunga tukiamini ni offside kumbe siyo kutokana na kuchezeshwa na wanaoijua kanuni hiyo.

Naamini kabisa Yanga ikijipanga vizuri itaitoa Al Ahly kutokana na kikosi imara cha mabingwa hawa wa Tanzania Bara.
 
Sikipendi kabisa kisingizio cha mapokezi yalikuwa mabovu, basi chakavu, uwanja mbaya wa mazoezi etc. Kwanini na nyie msiwapeleke hao Al Hilal wakafanye mazoezi kwenye uwanja wa TP Tandale Uzuri? Yanga kufungwa inajitakia.
©Bujibuji
 
Acha ujuha wewe Yanga haina uwezo wa kuifunga Al-Ahly. Kwa ligi ipi yenye ushindani? kwa uwekezaji upi? kwa aina ipi ya wachezaji ilionao?
Tumia akili mkuu. Jiongeze
 
Ndoto za mchana hizi, Al Ahly ni chama lingine kabisa zaidi ya Raja Casablanca.
Yanga lazima wakae, kumbuka refa sio wa TFF.
 
12592627_485031088369056_7823409023491016195_n.jpg
 
Back
Top Bottom